Katika miaka ya hivi karibuni mziki ya injili umekuwa ukipiga hatua kubwa kwenda kimataifa baada ya waimbaji wengi wa mziki huo kupata mialiko kwenye nchi mbalimbali Duniani. hii inaonyesha kuwa mziki huo unakubalika sana na kupendwa na watu wengi na kingine kuwa na upako kutokana na anayeimbiwa katika nyimbo hizo ni Mungu mwenyewe.
|
Mbasha Akiwa na Salim Kikeke nyuma ni Charles Hilary |
mwaka jana tumeona waimbaji mbalimbali kama Upendo Nkone,
Upendo Kilahilo, Christina Shusho, Rose Mhando na Flora Mbasha wakiwea
pipa na kwenda nje ya bara la Afrika kufanya huduma ya uimbaji na ambayo
imekuwa na manufaa makubwa sana kwa waimbaji wenyewe lakini hata kwa
mziki wa injili nchini.
|
Mbasha akihojiwa Radioni na John Solombi |
leo nataka nimuongelee Flora Mbasha ambaye yuko katika ziara yake UK
na baadae ataenda Australia. katika ziara yake ametembelea BBC ambalo ni
shirika kubwa la habari duniani ambalo habari zake zinasambazwa duniami
kote. kufanyika kwa mahojiano hayo yanaendelea kufungua ukrasa mpya
katika tasnia ya nyimbo za injili. hii ni mara ya pili kwa flora
kuhojiwa na kituo kikubwa cha habari baada ya mwaka jana kuhojiwa na VOA
(Voice of America) alipotembelea huko. kwasasa ninaweza kusema kuwa
amebakisha kituo kimoja ambacho nacho ni kikubwa duniani yaani DW sauti
ya Ujerumani na namwombea siku ifike nako afike kama imewezekana VOA na
BBC hata DW inawezekana.
|
Mbasha akihojiwa kwenye TV na Salim Kikeke |
katika mahojiano mafupi sana niliyofanya nae amehojiwa na
radio pamoja na TV ambavyo kuna uwezekano vipindi hivyo vya mahojiano
kuonyeshwa na kusikika wiki hihi. amesema baada ya kumaliza ziara yake
UK wataelekea Australia ambako huko nako watafanya huduma huko.
|
Mbasha akiwa na watangazaji wa BBC swahili Salimu Kikeke na John Solombi |
|
Mbasha na John solombi |
|
Baada ya kukausha koo kwa mahojiano hapa anaburudisha koo kwa vitu laini |
|
Mbasha Akikata kiu |
|
Mbasha akiwa na Charles Hiraly |
|
Maandalizi ya Uso kabla ya mahojiano ya TV |
|
Hii picha alipotembelea Sauti ya America Mwaka jana |
blog hii inamwombea ahudumu salama huko aliko na jina la Bwana lijulikane duniani kote. Mungu ibariki Tanzania na bariki waimbaji woooote wa gospel
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671
AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Maoni 2 :
I аm not surе whеre уou are gеtting yоuг informatіon, but
gooԁ topic. I needs tο ѕρenԁ ѕome time learning more oг understanԁіng more.
Thanks for grеat infо I was loοκing foг thіs infоrmаtion fοr my mission.
My ωeb-site; buy more twitter followers
my page: how to market your business
Thanks you are welcome again
Chapisha Maoni