Pasaka ni
sikuku iliyoamriwa na Mungu tangu siku za kale
kwa wayahudi
kuifanya katika mwezi wa Abibu au Nisani
katika
“kalenda ya kiebrania” yaani mwezi wa 3 au 4 katika
kalenda ya
kirumi, kwa lengo la kumbuka njisi Mungu
alivyowakomboa
kutoka utumwani Misri; Twasoma:
“Utunze
mwezi wa Abibu, ukamfanyie pasaka BWANA,
Mungu wako,
kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku BWANA; Mungu wako.
Nawe umchinjie pasaka
BWANA, Mungu wako katika kundi la kondoo na la ng’ombe,
mahali atakapochagua BWANA apakalishe jina
lake.”
(Kumbukumbu 16:1-2) Soma pia: (Kutoka 12:14)
Kama
tulivyoona katika pasaka wayahudi waliamriwa
kuchinja
mnyama mmoja katika kundi, lakini
tunapoendela
kusoma tunaona jinsia Mungu alivyoamuru
mnyama huyo
aokwe na kuliwa; Twasoma:
“Usimle pamoja na mikate iliyotiwa chachu;
siku saba
utakula naye
mikate isiyotiwa chachu, nayo ni mikate ya
mateso; kwa
maana ulitoka nchi ya Misri kwa haraka; ili
upate
kukumbuka siku uliyotoa nchi ya Misri, siku zote za
maisha yako.
Wala isionekane kwako chachu muda wa
siku saba
katika mipaka yako yote; wala katika hiyo
nyama
uchinjayo siku ya kwanza jioni, kisilale cho chote
usiku kucha
hata asubuhi. Usimchinje pasaka ndani ya
malango yako
yote akupayo BWANA, Mungu wako; ila
mahali
atakapochagua BWANA, Mungu wako apakalishe
jina lake,
ndipo mtakapomchinjia pasaka jioni, katika
machweo ya
jua, kwa wakati kama uliotoka
Misri.”
(Kumbukumbu 16:3-6); Soma pia: (Kut 12:3-13)
Katika mwezi
huo wa abibu ambao Mungu aliufanya kuwa
mwezi wa
kwanza kwako, Wayahudi walifanya karamu ya
Pasaka kuwa
kumbukumbu la jinsi Mungu alivyowaokoa
kutoka Misri
(Kutoka 12:1-51; Walawi. 23:5).
Pasaka maana
yake ni "kupita Juu", maana Mungu alipita
juu ya
nyumba zao asiwaangamize wazaliwa wao wa
kwanza;
Twasoma:
“Na ile damu
itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba
mtakazo
kuwapo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita
juu yenu,
lisiwapate pigo lo lote likawaharibu nitakapoipiga nchi ya Misri.” (Kutoka
12:13); Soma pia:(Kutoka
12:27)
JE? WAISRAELI
WALIKUWA NA SIKUKUU ZINGINE
ZAIDI YA PASAKA.
Biblia
inaeleza wazi ya kuwa wayahudi walikuwa na sikukuu zingine ambazo Mungu
aliwaagiza mbali pasaka;
basi hebu
tuzione sikukuu hizo;
PENTEKOSTE -
Pentekoste maana yake ni 50, Sikukuu hii
ilikuja siku
ya 50 baada ya Pasaka. Pentekoste iliitwa pia
Karamu ya
Juma, maana Mungu aliwaamuru wajihesabu
juma saba
kuanza baada ya Pasaka. Hivyo, karamu hiyo ilitokea mwezi wa 6. Siku ya
Pentekoste Wayahudi walimtolea Mungu mikate
ya ngano miwili iliyopikwa kutokana na mazao yao ya
kwanza. (Walawi 23:15-22)
KARAMU YA
VIBANDA - Sikukuu hii ilitokea mwezi wa 10.
Kwa muda wa
siku saba walikaa katika vibanda wakikumbuka jinsi Mungu
alivyowalisha na kuwatunza jangwani walipotoka Misri. Nao
wakamtolea Mungu shukrani kwa mavuno yao(Walawi
23:39-43).
SIKU YA
UPATANISHO. Mara moja kila mwaka (terehe 10
mwezi wa 10)
kuhani mkuu aliingia Patakatifu pa Patakatifu.
Humo aliweka
damu juu ya Kiti cha Rehema (funiko la Sanduku la Agano) kusudi dhambi za
Wayahudi zisahauliwe na Mungu kwa muda wa mwaka mmoja (Walawi 16:1-
34;
23:27-32), Wayahudi walijinyima chakula kuonyesha huzuni kwa dhambi zao na
kujinyenyekea kwa Mungu.
JE SIKUKUU
HIZI ZA WAISRAELI IKIWEMO PASAKA
ZINAENEDELEA?
Neno la
Mungu linaeleza wazi ya kuwa sikukuu hizi za kale
zilikomeshwa
na Mungu alitupa utaratibu mwingine wa jinsi
alivyotaka
tuenende; Twasoma:
“Tena
nitakomesha furaha yake yote, na sikukuu zake, na
siku zake za
mwandamo wa mwezi, na sabato zake, na
makusanyiko
yake yote yaliyoamriwa.” (Hosea 2:11)
“Angalia,
siku zinakuja, asema BWANA, nitakapofanya
agano jipya
na nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda. Si
kwa mfano wa
agano lile nililofanya na baba zao, katika
siku ile
nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano
langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa
mume kwao,
asema BWANA.”(Yeremia 31:31-32)
JE WAKRISTO
TUNA PASAKA LEO?
Ni kweli
wakristo tuna pasaka leo, walakini si katika utaratibu ule uliotumika katika
siku za waisraeli, kama tulivyoshuudia maandiko yaneleza wazi ya kuwa sikukuu hizo zilikomeshwa;
Basi hebu tuone utaratibu wa Pasaka ya
wakristo leo
ni upi;
Zingatia:
Kama tulivyoona hapo juu, waisraeli waliokolewa na damu ya
mnyama walio ipaka katika miimo na miisho ya milango yao na ndipo malaika wa
Bwana alipotambua na kupita juu; Soma
tena: (Kutoka 12:13, 27); lakini wakristo tunaambiwa pasaka wetu ni Yesu
mwenyewe aliyetuokoa kwa damu yake;
Twasoma:
“Siku ya
pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema,
Tazama,
Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhamb
ya
ulimwengu!” (Yohana 1:29); Soma pia: (Yohana 1:36)
“Nanyi
mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu;
mpate kutoka katika
mwenendo
wenu usiofaa milioupokea kwa baba zenu;
bali kwa
damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo
asiye na
ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.” (1 Petro 1-18-19)
“Basi
jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mapate kuwa
donge jipya,
kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa
maana Pasaka
wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka,
yaani,
Kristo;” (1 Wakoritho 5:7)
Basi kama
tulivyoona Neno la Mungu linatuthibitishia ya
kuwa kwa
sasa wakristo tunaokolewa na damu ya Yesu
ambaye ndiye
Pasaka wetu na si kwa damu ya mnyama
aliyekuwa
Pasaka wa kale. Basi kiwa
hivyo ndivyo, ni dhahiri hata utratibu wa kusherehekea
pasaka kwa wakristo ni tofauti, Basi hebu tuone
wakristo tunasherehekeaje pasaka yetu leo.
Yesu
alipokuwa akila Pasaka ya mwisho pamoja na wanafunzi wake, aligeuza Pasaka.
Aliwaambia kwamba, kuanza siku ile,
watakapokula mikate wangekumbuka mwili wake uliotolewa
kwa ajili yao badala ya kukumbuka kuokolewa kutoka
utumwani nchini Misri; Twasoma:
“Nao
walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki,
akaumega
akawapa wanafunzi wake, akisema, Twaeni mle;
huu ndio
mwili wangu
Akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa,
akisema, Nyweni nyote katika hiki; kwa maana hii ndiyo damu
yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa
ondoleo la dhambi.” (Mathayo 26:26-28)
“Kwa maana
mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa ninyi,
ya kuwa
usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, na ye akiisha
kushukuru
akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio
kwa ajili
yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Na vivi
hivi baada
ya kula akakitwaa kikombe, akisema, kikombe
hiki ni
agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kwa kila
mywapo, kwa
ukumbusho wangu. Maana kila mwulapo
mkate huu na
kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti
ya Bwana
hata ajapo.” (1 Wakorintho 11:23-26).
JE
WANAOSHEREHEKEA PASAKA YA KALE WAMEPOTEA?
Ni kweli
karibu ulimwengu mzima unasherehekea pasaka
kama
walivyokuwa wakisherehekea wayahidi nyakati zile,
wakidhani
ndivyo ilivyo agizwa, basi na tuzingatie maneno
yafuatayo;
Twasoma:
“Iko njia
ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini
mwisho wake
ni njia za mauti” (Mithali 14:12)
“Akajibu,
akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu
wa mbinguni
litang’olewa. Waacheni hao ni viongozi vipofu
wa vipofu.
Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.”
(Mathayo 15:13-14)
“Si kila aniambiaye, Bwana, Bwana,
atakayeingia katika
ufalme wa
mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya
Baba yangu
aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile,
Bwana, Bwana
hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa
jina lako
kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza
mingi? Ndipo
nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi
kamwe;
ondokeni kwangu, ninyi mtendao
maovu.”
(Mathayo 7:21-23)
“Basi ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano
wa
mimi na
Apolo kwa ajili yenu ili kwamba kwa mfano wetu
mpate
kujifunza kutokupita yale yaliyoandikwa; ili
mmoja wenu
asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha
mwenziwe.”
(1 Wakorintho 4:6)
Basi kama
tulivyoona, upotofu uliopo katika sikukuu hii ya
pasaka na
jinsi Mungu anavyo tuonya kuwa makini na
mafundisho
ya uongo, ni dhahiri tunawajibu wa kujifunza
neno la
Mungu kwa bidii ili tupate kujua yaliyo mapenzi
yake
tukayafanye; Soma: (Yakobo 1:22-25)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni