This
is automatic! Ukianza ku-focus kwa Mungu na kuondoa moyo wako kwenye mambo yote
yanayomchukiza Mungu, Mungu naye anaanza ku-focus kwako na KUJA karibu yako.
Wewe unakuwa kivutio kwa Mungu kama sumaku. Hapo ni bila kuomba chochote wala
kumwita Mungu; Atakuja tu.
“Kwa maana macho ya BWANA hukimbia-kimbia
duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo
kuelekea kwake” (2 Nyakati 16:9).
Na,
ukiondoa focus kwa Mungu, na kuhamishia MOYO wako kwa mtu au miungu mjngine;
Mungu anaondoka bila kufukuzwa, tena bila kuaga! Hii ndio maana halisi ya wivu;
Mungu ni mwenye wivu!
“BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule
amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake
amemwacha BWANA” (Yeremiah 17:5).
Kumbuka
KANUNI hii, “Mkaribieni Mungu, naye
atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha
mioyo yenu, enyi wenye nia mbili” (Yakobo 4:8) - WEWE ndio unaanza
KUMKARIBIA Mungu ili YEYE akukaribie wewe; Unafanya hivyo kwa KUULEKEZA moyo
wako kwake na kufanya mapenzi yake. Hapo UTANASA yale macho ya Mungu yanayo
kimbia-kimbia duniani mwote kusaka watu wa namna hii.
Chagua
leo, unataka UKARIBU na Mungu au na MTU (miungu mingine)? Kisha chukua hatua.
Frank
P. Seth
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni