siku ya Jumapili katika Kanisa la Magomeni TAG katika kusheherekea miaka
75 ya Kuanzishwa kanisa la TAG hapa Tanzania, iliandaliwa ibada ya
Kihistoria kwa Mchungaji wa Kanisa hili Dastan Kanemba Kuandaa Ibada kwa
kualika washirika wa Magomeni waliowahi kusali mahali hapo na kuwa na
chakula cha pamoja.
Katika ibada hiyo ziliimbwa nyimbo za mwaka 47 wakati kanisa linaanza,
watoto wa Sunday School ambao kwa sasa ni watu wazima walikumbushia enzi
za utoto wao kisha aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa hilo ambaye ndiye
mwasisi Mchungaji Sasali alihubiri siku hiyo. Kisha chakula cha pamoja
kiliandaliwa.
Sehemu Ya Umati Wa Waumini Waliokuwepo Kwenye Ibada
Akihubiri katika Ibada hiyo Mchungaji Sasali alisema Kanisa la TAG
halitaweza kuvuna mavuno mengi iwapo kuna chuki kati ya mtu na mtu, kati
ya kanisa na Kanisa, Yesu alipokufa alifanya kazi ya kuvunja
"viambaza". Aliwataka washirika wa Kanisa hilo kuvunja viambaza vyote
ambavyo yamkini watu bado wanavyo mioyoni ili kuweza kupiga hatua.
Vilevile katika ibada hiyo ambayo ilikuwa na watu wengi mpaka wengine kukaa nje kulikuwa na waimbaji mbalimbali wa hapa kanisani, kwaya zote bendi kongwe ya christ Boys, Anoiting soldier, Amosi, John Shabani na wengine wengi ambao waliwahi kusali katika kanisa la Magomeni.
vile vile kanisa lilitoa zawadi mbalimbali ikiwapo kanisa la Mivumoni, na kituo cha watoto cha Upendo. jambo lingine ambalo lililozungumzwa ni kumnunulia gari Mch sasali kwa kutambua kazi kubwa aliyoifanya kuanzisha kanisa hilo la magomeni, akizungumza katika ibada hiyo Mch Kanemba alisema kuwa wanatambua ugumu wa kuanzisha kanisa kuna magumu mengi ila kwa sasa kanisa ni kubwa na linaendelea kukua.
Ma Mc wa Event Ze Blogger Kushoto na Joseph Mwakibuti
Aliyekuwa Mchungaji Kiongozi wa Magomeni TAG pamoja na Mke wake Pastor Sasali akienda sawa katika Ibada hiyo
Pastor Matthew Sasali ambaye ni Mtoto wa Pili wa Mchungaji Sasali akifatilia Ibada kwa Umakini Mkubwa
Hapa Sijui Ilikuwa nini?
Mchungaji Kiongozi Wa Magomeni TAG Dastan Kanemba akitoa maelekezo Muhimu wakati wa Ibada
Ze Blogger akimpa Kisa Cha Zamani Sana Wakati Wa Kanisa hilo linaanza
Watu hawana Mbavu Ma-Mc wakiwa Kazini
Pastor Matthew Sasali akikumbushia Kinanda Enzi za Magomeni
Joel Sasali Uche wa Bongo akikamua Worship Siku ya Jumapili
Kitu Cha Cord...na Pastor Mathew Sasali
In His Presence
Ze Blogger akituma Vocal Wimbo wa Kuabudu
In His Presence...There is the Fullness Of Joy
Kitu Cha Sebene
Mtakatifu Mtakatifu Twakuita Mtakatifu Eeenh Yesu Wewe Mtakatifuuuu
Mchungaji Kiongozi wa Magomeni TAG Mch. Kanemba na Mke wake.
Mchungaji Sasali aliposimama kwenye madhabahu alipanda mama mmoja kupangusa kwa kitambaa chake miguu ya Mtumishi huyo
Mchungaji Sasa alikuwa na Mke wake Madhabahuni
Watoto wa Mchungaji Sasali
Mzee
Mzima Pastor Sasali akihudumu siku ya Jumapili kwenye Ibada ya
maadhimisho ya Miaka 75 ya TAG ngazi ya Kanisa la Mahali Pamoja
Pastor Sasali na Mama Sasali Wakiwaombe Watumishi Mch. Kanemba na Mke wake
Pastor Sasali na Pastor Kanemba wakifanya maombezi ya Washirika
Kwaya ya Mwaka 47 akiimba Katika Ibada, Hawa ndio waliokuwa Washirika Wa Mwanzoni Mwanzoni wakati Kanisa Linaanza
Vijana Waliofungishwa ndoa na Mchungaji Sasali wakitoa Sadaka Ya Shukrani
BAADHI YA BARAZA LA WAZEE WA KANISA |
KIPINDI CHA SEBENE |
WATU WALIKUWA WENGI MPAKA WENGINE WALIKAA NJE |
MCH KANEMBA NA MAMA MCHUNGAJI |
MCH KANEMBA AKIFANYIWA MAOMBI NA WATUMISHI |
BAADHI YA WASHIRIKA WA KANISA MIVUMONI KWA MCH N. SASALI |
ILIKUWA NI WAKATI WA FURAHA |
KWAYA ZILIJUMUIKA NA KUIMBA KWA PAMOJA |
WATU WAKIFUATILIA UIMBAJI |
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 84477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni