Alhamisi, 16 Agosti 2012

DON MOEN NA WENZAKE WAFIKA SALAMA ILA NICOLE AIBIWA LAPTOP

wana muziki maarufu wa gospel kutoka Marekani waliokuwa Dar kwenye Tamasha kubwa la kihistoria la ipende Tanzania, lililoisha jumapili wamesafiri salama ijapo Nicole katika ujumbe wake kwenye FB amesema kuwa laptop yake imeibiwa, mazungumuzo ya wote kwenye fb yanaonyesha kuwa walifurahi kuwepo TZ na kufurahi jinsi watu wengi walivyojitokeza katika tamasha hilo.
Nicole akiimba kwenye tamasha Dar Jumapili iliyopita

huku Don Moen siku ya jana ameonekana kuwepo kazini kwake akiwa katika maandalizi ya albamu mpya ya Chrismass katika maelezo yake amesema kuwa hiyo itakuwa ni albamu yake ya kwanza inayohusu Chrismass

                              Don akiongea na producer wake anayeandaa albamu ya chrismass

                               wapiga muziki wakiwa kazini kupiga muziki kwa kufuata note

              Don alifuatililia sheet ya muziki na kurekebisha sehemu zinazohitaji kurekebishwa

                           Don akisikiliza muziki unaopigwa na wanamziki na kufuatilia note

                                             hapa Don alipokuwa viwanja vya jangwani

                         Kiongozi wa wana mziki akiongoza upigaji muziki wakati wa kurekodi.

kwa picha hizo hapo juu utakubaliana na mimi kuwa mziki ni elimu muziki ni gharama. iwe changamoto kwa waimbaji wa injili hapa kwetu kama tunataka kubalika kimataifa.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: