Jumatatu, 23 Julai 2012

HATIMAE MKUTANO WA INJILI TAG TANDALE WAISHA KWA AMANI. POLISI WAIMALISHA USALAMA. WALIOFANYA FUJO WAOMBA MSAMAHA

Mkutano wa injili ambao jana uligubikwa na fujo na kijana wa kiislamu uliofanyika Tandale kwa Tumbo umeisha leo kwa amani. mkutano huo ulioandaliwa na section ya Magomeni jana uligubikwa na fujo mpaka kupiga simu polisi na kutuma gari iliyokuwa na askari kama 8 waliokuwa na siraha ili kuimarisha usalama. pamoja na kuimarisha usalama lakini kijana mmoja anaeitwa Joakim anayesali kanisa la TAG magomeni alipigwa ngumi ya nguvu kwenye taya na kusababisha kupelekwa hospitali na kung'olewa jino moja la kushoto chini. jana baba mzazi wa kijana huyo aliwafuata waadaaji wa mkutano huo ili kuomba msamaha baada ya kupata taarifa kuwa kijana wake kawafanyia fujo walokole na kijana wake anatafutwa na polisi.
Mwinjilisti Sote akihubiri

pamoja na mzazi huyo kuomba msamaha pia wale bodaboda wenzake na muanzisha fujo nao walimfuata shemasi Baltazary na kumuomba msamaha na kusema kuwa wao hawakupata taarifa sahihi kwa mwenzao na kumsaidia kufanya fujo ambazo baadae walipotafakari wameona wamefanya makosa. waandalizi wa mkutano leowalikuwa busy ili kukamilisha umalizaji wa mkutano hivyo ilikuwa ni vigumu kupata taalifa kutoka kwao. hata hivyo hakukuonekana namna yoyote ya kutokea vulugu. watu walikuwepo wengi na mkutano ulimalizika vizuri.

Mwinjilisti Sote aliona jukwaa ninamnyima uhuru na aliamua kutelemka chini


Watu wakiwa wamejaa kusikiliza neno.


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: