LEO asubuhi vyombo vingi vya habari vimeripoti Juu ya Uchomwaji wa Kanisa la The Pool of Siloam la huko Zanzibar kwa kutupiwa vitu vilivyosababisha moto huo.
Jioni hii tumezungumza na Mchungaji wa Kanisa wa Kanisa hilo ambaye amethibitisha kuwa vitu vyenye Thamani ya Shilingi Milioni 3 na nusu vimeharibika vibaya na vyote vilikuwa upande wa Madhabahuni.
Aidha Mlinzi wa Kanisa hilo amesema kuwa, mida ya Saa 9 usiku aliona watu watatu wakipita karibu na Kanisa hilo na kutupia vitu viwili ndani ya Kanisa hilo upande wa madhabahuni na baada ya yeye kuona hivyo alikimbilia Upande wa pili na muda mfupi baadaye aliona moto ukianza kuwaka upande wa madhabahuni hivyo kuamua kumpigia Simu Mchungaji wa kanisa hilo.
Kwa Mujibu wa Maelezo ya Mchungaji huyo, tukio hili ni la pili kulikumba Kanisa hilo kwani lilishawahi kukumbwa na tukio lingine kama hilo.
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni