Kadinali Pengo alisema amepata taarifa kutoka kwa watu ambao hana na shaka nao.
“Jana (juzi), niliongelea kwamba suala zima la tukio la Arusha
halihusiani na imani yoyote ya kidini. Tamko hilo nilitamka kutokana na
taarifa nilizofikishiwa na watu ambao sikuweza kuwa na shaka kwamba
wanaoniambia ni kweli na sidhani kama ningekuwa na sababu ya kusema
wamefika kwa kunidanganya kwa hiyo tamko litakuwa limesimama juu ya
msimamo huo,” alisema Kadinali Pengo na kuongeza:
“Lengo la msingi kabisa, langu na la kanisa ni kwamba tukio lolote
lile liwe kwa nia mbaya au nzuri kwa upande wetu isiwe ni sababu ya
kuanza mapambano na kuwa chimbuko la ukosefu wa amani katika nchi yetu,”
alisema Pengo.
Alisema kuwa kila anayehusika ajue amani ya kweli ya taifa lolote
haiwezi ikapatikana isipokuwa ikijengwa juu ya ukweli na ukweli kabisa
bila kufuta au kujaribu kupotosha ukweli kwa namna yoyote ile.
“Tusipojua kusema ukweli ulivyo hatuwezi kufaulu kuleta amani katika
taifa letu. Kwa hiyo pamoja na kuendelea kuwaomba waumini wa Katoliki
pamoja na watu wenye mapenzi mema kuendelea kumwomba Mwenyezi Mungu
arehemu taifa letu na mapambano ya aina yoyote ile. Tuendeleze nia yetu
njema ya kusema ukweli, haidhuru ukweli huu unamgusa nani,” alisema
Pengo.
Alisema kujaribu kuficha ukweli na kupotosha ni njia sahihi kwa ibilisi kuleta vurugu katika jumuiya ya watu na ieleweke hivyo.
“Naomba kila mtu akubaliane na tamko langu haidhuru pana kosa, amani
ya taifa letu ni jambo la msingi na amani itajengwa tu iwapo kila mtu
anayehusika atakuwa tayari kusema ukweli kama ulivyo,” alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni