Jumapili, 25 Novemba 2012

PROSPER MWAKITALIMA (MTOTO WA NABII)AFANYA TENDO LA KUMSHUKURU MUNGU KWA NAMNA YA TOFAUTI NA MFANO WA KUINGWA

Prosper Mwakitalima huwa namwita mtoto wa Nabii maana ni mtoto wa mchungaji wa siku nyingi pale Singida. namfahamu mtu huyu muda mrefu, hasa wakati wote tukiwa wapiga keybord katika kwaya zetu enzi hizo huko Singida. ni mtu asiye na makuu ni rafiki wa wote. ninafahamu mambo kadhaa ambayo Mungu amewahi kumtoa katika hayo moja wapo ikiwa ni kupona ugonjwa wa moyo ambao alikuwa nao utotoni na baadae kugundulika kuwa na tobo kwenye moyo wake. na hakati furani kwaya yao iliyovumaga na wimbo wao wa nyukilia waliangua kilio baada ya matokeo ya dr kuonyesha tatizo kubwa alilokuwa nalo ambalo lilionyesha kuwa asingeweza kuisha kwa muda mrefu. lakini Mungu si athumani yeye ni dr wa ma dr mweza wa yote kwa namna ya ajabu alipona kabisa tatizo hilo la moyo alilokuwa nalo na hata sasa anaishi.

mwaka jana lilitokea tukio la ajabu ambalo mtu yeyote kwa ufahamu wa kibinadamu si rahisi kuamini kuona mtu akitoka mzima bila hata mfupa wa kidole kuvunjiba ndani ya gari ambalo liligeuka chapati na hata zoezi la kumtoa lilichukua kama nusu saa hivi. lakini hapo napo Mungu alisimama kama Mungu kuokoa maisha yake, na kumpa maisha mengine tena.

katika wiki ambayo ilitokea ajari hiyo alishirikiana vijana wengine kuandaa tamasha la kihistoria ambalo halijawahi kutokea katika mkoa wa Singida ambalo lilikusanya watu wengi sana wengi wao wakiwa wanafunzi katika hoteli ya kitalii pale singida Singida motel. zaidi ya watu 5000 walihudhulia na ilipofika kipindi cha kuokoka vija wapatao 700 walikabidhi maisha yao kwa Yesu. hii ilikuwa ni furaha saana kwake na ni hivi aliandika kwenye page yake ya facebook
It happened on Singida Motel Grounds, approxmately 5,000 students and youths attended, and about 700 said yes to Jesus.It was a good way for me to celebrate what God did in my Life on 23rd Nov. 2011 (11 days after a big Dar Campus Night 2011), when He saved me from a fatal accident. This is the way I'll be honoring God for the rest of my Life.. winning souls to Christ. — in Singida, Tanzania.

ni mara chache sana mtu kushukuru Mungu kwa kuleta watu wengine kwa Yesu. kama vijana tunatakiwa tuwe na kiu ya vijana wenzetu kumjua Yesu wengine hawajaokoka kwasababu tu hawajapata wa kuwaeleza habari za Yesu, tusichoke kuwaambia watu habari za upendo wa Yesu

yafuatayo ni picha za tukio lenyewe ndani ya singida motel


Timu iliyoongoza uimbaji katika tamasha hilo kubwa The best singers team si wengine ni Riversof Joy International wakiwa on the stage

Event kama hizi huwezi ukakosa kumuona papaa wa sebene samuel sasali swahiba mkubwa wa prosper

Full shwangwe watu kibao

askari jasiri akiwa kazini kumwaibisha shetani

Pro, Wambula na Prezzo chavala wakiwakilisha

kama kawaida Pastor Nkone anayependa vijana akitoa suport ya kutosha kwa vijana wake

 mass choir kutoka Singida on the stage

picha kama hizi ni adimu sana utadhani Bolt anaanza mbio kumbe ni wambula akishusha sebene la nguvu

vijana zaidi ya 700 wakisalimisha maisha yao kwa Yesu

hili gari za prosper pamoja na kuwa hivi lakini kijana alitoka mzima

mamia ya watu wakishangaa gari dogo likiwa limekandanizwa na gari kubwa juu lakini mtu alitoka mzima utukufu kwa Yesu

mtoto wa nabii katika pozi

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: