|
Mwal Mwakasege |
Salamu zetu za mwaka mpya wa 2013 zinatoka katika 1mambo ya Nyakati 12:32 unaosema:
Na wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua
yawapasayo Israeli wayatende....walikuwa watu mia mbili na ndugu zao
wote walikuwa chini ya amri yao"
Ni Maombi yetu kwa Mungu ya kuwa
atakupa 'akili' za kujua mwaka huu wa 2013 unao au umemeba nyakati zipi.
Hii itakusaidia uweze kuzitambua na kuzitambua fursa zilizomo ndani
yake - ili ujue cha kufanya sawasawa na Yeremia 29:11.
Kwa
mfano,ikiwa utaweza kuona fursa moja kwa siku, ina maana utakuwa na
fursa 365 kwa mwaka 2013 za kutumia!Na ikiwa utaweza kuona fursa moja tu
kwa wiki,ina maana utakuwa na fursa 52 kwa mwaka 2013 za kutumia.
Kumbuka kuna watu wanaanza mwaka na wanaumaliza mwaka huo, bila ya kuona
fursa hata moja ya kuwasaidia watoke katika ngazi ya kimaisha
waliyokuwa nayo, wakati wanauanza mwaka. Utawatambua kwa kuona maisha
yao ya mwanzo wa mwaka hayana tofauti na maisha waliyonayo wanapoumaliza
mwaka!
Ndio maana salamu zetu kwako za mwaka mpya - ni maombi kwa
ajili yako ili Mungu akupe akilii za kujua mwaka 2013 umebeba nyakati
zipi ili uweze kuona fursa zilizopo na uzitumie ipasavyo sawa na Yeremia
29:11
Heri ya Mwaka Mpya!!
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671
AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni