AFLEWO ni
nini?
·
AFLEWO ni kifupi
cha “Africa Let’s Worship” ambayo maana yake ni Afrika Njoo Tuabudu
·
AFLEWO ni mradi wa
uimbaji katika Afrika ambao ulianza mwaka 2004 nchini Kenya na baadae kuenea
katika nchi ya Tanzania na Rwanda.
·
Tanzania huduma ya
AFLEWO ilianza 2011 na mwaka huu 2013 ni Aflewo ya Tatu Kufanyika.
Nini maana ya
maono ya AFLEWO?
KUTIA TUMAINI KATIKA YESU KUPITIA MATUKIO YA
KUABUDU MARA MOJA KWA MWAKA KATIKA MUZIKI NA MAOMBI IFIKAPO MWAKA 2017.
Hapa Tanzania AFLEWO ilianza mwaka 2011 na mkesha
wa kwanza ulifanyika ukumbi wa Diamond Jubilee tarehe 20/4/2011 na kuhudhuria
na watu karibu ya 5000.
Mwaka 2012 tukio la AFLEWO lilifanyika kanisa la
CCC, Upanga na kuhudhuriwa na watu karibu ya 5000.
Mwaka huu Mkesha Wa Aflewo Unafanyika Katika Ukumbi
wa Kanisa la BCIC Mbezi, kuanzia saa 3:00 Usiku Mpaka saa 12 Alfajiri.
Aflewo Mwaka 2013 Imeboreka zaidi baada ya kuongeza
miundombinu ya utendaji kazi kwa kutanua Uwigo wa Ushirikishwaji wa Makanisa
Katika Kufikia Kilele Cha Aflewo Mwaka 2013.
Mikesha yote ya Aflewo inakuwa haina kiiingilio ni
event ya bure kwa ajili ya Kila Mmoja.[1]
Nini Kusudi
Kuu la Mipango Ya AFLEWO?
1. Kuleta uzoefu wa kua “Mwili Mmoja”...ndio maana
Aflewo si Mkesha wa Kanisa Moja.
2. Kuombea Taifa La Tanzania hususani katika Amani,
Uchumi, Upendo etc.
Kuombea Kanisa la Tanzania Kwa Ujumla
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni