Jumanne, 25 Desemba 2012

KATIKA KUMALIZIA MWAKA BLOG HII IMEWEZA KUONGEA NA WADAU MBALIMBALI NA HIVI NDIVYO WALIVYOSEMA

 Blog hii ina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa mwaka mzima wa 2012. kiukweli tumeweza kufanya vizuri kwa sehemu na kuweza kuwafikia watu wengi Duniani nashukuru kwa wale waliotuletea habari, waliotushauri, nk pamoja na wasomaji wote wa Blog hii ambao kwa sehemu kubwa wamekuwa ndiyo ya sababu ya kuendelea kuwapa kile mnachokihitaji. tumeweza kushirikiana na watu wengi ambao siyo rahisi kuwataja mmoja mmoja ila Mungu akubariki kwa kuwa sehemu ya mafanikio yetu. tunakaza mwendo na kuangalia mbele ili kuhakikisha kuwa mwaka 2013 tunaendelea kuwapa habari kama kawaida yetu.

blog hii iliwasiliana na baadhi ya wadau na tulipata nafasi ya kufanya nao mahojiano na tulikuwa na maswali kama matatu hivi ambayo kila mtu aliyajibu fuatana na aliyoyafanya mwaka katika mwaka huu.

maswali ni yenyewe ni kama ifuatavyo.

1. Mwaka huu ndo unafikia mwisho una mambo gani katika huduma yako ambayo unaweza kumshukuru Mungu kwa kufanikiwa kuyafanya.
2. Mwaka ujao una mambo gani ambayo umepanga kuyafanya
3. Una nini la kuwaambia mashabiki wako.


Sarah Shilla  si mgeni katika tasnia ya nyimbo za injili alikuwa na haya ya kusema.
Yani namshukuru Mungu nimeweza kuzindua my first album. Ya let it rain in his presence ,na nimeweza kurecord album yangu, na pia huduma kama ya kuhubri na kuhudumia watu wa Mungu huku India Bwana ameikuza.

Mwakani nitakua na graduate mwanzoni mwa mwaka and nita anza tours baadhi ya mikoa ya Tanzania, ingawa pia nina mialiko katika inchi kama Zambia, Zimbabwe , South Africa, swaziland na inchi zetu jirani za Kenya na Uganda kwahiyo nimekua na mialiko kadhaa kwa muda kwenye hizi inchi kwahiyo naona mwakani itakua muda mzuri kutumika both nyumbani na nje ya nchi. kuhudumia wanafuzi pia ni jambo lipo sana kwa moyo wangu.

Wazidi kuniombea wazidi kua supportive wavumilivu sometimes wanatamani kupata alot but ninakua na delay kwasababu ya fedha wawe wavumilivu ila wategeme that popote nitakapo simama kuhudumu lazima watakutana na Mungu aliye juu saana kwa moyo wangu, na zaidi nawapenda.



Evangelist Sarah Mvungi
Ni mwimbaji wa nyimbo za injili na muigizazi mkongwe
Asante sana 1:Namshukuru Mungu sana nimemaliza albamu yangu ya pili katika mfumo wa audio na video na pia nimezindua tarehe 11/11/2012, na pia kuwa mzima mimi na watoto wangu hakika namshukuru sana Mungu

Nategemea kuanza kurekodi albam nyingine naamini nitafanya na Mungu atanisaidia,na pia nategemea kurudi katika sanaa ya maigizo lakini sitaacha kumwimbia Mungu nitaimba mpaka mwisho  na malengo yangu pia ni kutoka kuimba zaidi kimataifa.  peke yangu siwezi lakini MUNGU WANGU JEHOVA ATANISAIDIA AMEN

Matthew Sasali       
 ni meneja wa kituo cha radio ya TAG kilichopo mbeya vile vile ni mchungaji
Ok
1.Mara zote kuisha kwa mwaka kwa watu wenye malengo makubwa ni huzuni...maana tunatamani mwaka   ungekuwa na siku angalau 500 ili itupe nafasi ya kumaliza kila ulilopanga lakini haiwezekani tena.
Kwa kweli kipindi hiki ndio cha kufanya tathimini ya nini umefanikiwa nini umekwama...Kwa upande wangu namshukuru Mungu sana,mwaka huu umekuwa wa-mafanikio makubwa sana,Malengo mengi katika huduma yangu ya Media Pastor imekuwa ya mafanikio makubwa kimalengo,kifedha...n.k,tumewafikia wengi kwa Programs zangu/zetu,nimetembea vijiji vingi kuzika watu,kutembelea wapenzi wa redio yetu na wadau,kuwatia moyo watu,na hata kuwa na muda wa furaha na wengie pia...pia huwa nafanya huduma kwa wanafunzi wa vyuo...uliza Mbeya, mwaka huu nimesukuma sana huduma,mfano mwezi wa tano/sita hapo karibu graduation za fellowship karibu vyuo vitano ndio nimekuwa Mgeni Rasmi,nimekuwa speaker kwenye matukio mengi ukiwamo uzinduzi...nimehudumu makanisa tisa tofauti nimefingisha ndoa kadhaa na moja imebakia, nimebatisa watu,nimefundisha semina na makongamano vyuoni na makanisani...kwa ujumla ulikuwa ni mwaka wa mafanikio kihuduma. Lakini hiyo haimaanishi hakukuwa na vikwazo aaah vilikuwepo vingi tu,kushindwa kulikuwepo pia, kukata tamaa nako,kuumizwa pia...but all in all TUNAPAMBANA KUTENGENEZA HISTORIA ILI ISOMWE NA VIZAZI VIJAVYO.

2.Tuna kamsemo huwa tunasema....Bora Zaidi ya Jana.Kamsemo haka kanakufanya uangalie ulichofanya jana then unajipa mtihani wa kufanya zaidi ya vile ulivyokuwa umefanya kabla.
2013 najipa kazi na kubeba gharama ya kufanya zaidi ya 2012 katika kila nyanja
kwenye huduma, Kikazi pia tumejipanga kuanza mchakato wa kuongeza masafa yetu"coverage".

3.Niwaambie marafiki...mafanikio hayatokei kwa mtu akiwa amejitenga mwenyewe..tunahitajiana.
Niko tayari kushirikiana na wengine..huku tukijenga mafanikio yetu...yaani kwa kuwa pamoja nao,mimi nitaendelea kujenga historia lakini na wao hawatabaki vile walivyokuwa...yaani wao wananihitaji mimi kutoka na mimi nawahitaji wao ili kutoka.
Tuendelee kushikamana.

Neema Ng'asha Mwamba
 Ni mwimbaji wa nyimbo za injili
1.Namshukuru Mungu ameniwezesha kurekodi video ya albam yangu, USINIPITE.
2.Mwaka ujao albam yangu itakuwa sokoni pia natarajia kurekodi albam nyingine na kufanya uzinduzi wa albamu ya USINIPITE.
3.Naomba ushirikiano wao kazi yangu ikitoka waipokee ili kuniwezesha kusonga mbele katika huduma.Nawapenda na Mungu awabariki sana


Thomas Luvanda
ni produzer wa nyimbo za injili kwa sasa yuko mkoani Ruvuma katika huduma hiyo
Asante. Jambo la 1 namshukuru mungu kwa kunipa kibari ktk huduma yangu ninyofanya kupitia huduma hii ya muziki pamoja na kazi za studio namshukuru Mungu nimepata mafanikio makubwa..sasahivi namshukuru Mungu nimepata tena kazi nipo huku Songea mkoa wa Ruvuma napo Mungu kanipa kibari kwa watu kila kanisa wananitaka niwafundishie vijana wao muziki alafu kwa dau zuri nimewapa ratiba wanakuja nawafundisha wanalipa vizuri haya bado studio wateja wanamiminika kila siku na tayari nina kieneo cha kujenga kibanda huku Songea kupitia huu mziki napia nina mifugo nafanya biashara kweli ni mambo mengi ambayo Mungu amenitendea siwezi kuyasimulia.

.jambo la 2 najiandaa mwakani mwanzoni kufungua studio yangu tayari kuna baadhi ya vifaa km sound card tayari nimeshaagiza kuna mshirika wetu hapa church songea ataniletea. Lengo kuukuza muziki jambo la mwisho ni kuwaambia mashabiki wangu wakae mkao wa kula bado nawakumbuka sana na ninafanya juhudi kila cku kuongeza ujuzi..sina mengi nawashuku sana Mungu awabariki sana muendelee kuniombea..Karibuni sana Songea


  • Abel Orgenes

    Huyu ni mtumishi wa Bwana mwenye mzigo na vijana wengi mtamkumbuka akiwa pale Vijana Center

    1. Mwaka huu namshukuru Mungu kwa ushirikiano mzuri na radio wapo kurusha vipindi vya mafundisho kwa mwili wa Kristo karibu mwaka mzima ambavyo vimejenga mwili wa Kristo na kuwainua kiroho maelfu ya watu, pamoja na radio kumekuwa na program za ana kwa ana, kupitia blogs na mitandao ikiwemo facebook hii imesaidia kuwafikia watu sehemu mbalimbali ulimwenguni ikiwemo Sweden, Uingereza, Marekani, Australia, Uganda, Kenya, Burundi, Congo, Africa kusini, Zanzibar nk. kuwasaidia wengi kuzaliwa mara ya pili, kuwatia moyo, kutoa ushauri wa Kiroho na maombezi kwa namna ambayo isingewezekana kutembea kote huko kwa Mwaka mmoja!


  • labda nitoe mfano mdogo wa ujumbe niliopokea bila kutaja jina lake " Bwana Yesu asifiwe mtumishi,ni matumaini yangu kuwa uko salama kwa neema ya Bwana wetu Yesu ww na babies wako wote including dada Rebeca.nimetamani tu kukusalimu leo na kukushirikisha jinsi ninavyobarikiwa nawe hasa ukizingatia kuwa sala zako kwangu na juhudi zako ndizo zilizosaidia mm leo hii kumjua Bwana wangu Yesu na uzuri wake ,wewe huwezi kujua lakini mm ndo naujua ukweli maaana uliniingiza katika group ya Bfamily kabla sijamjua Mungu ,kwa kuwepo ndani ya group na kusoma mara kwa mara updates za wapendwa hatimaye nami niliweza kumkiri YESU ,NAWIWA KUKUSHIRIKISHA KITU HIKI maana hata wapendwa wengine humu ndani hawakujua kama mm nilikuwemo humu kabla sijaokoka najua huu ni mpango wa Mungu kwangu kupitia humu nimebarikiwa na nimepata jambo jema WOKOVU i blessyu so much mo inJESUS name" hii ni moja kati ya shuhuda kadha wa kadha kupitia mitandao ya kijamii..."B" family kirefu chake ni Born Again Blessed Family.


  • Pia kwa mwaka huu kwa kushirikiana na wengine tumekuwa na Program za mafanikio mazuri za Aflewo nikiwa kama mlezi mmojawapo, Aflewo ni Africa Lets Worship, huleta pamoja waimbaji, wanamuziki, waombaji, wahudumu, wachungaji katika mchakato wa umoja na haimae kuwa na Mkesha mkubwa wa Kuabudu wa pamoja wa mara moja kwa mwaka wenye kuambatana na maombi juu ya Africa ambao ulifanyika May 4.
    Program zingine ni za Baynet pia nikiwa kama mlezi. Baynet ni Born Again Youth Network - huthamini na kuleta pamoja Vijana waweze kujitambua, kutiwa moyo vipaji vyao, kuimarishwa na kuunganishwa ili kufanikiwa na kuinuliwa kiroho, kinafsi na kimwili pia....kwa hiyo Baynet imeandaa mikesha kuingia mwaka mpya, mikesha katikati ya mwaka, day conference nk....


  • hayo nilikuwa najibu swali lako la kwanza!


  • jambo jingine la muhimu ambalo lilifanikiwa mwaka huu ni kufungua website ambayo bado iko kwenye matengenezo www.bfamilyministry.org


  • kwa mwakani 2013 ....
    1. tunakusudia kuboresha huduma ya "B"family zaidi kuweza kuandaa festival na makongamano/semina mikoani.
    2. Kuanza rasmi kanisa - ABC - Active believers Church (ni muhimu ku note kuwa hii ni tofauti na huduma ya 'B' family ministry.) maono ya kanisa ni kuwa na watu watendaji zaidi wa Neno na si wasikiaji tu au watu wa dini tu wakisubiri wachungaji/wengine wawafanyie kila kitu.
    3. Kuendelea kushirikiana na wengine katika mwili wa Kristo Aflewo, Baynet nk....


  • Mengine ya kuwaambia ni kwamba Bwana amutuita mimi na mke wangu kutengeneza jeshi la Bwana wa Majeshi, na kujenga/kuimarisha familia ya Mungu, pia ni waimbaji na wana sanaa kwa ujumla, pamoja na suprises ambazo siwezi kutaja hapa, tunakusudia pia kurekodi live Video....na pia kutoa mafundisho kupitia vitabu, cd, video na products zingine nyingi za "B"family ministry. mawasiliano yetu ni +255 754 36 30 96, abelorgenes@yahoo.com

  • Rungu LA Yesu

    Huyu ni mwimbaji wa nyimbo za injili za hiphop
    nashukuru sana kaka kwa nafasii hii adimu Mungu akubariki sana kwa hili...nilikua na mipango mingi wakati mwaka unaanza ikiwepo mipango binafsi na Mungu wangu na huduma yangu ki ujumla lkn nitaongelea sana kuhusu huduma ambapo nilikua nina mkakati wa kupanua wigo wangu wa huduma ili kuweza kuwfikia watu wengi zaidi..ninaweza kusema nimefanikiwa kwa kiasi chake  ingawa sijafika napotaka...namshukuru Mungu nimefanya huduma katika mikutano mingi ya nje pamoja na wachungaji wengi nikishirikiana na waimbaji wengine wengi kitu ambacho kimepanua wigo wangu wa huduma kwa kiasi kikubwa..hata mitandao ya jamii kama facebook imeniwezesha pia kupanua wigo wangu wa huduma,,watu ndo mtaji wangu,kama watu wasingekuwepo sijui ningekua namhubiria nani sio siri huwa napata furaha napokutana na watu wapya kila siku,iwe ni mchungaji,mwimbaji, mtu wa kawaida hata a friend request on facebook huwa naifurahia kwa sababu angalau napata mtu mpya wa ku share naye kile ninachokifanya....ki ujumlanamshukuru Mungu kwa hapa huduma yangu ilipofikia na watu alionpa mpaka sasa wanao support kwa njia moja au nyinginee hata wale wanaonpa challenge


  • mwaka ujao nina mipango mingi sana...habari ya kufurahisha ni kwamba mwaka huu nimeweza kurecord nyimbo nyingi sana katika studioz tofauti kwa hiyo mwakani nitaweza kuachia nyimbo nyingi zaidi ...mkakati wa kupanua huduma yangu uko pale pale ambapo nina mpango wa kushirikiana na wachungaji wengi zaidi katika mikutano ya nje na ndani katika matasha na ibada za jumapili sio siri mwaka huu nimweza kupanda katka majukwaa mengi ila kubwa zaidi ambalo linanpa hamasa ya kufanya zaidi ni kuweza kuandaa semina ambayo niliisimamia mwenyewe..mwaka huu namshukuru Mungu aliniwezesha kuandaa na kusamimia semina mkoani Ruvuma naamin hatua inayofuata itakua mkutano..binafsi nakaribisha watu wote wanaopenda kufanya huduma na Rungu la Yesu kwa wale walio facebook wanaweza kuni add kama rafiki au wanaweza kuwasiliana pia na Martin malecela mmiliki wa blog hiii


  • mwsho kabisa napendaa kuwaambia watu wote wanaoimpenda na kuni suport Rungu la Yesu na mimi nawapenda sana nyinyi ni watu wa thamani sana kwangu Mungu awabariki sana nawaomba tuwe pamoja pia naomba muendelee kutoa ushirikiano kwa watumishi wa Mungu katika kila jambo jema...
    ......mtumishi nashukuru sana kama kuna lolote usichoke kuniuliza au kunijulisha Mungu akubarikisaana yan saana 2

    MC Pilipili Emanuel Mathias
    Ni mwana vichekesho anayechekesha katika matamasha mengi ya kikristo na ni MC hapo juu akiwa na mc mwenzake samuel Sasali.
    Nimefanikiwa kufanya matamasha mbalimbail hasa ya fof na campus night za Mwanza na Singida,pia nimefanikiwa kujitangaza zaidi na kusimama sehemu mbalimbali na kuhudumu as mc ktk harusi na sherehe mbambali, kupokea mwaliko kwenda Uganda this december, kuchekesha tz nzima kupitia clouds fm na praise power radio, kuwasaidia vijana kutambua na kutumia vipawa vyao.


    Prezzor Fredy Chavala-The King
    Ni mwana vichekesho anayechekesha katika matamasha mengi ya kikristo na ni MC
     1. Ninamshukuru sana Mungu kwa uhai na uzima,zaidi nimeweza kufanya ziara nyingi mikoa mingi sana na kutambulisha Christian Comedy Tz, nimehudhuria makongamano ya vijana mengi sana kama si hivyo nimekuwa na ziara za ki-MC maeneo ya Moro,Mbeya,Singida,Arusha na Tanga mara nyingi zaidi kuliko kwingine....Namshukuru Mungu kuniwezesha na hatimaye sasa LAUGH AGAIN CONCERT SERIES imetimiza mwaka mmoja tangu nimeanza na katika kusherekea hilo ndio nafanya tamasha langu la mwisho kwa msimu wa kwanza ambao ndio unaisha sasa na tamasha la mwisho kwa 2012 na tamasha hili litakuwa tar 30th Dec 2012 kuanzia tisa alasiri mpaka saa mbili jioni pale ndani ya Hema la Victory Christian Centre tabernacle (VCCT)

    • 2. Kwa mwaka ujao kweli mipango ni mingi sana,kwanza ndio tunaanza msimu mpya wa mfululizo wa matamasha, na msimu huu nitafanya ziara kwenye vyuo vikuu na mashule zaidi maana nahitaji kupata vipaji vya kutosha,maana mpango mwingine ni kuanza vipindi vya TV,hivyo nahitaji watu wa kutosha...nitafanya matamasha makubwa ndani ya kumbi kama mawili tu na yote yatakkuwa ni kwa ajili ya kufanya recording!!...pia mwaka huu namwamini Mungu kuzindua album yangu ya Comedy songs, nitatoa vitabu vitano(hapa ni pamoja na viwili ambavyo ilishindikana mwaka huu)...mawsala ya filamu na mambo kadha wa kadha yanakuja....niatatoa DVD za Stand up comedy ili sasa watu waone wakiwa nyumbani....na zaidi nitakuwa nazindua label ya nguo zangu!!
       
      3. Kwa ndugu jamaa na marafiki,mashabiki na watu wote nataka nitoe shukrani zangu kwa jinsi ambavyo wananipa shavu,ahsante kwa kunipenda kwa kila anipendaye na ahsante kwa kunichukia kwa kila anichukiaye, nimetoa zawadi ya kalenda kwa yeyote anayehitaji,utaipata kwa pesa kidogo ili kuchangia huduma,ahsante vyombo vya habari vyote kwa support na hii namaanisha ni pamoja na hiki.....mwisho naomba niawatie moyo wote kutembelea Chavala Blogs Group na kujifunza mengi na kwa wale wa karibu zaidi, naomba kuwataarifu kuwa mwakani natarajia kuoa 29/09/2013 hivyo karibu kama ungependa kuwa mmoja wao!!! ahsante sana Martin malecela na Mungu akubarikini nyote,Amen!!


    Mungu awabariki woote kwa waliotoa ushirikiano 
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

Mungu awabariki kwa kazi nzuri katika mwaka mzima big up keep it up