MALENGO
1. Utangulizi
2. Jinsi ya kupata ujauzito
3. Jinsi ya kuzuia mimba
4. Kuhesabu Kalenda
5. Lini tuanze tendo la ndoa baada ya
kujifungua
6. Faida za uzazi wa mpangilio
7. Uzazi unapochelewa
Utangulizi
MWZ 1:27A zaeni mwongezeke mkaijaze
nchi.
Uzazi wa mpangilio (child spacing): ni sehemu
ya uzazi wa mpango ambapo wanandoa/wenza hupanga ,lini wapate mtoto /watoto wao
wa kwanza ,na wapumzike kwa muda gani , ili waweze kupata mtoto/watoto wanaofuata.
Uzazi wa mpango: ni tendo la wanandoa /wenza
kupanga na kuamua wawe na watoto
wangapi na ni kwa kipindi gani
Mambo mhimu
•
Wanandoa wafanye maamuzi
ni lini wapate watoto na idadi ya watoto wanao wahitaji
•
Kama watahitaji kuzuia mimba ,ni vema wakaenda hospitali
wakapewa ushauri na wataalamu
•
Uamzi wa kuchelewa kupata watoto ni vema ukazingatia yafuatayo:
Umri wa mke/mme (Wanawake
wanashauriwa kuzaa mpaka miaka 35,Zaidi ya hapo kunaweza kuwa na athari)
•
Uwezo wa kiuchumi
•
Fursa za kielimu zilizopo
mf. Kwenda masomoni n.k.
•
Kama mwanandoa anaugonjwa
sugu mf Kisukari n.k.
Jinsi ya kupata
ujauzito
Ujauzito
hupatikana pale mbegu ya mwanaume iliyo
kwenye shahawa ikikutana na yai la
mwanamke lililoko katika mfuko wa uzazi
Kitaalamu
mwanamke yeyote ambaye hajazuia mimba kwa namna yoyote na
yupo kwenye mahusiano ya kindoa anatakiwa abebe mimba ndani ya mwaka
mmoja.
Jinsi ya kuzuia mimba
ziko njia
kdhaa za kuzui mimba:
•
Njia zote zina faida na maudhi madogomadogo
•
Ni vyema tukaambiwa hospitali kuliko kusikiliza maneno ya
mtaani
•
Tusitumie njia yoyote ya kuzui mimba bila ushauri wa
kitaalamu
•
Siyo kila njia itamfaa mtu ,kila mtu ana njia yake kulingana
na mwili wake
Njia
mbalimbali zinatumika kuzuia mimba ambazo ni njia za kisasa na asili:
Njia za kisasa
•
Njia za muda mfupi:
mfano sindano,vidonge na mpira wa kiume na wa kike (condom)
•
Njia za muda
mrefu: mfano kipandikizi,kitanzi
•
Njia za kudumu :
kufunga mirija ya uzazi kwa wanaume na wanawake.
•
Njia za asili ni kama vile:
•
kunyonyesha ndani ya
miezi 6 endapo mama ananyonyesha muda wote,hajaanza kuona siku zake,
•
kufahamu siku za hatari (i.e fertility awereness),
•
kutumia kalenda ,
•
kumwaga mbegu nje kwa wanaume
NB- Kwa
upande wa ndoa changa ni vema kuzuia mimba kwa kuhesabu kalenda (safe days).Kwa
sababu haitakuwa inaingilia mfumo wa
mwili na vichocheo (hormones) wakati wa siku za hatari tumieni
condom.
Kuhesabu Kalenda
•
Mwanamke hupata hedhi kila mwezi
•
Mzunguko unaweza kuwa mrefu zaidi ya siku 35, mfupi
siku 21 na mzunguko wa kawaida siku
28-35.
•
Siku salama ni siku zisizokuwa na uzazi
•
Siku hatari ni siku zenye uzazi
•
Yai hupevuka siku 14 kabla ya kuona hedhi yako (Ovulation)
Mfano kama
mzunguko wako ni siku 21 yai litapevuka
siku ya 7, na kama ni siku 35 itakuwa ni siku ya21 nk.
Ili
kutumia njia hii mama ni lazima awe na mzunguko wa kueleweka (regular cycle) na
ajue mzunguko una siku ngapi.
Siku
zisizokuwa na uzazi zitakuwa siku tatu baada na kabla ya yai kutoka katika
hedhi
Dalili za kupevuka kwa yai (Ovulation)
•
Joto la mwili hupanda kidogo siyo homa (0.5-1)
•
Kuongezeka hamu ya tendo la ndoa
•
Maumivu ya tumbo chini ya kitovu kwa upande mmoja yaani
kushoto au kulia.
•
Matiti kuuma kidogo
•
Ute huwa mwingi ukeni kama
ute mweupe wa yai,na huvutika sana.
Lini tuanze tendo la ndoa baada ya kujifungua
•
Baada ya kila
uzazi mwanamke hutokwa na damu/uchafu
(lochia) ambayo kwa wengine huchukua hadi wiki sita
•
Kwa wanawake wanaojifungua kawaida ,baada ya wiki sita
wanakuwa tayari wamepona.
•
Kwa wanawake wanaojifungua kwa upasuaji,kidonda kinapona
ndani ya wiki sita na maumivu ya tumbo yanakuwa yameisha, hivyo wanaweza kuanza
tendo la ndoa . Kama tumbo linauma unashauriwa kwenda hospitali kutibiwa
Mwanamke
yeyote ambaye ananyonyesha kidogo au hanyonyeshi anaweza kupata ujauzito kuanzia wiki 4-6
baada ya kujifungua.
•
Unashauriwa kuwaona wataalamu kabla ya kuanza tendo la ndoa.
•
Shauriana na mwenzi wako ni lini mnataka kupata mtoto
mwingine, kabla hamjaenda kwa mtaalam.
•
Ni vizuri wote mke na mme mkaenda pamoja kupata ushauri.
UMUHIMU WA UZAZI WA MPANGO
•
Uzazi wa mpango hupunguza vifo vya mama na mtoto
•
Hupunguza mimba zisizotarajiwa
•
Husaidia watoto kuwa na afya njema
•
Husaidia wazazi kujiandaa na kujiweka sawa kiuchumi
Muda mzuri wa kupata ujauzito
•
Kati ya miaka 18-34
•
Angalau miaka miwili (2)baada ya kujifungua
•
Angalau miezi sita(6
) baada ya kuharibika kwa ujauzito
Faida za Uzazi wa mpangilio
Uzazi wa
mpango una faida kubwa kwa mama na mtoto kama vile:
•
Kupata watoto wenye
afya nzuri na waliofikisha umri wa kuzaliwa.
•
Kupunguza vifo vya watoto wachanga
•
Afya ya mama kuimarika
•
Kipato cha familia kuimalika.
Madhara yatokanayo na mama kupata ujauzito wa mara kwa mara
•
Kupata mtoto mwenye uzito mdogo
•
Kuzaa mtoto njiti
•
Vifo vya watoto wachanga.
•
Kupasuka kizazi wakati wa kujifungua na pengine kupeleke
kifa kwa mama
Uzazi unapochelewa
•
Hiki ni kipindindi ambacho mwanamke anashindwa kupata
ujauzito baada ya mwaka mmoja ,akiwa
anaishi na mwenzi wake ,muda wote na hajatumia njia yoyote ya uzazi wa mpango
•
Baada ya mwaka mmoja wanashauriwa wote wawili mke na mume
,kwenda hospital kupima,
•
Mume anatangulia kupima mbegu zake,akionekana hana
tatizo,mke naye hupimma (vipimo vya mwanamke vinauma sana),lazima tuwe na
uhakika kuwa mme yuko vizuri.
Katika
swala zima la ugumba wanaume huchangia 40%,wanawake 40% na 20% ni kwa wanandoa
wote.
Angalizo -Ni lazima
mme akapime
-Ni vema kwenda hospitali badala ya
kwenda kwenye tiba mbadala
-Kama wanandoa hawaishi pamoja
wanahitajikukutana wakati wa siku za hatari.
HITIMISHO
-
Watoto kwetu ni zawadi bali ni urith kwa Bwana
-
Sala na Hana walipitia katika jaribu hili lakini walishinda,
hilo ni jaribu lako kuna mlango wa kutokea.
-
Kanisa tuwe washauri wazuri na kama tumeshiriki katika
kunena vibaya tutubu.
MUNGU
AWABARIKI
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Maoni 1 :
Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe cha kusimama peke yangu bila mwili wa kusimama na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na Dk DAWN, baada ya kumwambia. kuhusu hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kiukweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi huku akiniomba kuwa hatoniacha kamwe. tena. Miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
* upendo
inaelezea * inaelezea kivutio
* kama unataka ex wako nyuma
*acha talaka
* kuvunja obsessions
* huponya viharusi na magonjwa yote
* uchawi wa kinga
*Ugumba na matatizo ya ujauzito
* bahati nasibu
* uchawi wa bahati
Wasiliana na Dk Ediomo kwenye barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp:+2349046229159
Chapisha Maoni