Jumatano, 5 Desemba 2012

KATIKA KUAZIMISHA MIAKA 12 YA NDOA YAO MWL WILLBROAD PROSPER ATAZINDUA KITABU KIPYA CHA MALEZI KWA VIJANA

Ni watu wengi sasa tuna mfahamu mwl Willbroad Prosper ambaye yeye ukiacha taaluma yake ya ualimu lakini amekuwa mwl mzuri wa mafundisho malezi ya familia na ndoa kwa ujumla. mafundisho mengi ambayo amekuwa akifundisha sehemu mbalimbali hapa afrika mashariki, sasa ameamua kuwaweka kwenye kitabu ambacho mtu anaweza kununua na kuendelea kujisomea kitabu hicho ukiwa hata nyumbani kwako.

habari zilizoifikia blog hii kuwa kitabu kiko tayari na jumapili hii 09/12/2012 utakuwa ni uzinduzi wa kitabu hicho. pamoja na uzinduzi wa kitabu hicho pia mwalimu huyo ataadhimisha miaka 12 ya ndoa yao. katika ibada hiyo itakayofanyika katika kanisa la CITY HARVEST. Ambapo ibada hiyo itaanza saa 10:00 - 12:30 mchana. mwalimu ameomba watu wengi kuzitokeza katika uzinduzi huo na kuanzia siku hiyo vitaanza kuuzwa kwa sh 5000 tu ya kitanzania.
Mwl Willbroad Prosper

ifuata ni wasifu mfupi wa Mwalimu Willbroad Prosper alizaliwa mwaka 1968 katikawilaya ya Karagwe, mkoa wa Kagera. Ameoana na Grace prosper. Mungu amewabariki na mtoto anayeitwa James Prosper ambaye yuko darasa la tano. Ni mwalimu kwa taaluma katika masomo ya Kiingereza na Geografia. Amesoma elimu yake ya sekondari katika seminari ya St. Charles Lwanga katika wilaya ya Biharamulo. Amepata Diploma ya ualimu katika chuo cha Ualimu cha Dar es salaam. Amefundisha katika shule ya sekondari ya St.Anthony’s tangu mwaka 1996 mpaka 2001.

Amekuwa mwalimu Mkuu wa Capstone Christian School tangu 2002 mpaka sasa. Amefanya kozi mbali mbali katika taaluma ya ualimu, elimu ya Kikristo, uongozi, ushauri nasaha kwa vijana na wazazi hapa nchini na katika nchi za Uganda, Kenya na Afrika Kusini. Willbroad Prosper ni mwalimu wa Neno la Mungu katika malezi ya watoto na vijana pamoja na ndoa. Pia amefanya semina na makongamano juu ya vijana, malezi na ndoa kwa wazazi katika vituo vya redio na Luninga hapa Dar es Salaam na makanisa mbalimbali katika mikoa ya Mwanza, Kagera, Morogoro,Pwani, Tanga, Dodoma, Mtwara, Mbeya, na Kilimanjaro .

 Uzoefu wake tangu 1996 na karama alizopewa na Mungu katika maswala ya familia umemfanya afanye kazi pamoja na Family Outreach Tanzania (FOTA), Family Impact –Kenya na ni Mkurugenzi wa Tanzania Christian Talents (TCT). Kitabu hiki kitawafaa sana wazazi/walezi, wachungaji, vijana, walimu wa watoto na vijana pamoja na mtu yeyote anayetaka kuongeza ujuzi katika eneo la malezi
bora ya watoto na vijana.


Muonekano wa kitabu cha mwl Prosper.
Kwa maelezo zaidi au manunuzi ya vitabu kwa lejaleja au jumla unaweza kuwasiliana moja moja na mwl
wprosper.blogspot.com

Hakuna maoni: