Kumezuka ghasia zaidi nje ya ubalozi wa Marekani mjini Cairo
kati ya polisi na waandamanaji wanaokashifu filamu ambayo wanasema kuwa
inakejeli imani ya Kiislamu.
Nchini Yemen waandamanaji wamevamia ubalozi wa Marekani wakichoma moto magari kabla ya vikosi vya ulinzi kuwadhibiti kwa kuwafukuza kutoka eneo hilo.
Maandamano zaidi pia yamefanyika katika nchi za Tunisia, Morocco, Sudan, Mauritania na Iran.
Wakati huohuo maafisa wa Marekani wanasema serikali ya nchi hiyo inachunguza ikiwa mashambulio ya jumanne kwenye ubalozi wa Marekani katika mji wa Libya wa Benghazi yalikuwa ni ya kupangwa au la .
Balozi wa Marekani nchini Libya , Christopher Stevens, aliuawa .
Maafisa wa Marekani wameelezea mashambulio hayo kama yenye utata na yenye kupangwa kitaalamu na kuna tetesi kwamba makundi ya jihad huenda yalihusika .
Awali ilifikiriwa kuwa mashambulio hayo yalikuwa na uhusiano na maandamano ya kupinga filamu iliyokuwa inamkejeli Mtume Mohammed.
Takriban waandamanaji mia mbili wamekusanyika karibu na ubalozi wa Marekani mjini Cairo Misri kwa usiku wa pili kuelezea hasira yao juu ya filamu hiyo .
Watu wenye silaha waliokuwa na maguruneti walichomo moto jengo la ubalozi na walioshuhudia wanasema watu hao walizingira eneo hilo.
Rais Obama amelaani vikali shambulio hilo na ameahidi kushirikiana na serikali ya Libya kuwafikisha mbele ya sheria wahusika
ANGALIA BAADHI YA SEHEMU YA PICHA HIYO
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Maoni 1 :
ndugu zetu waislam wamekosa uvumilivu hasa kumuua balozi wa usa libya kwa inshu ya hiyo video wakidhani wanamtetea Mungu, kumbe hakuna mwanadam awezaye kumtetea ila yeye mwenyewe! kwani! wale wote wanaofanya dhambi Mungu anashindwa kuwazuia? hasha anao uwezo wote! sasa, kama wameona kuwa kwa kutoa video hiyo ni kumkashif mtume wa Mungu kwa nn wacmuachie Mungu ahukumu?
Chapisha Maoni