BARAZA
la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema wiki iliyopita lilikabidhi kibali
kwa ajili ya uendeshaji wa Tamasha la Krismasi litakaloendeshwa na
kampuni ya Msama Promotions. Tamasha hilo ni muendelezo wa tamasha la
Pasaka lililoasisiwa tangu mwaka 2000 likiwa na lengo la kumtukuza na
kumtumikia Mungu kupitia nyimbo mbalimbali za waimbaji wa ndani na nje
ya nchi.
Kabla ya tamasha la Krisimass, Msama alipewa mawazo mengi kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari wa kutoka vyombo mbalimbali vya habari. Sababu za kumtaka Msama kuandaa Tamasha la Krisimass ni kupanua wigo wa kuhubiri Neno la Mungu na kuwapa waamini na wadau wa muziki wa Injili fursa ya kupata burudani kupitia nyimbo za watumishi mbalimbali.
Kampuni ya Msama inayoandaa matamasha hayo mawili yenye mlengo unaofanana, imedhamiria kuandaa matamasha hayo mawili ni kufikisha neno la mungu kupitia nyimbo sambamba na mapato yatakayopatikana yatasaidia yatima, walemavu, wajane, waathirika wa Ukimwi na wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kampuni hizo, Alex Msama tamasha la Krisimas litafanyika mikoa mbalimbali ili kuwafikia waumini wengi zaidi lengo likiwa ni kumtukuza na kumuabudu mungu. “Waumini baada ya kuguswa na neno la mungu katika tamasha la Pasaka, wamenishauri niandae tamasha la Krismass lengo likiwa ni ibada,” alisema Msama.
Ili kunogesha tamasha hilo lenye hadhi ya kimataifa,kupitia waimbaji wa Tanzania pia litashirikisha waimbaji kutoka nchi mbalimbali za Afrika kama ilivyo kwenye tamasha la Pasaka siku hiyo waimbaji wote wataimba ‘live’ na hakutakuwa na matumizi ya Play back CD ama mshindo nyuma. Lengo la Tamasha la Krismasi kumuabudu Mungu kwa njia ya sifa lakini pia mapato yatakayopatikana yatasaidia wenye uhitaji maalum kama wajane,walemavu, yatima, waathirika wa Ukimwi na wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Anasema lengo lingine ni kusherehekea sikukuu ya Krismass na mashabiki na wadau wa muziki wa injili hapa nchini na kufikisha ujumbe wa neno la mungu wenye lengo la kudumisha amani na utulivu nchini.
Anasema pia tamasha hili litashirikisha watumishi wa Mungu kutoka huduma na makanisa mbalimbali kwa ajili ya kuiombea Baraka na amani Taifa laTanzania pamoja na viongozi wao. Aidha Msama alitumia fursa hiyo kuwataka mashibiki na wadau wa muziki wa injil waendelee kufuatilia ratiba kamili ya tamasha hilo kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
Aidha Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa wa Basata, Nsao Shalua anashauri, tamasha la krismass mwaka 2013,lianzie mikoani na siku ya kilele ambayo ndio sikukuu yenyewe tukio lifanyike Dar es Salaam.
Anasema kuwe na vitu vya ziada kama akina mama wajasiriamali kutoka makanisani na vikundi vingine vitumie fursa hiyo ili kuleta hamasa ya tamasha husika. Mkuu wa Matukio wa Basata, Kurwijira Maregesi alisema waimbaji watakaopanda jukwaani mbali ya kuimba nyimbo zilizozoeleka waimbe pia tungo zenye ujumbe wa Krisimass ili kudhihirisha uhalisia wa siku yenyewe.
Pia amesema kabla ya tamasha hilo, Basata itatoa semina kwa waimbaji ili kuwaweka sawa kabla ya matamasha hayo kuanza.
Maregesi alitumia fursa hiyo kuwaasa waandaaji wa tamasha hilo kulitumia tamasha hilo kama sehemu ya kuwaasa vijana kuachana na mavazi yasiyo ya heshima na matendo mengine yanayomchukiza mungu na kudumisha maadili ya muziki wa injili. “Ifike mahali Tamasha kama la Krismass kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu mienendo mibovu kama mavazi na mengineyo yanayomchukiza mungu".
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni