Vijana wengi wa mkoa wa Dar, Tanzania kote na Duniani. si wageni kusikia jina Samuel Sasali aka Papaa wa sebene, anamiliki blog ya kikristo yenye wasomaji wengi Duniani na wengine wamefuata nyayo zake kwa kuanzisha blog zao, ni kijana ambaye amekuwa akishiriki kwenye matamasha mengi makubwa, kama Afwelo, FOF, Cumpass night, amekuwa ni Mc katika sherehe mbalimbali hata mimi harusi yangu iliyofungwa miaka 6 iliyopita Mc alikuwa Samuel enzi hizo akiwa bado kijana mbichi kabisa. blog hii ilifanya mahojiano kuweza kujua mambo mbalimbali ikiwa lile la mpango wake wa kuwaleta baadhi ya wana Jouyer's celebration kutoka South Afrika fuatana nami katika mahojiano haya utajua nini amesema
|
Blogger Samuel |
Martin Malecela
Shalom mwanzoni mwa mwaka uliahidi kuwaleta baadhi ya wana Joyers imeishia wapi
Samuel Sasali
Tatizo kubwa ni Fedha na Makubaliano ya Msingi
na Nilikosa muda wa kutafuta wadhamini
-
Samuel Sasali
Yap sababu kuna isue kama tatu zikikaa sawa naachana na ajira ya kuajiriwa na bepari na mimi nakuwa bepari hapo ndipo nitaweza
Martin Malecela
ok
mwaka huu mmefanya matamasha mfurulizo katika mikoa mbali mbali
nafikiri itafuata Mbeya, Singida na sasa mtaenda Moro nk waratibu wakuu wa matamasha haya ni nani na
wadhani ni akina nani
Samuel Sasali
Wadhamini ni tofauti tofauti
Lakini
ni Kanisa VCCT na Makanisa wenyeji wa kule tunakokwenda mfano mbeya
walikuwa RICC na Singida kwa Pastor Mwakitalima na Morogoro. Ni
Mtokambali
Martin Malecela
ok naona speed mnayokwenda nayo ni kali je mna mpango wa kufuta nyayo za fiesta?
-
Martin Malecela
changamoto
gani ambazo mnakutana nazo mpaka sasa ambazo uafikiri labda wakitokea
watu kuwasaidia inaweza ikaongeza speed ya hiyo huduma
|
Moja ya kazi anazozifanya ni u mc kwenye shughuli mbalimbali |
Samuel Sasali
1.
Finances sababu inatugharimu kuwasafirisha wanafunzi
2. Fiances kwenye
Publicity
3. PA System sababu we need to have our own PA and stage
4.
Cooperation kutoka makanisa mengine maana wanachukulia hiki kitu cha
kanisa fulani
5. Transport most tunazunguka na mabasi au min bus za
kukodi...kwa Ujumla wake Fedha ni Jawabu la Mambo yote
Martin Malecela
kuna
makampuni yanayotoa udhamini katika mambo mengi kama makampuni ya simu
na makampuni ya vInywaji baridi je? mumewahi waza au kujaribu kuwaomba
ili kupata udhamini maana najua wanaweza kujitangaza kupitia huduma yenu.
Samuel Sasali
Makampuni mengi ya siku hayana interest na mambo ya kidini tumejaribu kwenda lakini response yao imekuwa ya kujivuta
Martin Malecela
kuna
FOF na
Campus Night ambavyo vyote mmekuwa mkivifanya kwanza mtu
ambaye hajui hivi vitu unaweza kueleza tofauti yake na makusudi ya hivyo
vitu viwili
|
Baadhi ya waandaaji wa FoF |
Samuel Sasali
FoF ni entertainment event and Networking Campus Night ni maalumu kwa ajili ya wanafunzi kwa ujumla
FoF ni Kila Mwezi Campus Night Mara moja kwa mwaka katika mkoa husika.
Martin Malecela
je
FOF ukiacha burudani kunakuwa na nini vitu vingine hasa ukiangalia
malika kuna watoto vijana na wazee je yapo mambo ya kuwalenga wote au
kuna watu maalumu ambao inawahusu
Samuel Sasali
Kuna
Business Presentations, Kuna dinner, Kuna, Uimbaji wa nyimbo za Injili,
Kuna games, Kuna comedy, kuna Life sharing experiance (shushuda) etc
Martin Malecela
sasa
hivi mko kwenye maandalizi ya FoF Extravaganza ninafikiri ndiyo
itakuwa FOF ya mwisho kwa mwaka huu 2012. kwa wale wanao hudhuria wategeme
nini na je? kwa wale ambao hawajawahi kufika kabisa kwenye FOF una lipi
la kuwaambia ili liwashawishi kufika.
Samuel Sasali
Kwanza
kwa Mara ya kwanza tumewaleta Glorious ambao kama Glorious hawajawahi
kuja so tumekuja new flevors za muziki, Flora Mbasha and Shusho, Pia
watarajie kitu cha tofauti Upande wa Burudani sababu tunafanya full
burudani, pia. Watarajie games mpya kabisa na Kitu cha Mwisho ni kwamba
FoF imeshusha bei ni sh 15,000 tu ila safari hii watu watajinunulia chakula
|
Tangazo la FoF ya mwisho kwa mwaka huu |
-
-
Huduma zote unazofanya FoF, cumpas Nights n.k
Samuel Sasali
Ndugu
mwandishi kwanza nikutofautishie jambo moja, Campus night Iko chini ya
VCCT, na FoF haiko chini ya Kanisani ni sehemu ya kazi za FoF Committee.
Kuhusu kujipanga Campus Night nisiwe msemaji wa VCCT sababu iko chini
ya Campus Ministry, kwenye FoF tumejipanga mpaka mwaka unaisha tuwe
kwenye mikoa 10 Tanzania bara na Event Moja Zanzibar sababu FoF. Ni Kila
mwezi
Martin Malecela
Asante kwa ushirikiano wako. swali la kizushi najua wengi wangependa kufahamu unaoa lini
Samuel Sasali
Ninaona Mwakani katikati ya mwezi wa 10-12.
Pamoja na hayo mengi umefahamu kuhusu Samuel pia ni mwalimu mzuri sana katika ufundishaji wa neno la Mungu ijapo yeye bado suala la kufuata nyayo za familia yao ya kichungaji hataki kulizungumzia kabisa.
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671
AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni