Mchungaji Kiongozi wa huduma ya Assaph Ministries International Rev Ben,
hivi karibuni alionyeshwa katika maono nchi ya Tanzania ikiwa katika
vita kubwa. Mtumishi amesema hii ni Mara ya tatu sasa anaonyeshwa na hii
imekuwa ni kubwa hata kumfanya baada ya kutoka kwenye maono hayo moyo
kumwenda mbio. Alieleza aliona jinsi watu watakavyopata shida katika
kukimbia hasa watoto akina mama na wazee.
Ikumbukwe miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mivutano mbali mbali ya
kisiasa na mihemuko ya wanajamii katika sehemu mbalimbali na kusababisha
hata baadhi ya watu kupoteza maisha bila hatia lakini pia kumeongezeka
maasi yanayotokana na kuporomoka kwa maadili na mabaliko ya kijamii
yatokanayo na utandawazi.
Lakini kumekuwa na mihemuko ya kidini sehemu ambayo imesababisha vurugu
za hapa na pale na hata watu kumwagiwa tindi Kali na utumiwaji wa siraha
za moto kama risasi na mabomu. Katika maelezo Yake amesema kuna msukumo
wa chini kwa chini kutoka nchi nyingine kwa kutaka kuharibu tu amani
iliyopo Tanzania. Wanajiuliza kwanini Tanzania iwe na amani tuuu
wanaweza hata kutumia pesa kuwatumia baadhi ya watanzania kutuvuruga,
aliuliza kama Tanzania kutatokea vita tutakimbilia wapi? Maana majirani
wote wanaotuzunguka si swali. Alimaliza kwa kusema anatamani watanzania
wapate ujumbe huu ili kwa pamoja tuungane kuombea amani nchi yetu ya
Tanzania.
Mungu anasema katika kitabu cha 2nyakati 7:14 Ikiwa watu wangu,
walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta
uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na
kuiponya nchi yao. hivyo hata mtu mmoja akimaanisha basi Mungu yuko
kusikia na kughaili hivyo watanzania tunahamasisha kuiombea inchi Yetu
ili Mungu atunusuru na vita.
Ikumbukwe huko nyuma kulikuwa na huduma ya Tanzania itubu ambayo
ilihamasisha watanzania kutubu ili tusipatwe na majanga ni wakati wa
kumrudia Muumba wetu ili aiponye inchi yetu.
kwa hisani ya https://www.assaphministriesint.blogspot.com
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni