Katika waimbaji wa nyimbo za injili ambao ni mihimili ya waimbaji wa nyimbo za injili huwezi ukaacha kumtaja bahati Bukuku ambaye ametoa matoleo mengi ya albam, na ni kati ya waimbaji ambao wamefanikiwa kimaisha kupitia uimbaji. waimbaji wa nyimbo hizi za injili wamekuwa na uhuru wa kuimba aina yeyote ya mziki wanaotaka kama regger, zouk, sebene, segele, south, jazz, blues.mduara nk. leo namuangazia Bahati ambaye baada ya kufuatilia nyimbo zake nyingi nimegundua kuwa anapenda sana nyimbo za regger na hakuna hata albamu hata moja aliyotoa bila kuweka nyimbo za regger na kiukweli anazitendea haki.
Upo wimbo mwingine pia ambao ni maarufu sana na unakubalika sana na watu wengi nao ni mahadhi ya regger huu unaitwa waraka Naamani, huu wimbo ulipoingia ulikuwa unapigwa kila mahali na kweli bahati aliutendea haki
huu nao ni wimbo wa regger ambayo nao umekaa vizuri sana unaitwa lazima usamehe kwa mtu yeyote anayependa miziki ya regger atakubaliana na mimi kuwa miziki hii iko vizuri sana na zimetendewa haki.
Lakini si hivyo tu katika albamu mpya aliyotoa ya dunia haina huruma, kuna nyimbo mbili za Abinel na Ahabu ambazo nazo ukizisikiliza kwa kweli zipo katika kiwango cha kimataifa tafadhali tafuta uzisikilize
Maoni 1 :
Nyimbo ya mduara naitafuta sana, Ile "wanaimba wanaruka wako ndani ya Yesu" inaitwaje?
Chapisha Maoni