Sara mvungi maarufu kama "Honey" katika tasnia ya filamu pia ni
mwimbaji wa nyimbo za injili siku ya Jumapili alizindua album yake ya
kwanza ya nyimbo za Injili iitwayo "NIACHENI NIMFUATE YESU",Uzinduzi
huo ulifanyka katika Kanisa la Akuzamu Ministry Posta katika Jego la
IPS.
Katika Tamasha hilo Mgeni Rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Mariedo Boutique
Rose Mary Edward ambaye ni mke wa Mchungaji Kiongozi wa Huduma Akuzamu
Ministry.
Uzinduzi huo ulisindikizwa pamojana na wanamuziki mbalimbali kama Enock
Jonas, Afande Bupeh, Msasani kwaya, Amani kwaya toka Yombo, Madam Ruth
na wengine wengi
Pia uliudhuliwa na wasanii wa Bongo Movie kama Irene
Uwoya,Dotinata,Tino Kutoka Star tv mtangazaji wa Kipindi cha Bongo Beat
Sauda Mwilima, ITV alikuwepo mtangazaji wa Kipindi cha Hawavumi lakini
wamo pia alikuwepo kuwakilisha bila kumsahau Maimatha wa Jesse.
Uzinduzi huo wa Album uliambatanna na uchangishaji wa fedha ambazo
asilimia flani zitakazo kwenda kusaidia watoto wanaoishi kwenye
mazingira .
Nikizungumza na Sara Mvungi kwa njia ya simu kanieleza kuwa Album yake
ina nyimbo 9,akiwa amewashirikisha waimbji wengine kama Enock
Jonas,Stela Swain a Mtoto wake aitwae Neema katika album hiyo
|
Mgeni
Rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Mariedo Boutique Rose Mary Edward akiwa na
Mme wake Mchungaji Kiongozi wa Huduma ya Akuzamu Ministry. |
|
Watumishi wa Mungu mbalimbali walioudhulia uzinduzi huo. |
|
Maimatha Jesse |
|
Kutoka Star tv mtangazaji wa Kipindi cha Bongo Beat Sauda Mwilima |
|
Kutoka ITV alikuwepo mtangazaji wa Kipindi cha Hawavumi lakini wamo aliye changia kwa kiasi kikubwa katika huduma ya Sara Mvungi |
|
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Afande Bupe |
|
Mtumishi wa Mungu Dotinata |
|
Irene Uwoya |
|
Vikundi mbalimbali vilialikwa kuhudumu katika uzinduzi huo |
|
Kwaya mbalimbali zilialikwa kuhudumu katika uzinduzi wa Sara Mvungi |
|
Wadau wengi walijitokeza kuhudhulia uzinduziwa huo |
|
Akabebwa na washabiki wake juu juu...! |
HABARI HII KWA HISANI YA
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671
AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni