Jumatatu, 21 Oktoba 2013

MCHUNGAJI AUWAWA KWA RISASI MOMBASA KENYA


Mchungaji Charles Mathole enzi za uhai wake. Picha kwahisani ya mwinjilisti Munishi.
Mchungaji Charles Mathole ameuawa kwa kupigwa Risasi na watu wasiojulikana katika kanisa analoliongoza la Redeemed Gospel Church lililoko Vikwatani Mtopanga Mombasa majuma mawili baada ya Shekhe wa dini ya Kiislamu kwa jina la Rogo kuuawa katika mazingara ya kutatanisha ikapelekea maandamano ya Waislamu Mombasa na Kanisa likateketezwa moto.

Pastor Charles Mathole wa Redeemed Gospel Church Mtopanga Mombasa alipigwa risasi ya kichwa Ndani ya Kanisa USIKU wa kuamkia Leo Jumapili ambako anadaiwa alikuwa ameenda kumuombea mama aliyekuwa namatatizo ya ndoa na Mume wake na haijulikani nini kilifuata baada ya hayo.

Polisi wameanza uchunguzi na japo waumini waliokuja kuabudu waligeuka waombolezaji na kufanya maombi kanisani hapo kwa kuvunja nguza za shetani zinazojiinua kanisani hapo. Morris Ali ambaye ni mmoja wa wanakwaya kanisani hapo ambaye aliitwa kujionea tukio hilo, alisikitika kwa jinsi alivyouona mwili wa mchungaji huyo ukiwa upo kwenye kiti sehemu ya kinanda huku Biblia ikiwa mikononi, kichwa chake kikiwa kimelala kwenye kona ya kiti cha plastiki, ambapo mwimbaji huyo amesema waliposogea karibu ndipo walipoona damu zikitoka kichwani mwa mwili huo.
Kanisa la Vikwatani Redeemed Gospel alipouwawa mchungaji huyo. Picha kwahisani ya Labban Waloga Daily Nation.
Ambapo kwa mujibu wa Katibu wa makanisa Mombasa bwana Stanley Prince Nyachae amesema hakuna mali iliyoibwa kanisani hapo na kutaka mamlaka husika kufanya uchunguzi wa haraka ili kubaini waliofanya tukio hilo.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Hakuna maoni: