Jumanne, 21 Agosti 2012

MIRIAM LUKINDO MAUKI NA CHRISTINA SHUSHO KUPAMBA UZINDUZI WA KWAYA YA SAUTI ZA SIFA. UKONGA JUMAMOSI HII

MWIMBAJI wa muziki wa Injili nchini, Miriam Lukindo Mauki ‘Binti Afrika’ Jumamosi hii anatarajiwa kuiteka Matembele ya Pili, Ukonga jijini Dar es Salaam atakaposhiriki uzinduzi wa albamu mbili za kwaya ya Sauti za Sifa iliyo chini ya Huduma ya The Word of Reconciliation Ministries (WRM).


Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwalimu wa kwaya hiyo, Elibariki Isango, alisema, Miriam amekubali kuungana nao na siku hiyo atapanda jukwaa moja na Christina Shusho kuimba, wakati wa uzinduzi wa albamu zao hizo ambazo ni ‘Enendeni kwa Roho’ na ‘Pokea Sifa’.

“Miriam amekubali kuja kutuunga mkono katika shughuli yetu ya kuzindua albamu zetu mbili na ataungana na Shusho kuimba nyimbo zao mbalimbali, hivyo naomba wakazi wote wa Dar es Salaam na vitongoji vyake, kufika kwa wingi kwenye uzinduzi huo,” alisema Isango.

Mwalimu Isango alisema kuwa, lengo la uzinduzi wa albamu hizo ni kukusanya fedha kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la huduma hiyo, ambalo kwa sasa lipo katika hatua za mwisho, hivyo kila atakayefika katika uzinduzi huo na kununua CD zao, atakuwa ametoa sadaka yake ya kukamilisha hekalu la Bwana.

Waimbaji wengine watakaoimba kwenye uzinduzi huo ni Ami Mwakitalu, Madame Luti & Chris, Faraja Moleli, Queen Talaba, Wilson John, Magreth na wengine wengi, ambako shughuli itaanza majira ya saa 6:00 mchana na kumalizika saa 12 jioni.

Mwalimu Isango aliongeza kuwa, hakutakuwa na kiingilio katika uzinduzi huo, hivyo wadau wa muziki wa injili, hasa wanaoishi maeneo ya Kitunda, Ukonga na Gongo la Mboto kufika kwa wingi, kwani hiyo ni mara ya kwanza kwa waimbaji kama Shusho na Miriam kuimba eneo hilo.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: