Jumanne, 21 Februari 2017

KUAMINIWA na WATU


BWANA akamwambia Musa, Tazama, mimi naja kwako katika wingu zito ili watu hawa wasikie nitakaposema nawe, nao wapate kukuamini wewe nawe hata milele. Musa akamwambia BWANA hayo maneno ya watu” (Kutoka 19:9). 
Kama kuna jambo linaweza kukuumiza maishani ni kupoteza KUAMINIWA, hasa kuaminiwa na watu wa KARIBU. Kumwamini mtu sio kitu rahisi, ila ni rahisi kupoteza imani kwa watu kwa jambo moja tu, tena la  kijinga kabisa na lisilo na tija yoyote ya maana!

Fiki unafanya jambo kwa kumaanisha kabisa, kwa roho safi, lakini watu hawakuamini! Unasema KWELI kabisa, lakini watu wanaona UNAWADANGANYA tu! Tena wanakukebehi; Kumbe! Ni kwa sababu ulipoteza uaminifu wako kwao! Hiyo inauma sana. Hapo ndipo utaelewa umuhimu wa KUAMINIWA na watu.

Sio kila mara utaaminiwa kwa maneno au matendo yako peke yake, Kuna wakati unahitaji msaada wa “mwingine” ili uaminiwe. Mungu akaona afanya jambo maalumu ili Musa aaminiwe na watu milele!  

Halikadhalika, hata sisi tunahitaji Mungu au watu wengine watusaidie kuaminiwa kwetu. Kwa mfano, usipuuze mtu anayeweza kusema habari zako nzuri mbele ya watu wengine, hasa kama ukiwa haupo, huyu anaongeza imani ya hao watu kukuamini wewe. Kwa upande mwingine, mtu akisema habari zako mbaya kwa watu wengine, huyo amekufanyia uharibifu mkubwa; hasa akiwa ni mtu wako wa karibu. Imani yao kukumini wewe inaathirika; hata kama una majina yako matukufu, hutaaminiwa tena.

Mara nyingi sana watumishi wa Mungu wanadhani kigezo cha kumtumikia Mungu pekeyake kitawapa KUAMINIWA au KUHESHIMIWA na watu! Ndio maana unaweza kukuta mtu akijitetea, “mimi ni mchungaji”, “mimi ni mtumishi wa Mungu”, nk., lakini watu hawawaamini hata kwa maneno yao mazuri!

Mungu alijua watu wanamwamini Yeye kama Mungu, lakini aliona UMUHIMU wa Musa mtumishi wake “naye” kuaminiwa na watu! Safari hii, Mungu alishuka katika wingu ili watu wamwamini Musa, sio watu wamwamini Mungu.

Sasa angalia jambo hili, Musa hakuomba neno hili; Mungu ndiye aliona afanye hivyo kwa MASLAHI ya Mungu sio kwa maslahi ya Musa, japo anayeaminiwa hapo ni Musa!


#Frank_P_Seth


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Hakuna maoni: