Jumatano, 25 Julai 2012

KANGA MOKO, NDEMBE DEMBE WATAFUNGIWA LINI? MCH GERTRUDE NA WABUNGE WENGINE WAHOJI BUNGENI

BAADHI ya wabunge jana walikijia juu kikundi cha burudani cha Khanga Moja Ndembendembe, kwa madai ya kukiuka maadili ya Mtanzania na kuitaka Serikali ieleze ni lini kikundi hicho kitapigwa marufuku.
Mch, Mh Dr Gertrude Rwakatare

Mbunge wa Viti Maalumu, Mwanamrisho Taratibu Abama (Chadema) anayetokea Zanzibar ndiye aliyeanzisha hoja ya kuitaka Serikali ikifungie kikundi hicho.
Akichangia mjadala wa hotuba ya makadirio ya bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mwanamrisho alisema pamoja na watu wenye fedha zao kwenda kuangalia kikundi hicho, lakini muziki wake na namna wanavyocheza vinakiuka maadili.

“Nataka Waziri akija hapa, aseme amekifungia kikundi hicho au vipi,” alisisitiza Mwanamrisho.
Bada ya kumaliza kutoa hoja hiyo iliyoonekana kushangiliwa na wabunge, Mbunge mwingine wa Viti Maalumu, Mchungaji Getrude Rwakatare naye aliibua hoja hiyo.
Mchungaji Rwakatare alisema wanenguaji wa kikundi hicho mbali na kucheza wakiwa wamevaa khanga moja, pia khanga hizo huwa zimelowanishwa maji.
“Tena wanalowanisha maji hizo khanga wanazovaa mabinti, wanafanya minenguo kiasi kila kitu kinaonekana wazi…huu ni mchezo ambao ukichezwa, watu wanafurahia na wanakwenda,” alisema Mchungaji Rwakatare.

Alisisitiza kuwa mchezo huo unakiuka maadili na kuwataka wananchi hata kama hawafuati maadili ya dini zao, basi wafuate maadili ya taifa.
Kuhusu filamu, Mwanamrisho alisema filamu za Tanzania sasa hivi zinaangaliwa na watu wengi lakini zimekosa maadili na wanashindwa kuziangalia na watoto.
“Hizi filamu zinaashiria ushoga na usagaji, nataka Waziri akija kujibu hoja aseme ni ngapi amezifungia?” Alihoji Mwanamrisho.

Naye Mchungaji Rwakatare, alisema katika vipindi vya televisheni, habari zinapewa muda mfupi huku vipindi vya muziki na tamthiliya vikipewa muda mrefu wakati havina mafundisho.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: