“1 Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa
lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na
Samaria, isipokuwa hao mitume. 2Watu watauwa wakamzika Stefano, wakamfanyia
maombolezo makuu. 3Sauli akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na
kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani. 4Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno”
(Matendo ya Mitume 8:1-4).
Kuna
awamu tatu muhimu za ukristo ambazo ukiwa dunuani imekupasa kuzipitia na kutoa
hesabu yake. Hatua hizi ni: kuzaliwa, kukua na kuzaa.
i.
KUZALIWA
Ukristo
unaanza na kuzaliwa kwa mara ya pili, kwa kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi
wa maisha yako. Kwa tafsiri nyingine, hii inaitwa “kuzaliwa kwa maji na kwa Roho” (Yohana 3:1-6). Hili huwa zoezi
rahisi tu kama ukiamua leo, “Kwa maana
kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu”
(Warumi 10:10).
ii.
KUKUA
Mtoto
azaliwapo, hunyeshwa maziwa safi (yasiyoghoshiwa/yasiyotiwa maji) ili aweze
kukua vizuri. “Kama watoto wachanga
waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo
mpatekuukulia wokovu” (1 Petro 2:2). Hii ni hatua ya muhimu sana ya Mkristo
ya KUTAMANI kujifunza neno la Mungu ili aweze kukua.
Kiwango
tofauti cha KUTAMANI maziwa hupelekea watoto wa kiroho kukua kwa KASI tofauti.
Ndio maana ndani ya kanisa utakuta watu wawili, mmoja anamiaka kumi kanisani
lakini bado analishwa maziwa tu wala hajakua popote. Mwingine ana mwaka mmoja
lakini ameshakomaa kiasi cha kuanza kuzaa! Hii yote ni UAMUZI wa mtoto husika,
je! Unatamaini MAZIWA?
iii.
KUZAA
Kazi
ya kondoo ni KUZAA kondoo wengine. Kazi ya mchungaji ni kulisha kondoo ili
wakue, tena kwa kusudi maalumu. Kondoo asipozaa huyo huondolewa kundini mapema
kwa maana hana faida kwa mchungaji, tena yamkini, huharibu na kondoo wengine.
Angalia
tena kwa namna hii, kama BWANA Yesu ni mzabibu, na sisi ni matawi; maana yake
tuko kwake tayari, yaani tumevuka hatua ya kuzaliwa na tunaendelea kukua,
lakini kuna hatua ya kuzaa matunda inakuja hapo. Akiona tawi LISILOZAA, Yeye
hulikata! Na lile lizaalo hulisafisha ili liweze kuzaa zaidi (Yohana 15:1, 2).
Lengo la kubaki kwenye mzabibu ni kuzaa!
Ukiangalia
Matendo ya Mitume 8:1-4, utaona jinsi ambavyo kanisa liliongezeka kwa ‘kondoo
kuzaa kondoo’ kwa sababu baada ya kufanyika WANAFUNZI wa Yesu (wakristo), chini
ya mitume, ilibidi watawanywe kwa nguvu ili wakazae huko waendako. Mitume
(wachungaji) wakabaki Yerusalemu, kondoo (waumini) wakaenda kuhubiri injili na
kuzaa matunda (waumini wengine) huko walikokwenda.
Ni
jambo lililozoeleka kwa nyakati hizi kwamba kazi ya kuzaa kondoo ni ya
mchungaji (viongozi wetu wa kiroho), kisha kuwatunza na kuhangaika tena kuandaa
mikutano na seminia za kiroho ili kuzaa tena na kukuza wachanga. Wakrito
(kondoo) wamekaa tu kanisani wanaingia na kutoka jumapili kwa jumapili; hawazai
kitu! Hii sio sawa.
Kumbuka,
“shoka limekwisha kuwekwa penye mashina
ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni”
(Mathayo 3:10). Bwana akikutazama anakuombea kwa BABA kwamba upewe mwaka huu
tena kama utazaa au la, na anakuwekea mbolea (unapata mafundisho mbalimbali na
huduma zingine za kiroho), ili uzae; lakini usipozaa utakatwa tu kwa maana
unaiharibu nchi. Tena sio kuzaa tu, unatakiwa kuzaa matunda MAZURI.
Angalia
jambo hili, mitume walizaa wakristo wengi kwa KUSHUHUDIA habari za Yesu.
Walijiita mashahidi. Yaani, WALISEMA yale waliyoona na kusikia kwa Bwana, hayo
wanawaambia na wengine ili waamini (Matendo 22:15). Je! Wewe umewashuhudia
wangapi?
Watu
wengi wamejifariji kwamba kutoa SADAKA inatosha. Angalia, kutoa sadaka ni
muhimu, lakini je! Wewe ni SHAHIDI wa BWANA? Kama wewe ni kondoo, ni vyema, ila
swala ni KUZAA sio kutoa sufi (sadaka) tu, kuzaa ni LAZIMA!
Kila
mtu anajua kwamba mti unafaida nyingi, kwa mfano: kuni, mbao, kivuli, nk.
Lakini mwenye shamba anataka MATUNDA kwanza! Tunajua unavipawa vingi na unatoa
sadaka nyingi kanisani kwako, je! Umezaa kondoo? Hili ni swali la kujiuliza na
ni changamoto kwa kila mtu. Kumbuka, matunda ni ya kila msimu na yanatakiwa
yawe mazuri na ya mengi. Ndio maana tawi lizaalo
husafiswa ili lizae ZAIDI. Bwana anataka matunda zaidi; yaani kuongezeka katika
kuzaa mwaka hadi mwaka.
Jitathmini
umri wako wa kiroho. Kila siku unalishwa tu pale kanisani kwako. Je! Hukui tu?
Utazaa lini? Je! Unajua una MUDA ambao ukifika ni LAZIMA uzae? Ndio maana ule
mti ulipewa MUDA wa kuzaa kabla ya kukatwa. Jitahidi kuweka jambo hili kwenye
maombi na matendo kwa maana hukuitwa kupiga pambio, kusikiliza neno na kuandika
notsi tu pale kanisani kwako; leta matunda yako kwa mamana UNADAIWA. Au
unasubiri ulazimishwa kwa adha kama lile kanisa la mwanzo?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni