ISamuel 2:22 – 23
Basi Eli alikuwa mzee sana,;naye alisikia habari za mambo yote ambayo wanawe waliwatenda Wa/israel; najinsi walivyolala na wanawake waliokuwa wakitumika mlangoni pa hema ya kukutania. 23 Akawaambia mbona mnatenda mambo kama hayo? Maana nasikia habari za matendo yenu mabaya kwa watu hawa wote.”
Madhaifu ya Wazazi Yanayo Changia Kuwaharibu Watoto.
1. Mahusiano Mabaya ya Wazazi na Watoto Wao.
Eli kama mzazi,hakuwa na mahusiano ya karibu na watoto wake.
• Wazazi wengi leo wapo bize sana kiasi kwamba hawana muda kabisa wa kukaa na watoto wao nakuwajenga na kuwafundisha mambo ya msingi.
• Wanatumia muda mwingi kutafuta pesa na maisha huku wakisahau kubeba jukumu lao la kuwalea watoto na vijana wao katika maadili mema.
Mfano:
• Mtoto mdogo aliyemuuliza baba yake kama anaweza kumwamini House girl na kumpa hati za nyumba, mashamba na kadi za magari. Mzazi alisema hawezi kufanya kitu kama hicho cha kumkabidhi house girl vitu vya thamani kama hivyo.
• Mtoto alimuuliza baba yake kama hawezi kumwamini house girl na kumkabidhi vitu vya thamani kama vivyo, mbona baba ameyakabidhi maisha ya mtoto mikononi mwa house girl ayafanyie anavyo taka yeye??
• Mzazi alihukumiwa kwa maneno hayo na kujikuta akikosa kitu cha kujibu.
2. Tatizo la Wazazi Kutokujua Kinacho endelea katika maisha ya Watoto Wao.
Eli hakuweza kujua kilichokuwa kikiendelea kwa watoto wake mpaka alipokuwa akisikia watu wakisema nje.
• Wazazi wengi wa leo hawajui mambo ambayo watoto wao wanayafanya kila siku katika:
• Simu zao Mkononi,
• Kompyuta za watoto,
• Mashuleni kwenye vikundi mbalimbali ambavyo watoto wanashiriki,
• Vyumbani mwao n.k (Ndio maana wamarekani vyumba vya watoto hawaweki makomeo wala vitasa.
Vijana wengi wana sura mbili.
Suraya kwanza ni ile ya kuigiza nakujifanya yeye ni mtu mzuri hasa nyumbani na kanisani.
Suraya pili ni ile sura yake halisi ambayo huonekana hasa akiwa nje na marafiki zake hapo ndio huwa yeye katika uhalisia wake.
• Anatukana
• Anaiba
• Anakunywa pombe
• Anavuta sigara
• Anafanya uasherati nk.
3. Tatizo la Wazazi Kupelekea Watoto wao Kujivika Ngozi yakondoo.
Vijana wengi leo wana vaa ngozi ya kondoo wanapoingia mlango wa Kanisa au nyumbani, lakini huvaa ngozi ya mbwa mwitu wanapokuwa nje na nyumbani kwao.
Ni bora tuwafundishe watoto wetu maisha mazuri na faida zake ili wasivae tena ngozi ya mbwa mwitu bali wawe kama kondoo kuanzia ndani hadi nje.
4. Mambo hayo Hupelekea Kuchafua njia za Watoto wasifike kule waliko kusudiwa.
Zaburi 119:9
9Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwakutii, akilifuata nenolako.
Njiaza watoto wengi leo ni chafu maana vijana hawazisafishi na badala yake wanaendelea kuzichafua.
• Wapo vijana ni wavuta bangi na wapo makanisani na wazazi wao hawajui.
• Wapo vijana ni wanywaji wanakunywa pombe na wazazi wao hawana habari.
• Wapo vijana ni waasherati na wapo makanisani.
Vijana wanaotembea na wamama watu wazima.
Mabinti wanaotembea na wababa na wababu watu wazima.
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni