Utangulizi
Mathayo alikuwa mtoza ushuru ambaye
Bwana Yesu alimwita awe mwanafunzi wake mwanzoni kabisa wa huduma yake ya
hadharani. Kwa hiyomambo mengi anayoyaelezea
aliyashuhudia kwa macho yake mwenyewe.
Anaanza kwa kueleza kwa kirefu
kuhusu kuzaliwa kwa Yesu
na Bikira Maria, kubatizwa kwake na
kujaribiwa kwake nyikani. Yesu alikuja akihubiri juu ya Ufalme wa Mungu ambao
ni wa kila mtu anayetaka kupata uzima wa milele. Mtu anaingia katika Ufalme huu
kwa kutubu dhambi na kumwamini Yesu. Mathayo ameyagawa mafundisho ya Yesu
katika sehemu kubwa tano: Maadili, Kueneza Habari Njema, Mifano, Ushirika na
kuja kwa Ufalme wa Mungu. Sehemu ya Mwisho ya Injili ya Mathayo inaeleza juu ya
kufa na kufufuka kwa Yesu, na agizo alilotoa kwa wote wanaomwamini kueneza
Habari Njema ulimwenguni kote. Wazo Kuu Shabaha kuu ya Mathayo katika kuandika
Injili hii, ilikuwa ni kuonyesha kwamba Bwana Yesu anakamilisha
ahadi aliyoitoa Mungu katika Agano
la Kale. Kwa sababu hii, Bwana Yesu anatambulishwa kuwa ni mwana wa Mfalme
Daudi na pia mzao wa Abrahamu
(1:1). Kadhalika Mathayo anatumia
mifano mingi kutoka katika unabii
uliotolewa na manabii wa Agano la
Kale, kueleza maisha ya Bwana Yesu ambaye alikuja kuwa Mwokozi wa Wayahudi
(1:21),wa watu Mataifa mengine
(4:13-16)na hatimaye Mwokozi wa
ulimwengu wote
(28:19).Maadili yawapasayo watu
wanaoingia katika Ufalme wa Mungu yanaelezwa katika Mahubiri ya Mlimani
(Sura 5-7),ambapo wana wa Mungu
wanaagizwa kukataa kufuata maad
ili ya dunia hii na kutafuta kwanza
Ufalme wa Mungu na haki yake, ndipo hayo mengineyo watakapozidishiwa
. (6:33). Mgawanyo
1 Maisha na huduma ya Bwana Yesu
(1:1-4:25)
2 Mahubiri ya Mlimani (5:1-7:29)
3 Mafundisho, Mifano na Mazungumzo
(8:1-18:35)
4 Safari ya kwenda Yerusalemu na
maonyo ya mwisho (19:1-23:39)
5 Unabii kuhusu mambo yajayo
(24:1-25:46)
6 Kufa na kufufuka kwa Bwana Yesu
(26:1-28:20)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni