Jumamosi, 20 Agosti 2011

JIAMINISHE MBELE ZA MUNGU ILI AKUAMINI

Shalom
Nianze na mfano ili kujenga hoja uweze kunielewa mimi nina mtoto wangu mdogo anakaribia miaka 2 nyumbani tuna simu zisizopungua 4. simu yangu nimenunua hivi karibuni ni mpya na ya thamani kwangu, mimi na mke wangu tunatambua hilo lakini mtoto wetu yeye hatambui hilo nasi twajua kweli hajui tofauti ya hizo simu hivyo sisi huwa tunamwachia aguse hizo nyingine na hii ya thamani huwa tunaiweka mbali nae na kama ikitokea akaigusa tunampokonja na kuiweka mbali. pamoja na hayo bado naamini kuwa ipo siku nitakuja kumwachia pale atakapo kuwa na kugungua kuwa kitu alichoshika ni cha thamani na hawezi kukiharibu maana ni cha thamani. 

sasa nirudi kwenye mada yangu baada ya kutoa mfano huu. sisi ni watoto wa Mungu na kila mtu anatumika katika shamba la bwana kwa sehemu yake mimi sijui wewe unatumika wapi ila wewe unajua. siku zote Mungu anakuza huduma zetu kutokana na ufahamu wetu kwa Mungu na ndiyo maana tunatofautiana katika huduma na hii haijalishi umekuwa kwenye wokovu kwa muda gani hasa bali ni jinsi gani unavyomfahamu Mungu wako.

yamkini wewe ulikuwa uwe mwimbaji kuliko hata Rose Mhando lakini kwa sababu Bwana hajakuamini kuwa unaweza kumwakilisha ipasavyo kwa watu wake uwezo huo amewapa wengine, au ungeweza kuwa mtu furani wa tofauti sana lakini haijawa hivyo. Biblia inasema amelaaniwa amtunikiaye Bwana kawa ulegevu! kwa maana nyingi Mungu anapenda watu wanao mtumikia kwa bidii kubwa na kuweka maarika katika kutumika kwao, wanaotumia hadi uwezo wao wa mwisho katika jambo wanalifanya katika Mungu, wanao fuata taratibu na sheria za Mungu.

hebu mfanye Mungu akuamini kwa kufanya kazi yake kwa bidii mpaka ajivunie kuwa yupo mtumishi anayetumika kwa nguvu zake zote kwa maana nyingine kuna vitu vya thamani naamini bado havijaachiliwa kwako ila akikuamini kuwa utavitendea haki basi Mungu ataviachilia kwako. wakati mwingine watu wameona huduma imekuwa ngumu na hata kuacha kile walichokuwa wakifanya na kufuata mkumbo kwa wengine wanacho kifanya sasa kama wote tukakuwa mitume nani atakuwa Mchungaji, au kama wote tutakuwa manabii nani atakuwa mwalimu tambua nafasi yako tumika kwa bidii ili kwa kupitia wewe Mungu autanue ufalme wake hapa duniani. jioaminishe mbele za Mungu ili akuamini kuwa unaweza na akutumie katika mambo makubwa kama alivyomtumia Musa, Elia, Elisha n.k

chao.  
Chapisha Maoni