Ijumaa, 28 Oktoba 2011

UZINDUZI WA IBADA ZA JUMAPILI PENUEL CHRISTIAN CENTER KIGOGO (KWA MCH LINDE)


             Ibada ya ufunguzi wa kanisa la Penuel Christian centre linaloongozwa na mch Linde ilifanyika jumapili ya Tar 23/10/2010 katika kanisa hilo lililoko kigogo kwenye viwanja vya mpira. ibada hiyo ilitanguliwa na mkutango wa injili ulioandaliwa na zone no 3 ambao ulikusanya watu wengi wanaoishi maeneo ya karibu kuzunguka kanisa hilo na nguvu za mungu zilitawala na watu wengi waliokoka na kufunguliwa. Mkutano huo ambao ulihubiliwa na wainjilisti wawili akiwepo Mch. Mwalubalile wa TAG hananasifu.


Mkutano huo ulihudumiwa na waimbaji kutoka makanisa mbali mbali kama TAG Magomeni kwaya zote mbili Revival na Diodoxer, Kwaya ya TAG Hananasifu, Kwaya ya TAG Kwa Tumbo na waimbaji wengi binafsi akiwamo Godlucky na Mama Mch Linde. Watu wapatao 75 waliokoka katika mkutano huo na jumapili hiyo katika ibada ya asubuhiwatu wapatao 25 walihudhulia na nguvu za Mungu zilionekana wa watu wengi walifunguliwa kutoka katika vifungo vya nguvu za giza na kuna binti mmoja yeye alikutana na nguvu za Mungu akiwa nyumbani kwao wakati maombezi yakiendelea na kuletwa hapo kanisani nakufanyiwa maombi ambapo alifunguliwa kutoka katika vifungu vya shetani utukufu ni kwa Yesu.

 


Watu wakicheza wakati kipindi cha sifa mkutanoni

Mwinjilisti Mwalubalile akihubiri kwenye mkutano.

Mama Mch Linde akiimba kwenye mkutano.

Yesu anawapenda watu wote hata mateja nao walihudhulia kusikiliza mahubiri.
Kwaya ya Revival wakijianda kuimba
Wachungaji wa makanisa zoni no 3
Revival wakiimba wimbo wa imani
Wachungaji
Watu wakikata shauri kwenye mkutano.


            


Chapisha Maoni