SCOTT
ROSS: Ulikuwa na miaka mingapi ulipokuwa una igiza filamu?
JIM
CAVIEZEL: Inavutia. Siku
nilipo kubali jukumu, nilipokea simu kutoka kwa Mel. Akasema, habari, mimi ni
Mel.' 'Mel yupi?, Mel Gibson, Tom cruise, hivi ndivyo nilivyo wafahamu. Sikuwafahamu
kwakuwa ilikuwa ndo mara ya kwanza kusikia jina la kikundi hicho. Akasema, mimi
ni Mel. 'Akaanza kunielezea kuhusu filamu hiyo na majukumu ambayo alitaka
niyafanye katika filamu hiyo.
SCOTT
ROSS: Ulizungumza nini kuhusu hilo? Na hasa
baada ya yeye kulileta kwako?
JIM
CAVIEZEL: Siku iliyo fuata, alinambia,
'Nataka uwe makini sana kwa kile ambacho utaenda kukifanya. Hauta kifanya tena.'Alilisema
hili mara nyingi kwa uwazi. Nika mwambia, 'Mel, hichi ndicho ninacho amini.
Kila mtu ana msalaba anatakiwa aubebe. Inanibidi ni bebe msalaba wangu binafsi.
Kama tusipo kubali kubeba misalaba yetu tutaumia. Kwahiyo twende tukafanye kazi
hiyo. Na ndipo tulipo anza kuandaa filamu hiyo
SCOTT
ROSS: Ulikuwa una umri gani?
JIM CAVIEZEL:
Nilikuwa na umri wa miaka 33.
SCOTT
ROSS: Awali Ulilichukuliaje swala hili?
JIM
CAVIEZEL: Kiukweli nilivuta puumzi, huku
nikiwa na hofu. Nilikuwa nalifikiria swala hili kila wakati.
SCOTT
ROSS: Situ kwasababu wewe ni msanii, lakini
je ulijiandaaje kuigiza kama mwana wa Mungu?
JIM
CAVIEZEL: Ni swali zuri. Kuwa
nilijiandaaje? Kwa moto. Nyuma kulikuwa na maneno mawili, yenye ‘Moto
usiozimika,’ kilichokuwa kigumu ni kwamba kuumia kulikuwa halisi. Nilikuwa nikianza kuanzia saa 8 usiku
mpata saa 10 alfajiri nikiwa mwenyewe mahali pale, ilikuwa ni nafasi mbaya, situ
mbaya pia lilikuwa ni nafasi iliyo nifanya niwe na wasiwasi. Sikuweza kukaa
hata chini. Kadri siku zilivyokuwa zikienda, niliugua, pia mabega yangu yalikuwa
kama yametenganisha, ilinilazimu kufanya maombi. Nilifanya hivyo nikimaanisha
kabisa nikiwa kama punguani.
SCOTT
ROSS: Unasema uliingia kwenye maombi. Je
uliamini ulicho kuwa ukiomba kutokana na nafasi ulioicheza? Wewe ni mwamini?
JIM
CAVIEZEL: Vizuri, hapakuwa na swali kama
niliamini. Nafikiri watazamaji wako wengi wanelewa kuhusu kile ninacho kisema.
Kwa nini kuwekewa masharti mwenyewe kwa mateso isipokuwa wewe kujua kwamba hiyo
ni kweli? Ngoja ni kwambie,nilikuwa msalabani. Watu wengi walinitazama, naigiza
kama Kristo, lakini mara nyingi nilijihisi kama Shetani. Nilikuwa na matusi yakitaka
kunitoka. Ilikuwa ni ya baridi ilikuwa ni kama visu vinaingia ndani yangu.
Sijui kama umewahi kushughulikiwa kivile, Siku ile nilijisikia baridi sana
sikuweza hata kusema. Kinywa changu kilikuwa kikitetemeka sana. Mikono na miguu
yangu iliumia sana. Nilizimia pale msalabani. Kwa nusu ya muda, watu walikuwa
wakinitazama huku wakicheka.
SCOTT
ROSSS: Ilikuwa kweli kupita
miongoni mwawatu mkiwa na kundi la watu?
JIM
CAVIEZEL: Hapana, tulikuwa na watu wanao jua
huzuni katika hali ya ubinadamu, tulikuwa na watu wenye majonzi,
wenye utofauti, na ni watu ambao walikuwa wameguswa na tukio. Kuangalia vile
kiubinadamu nilitamani hata kupasuka, nikasema waambieni hao watu wakae kimya,
au waondoke.
SCOTT
ROSS: Je haikuwa kinyume sana kwa
yale waliyomfanyia, na Yesu kuwasamehe maadui zake?
JIM
CAVIEZEL: Unafikiri katika hatua hiyo utafanya nini? mimi ni fundi, mimi
ni muigizaji. Kwa kumaanisha niliingia kwenye maombi, hayakutoka kwenye ufahamu
wangu, yalitoka kutoka ndani ya moyo wangu.
SCOTT
ROSS: Wakati unachapwa viboko na kupigwa makofi ilikuwa ngumu kuangalia
kwa sababu ilichukua muda mrefu. mimi nilijaribu kuhesabu mapigo. Nilivyo waangalia
watu katika ukumbi wa michezo mbele yangu, nikaona wakigeuza mbali nyuso zao
kwa sababu hawakuweza kuendelea kuangalia.
JIM
CAVIEZEL: Umesema kitu muhimu sana: Watu waligeuza nyuso zao mbali walipo
kuwa wakiangalia. Kile walichokuwa wakikiona ni dhambi zao. Sikutaka
kushughulika, mara kwa mara, na dhambi zao wenyewe. Ndio maana ni ngumu sana
kuangalia. Lakini filamu hii inakulazimisha wewe mwenyewe kujiona, si vile
unavyotaka kujiona mwenyewe, bali kamavile Mungu anavyo kuonano wewe.
SCOTT
ROSS: Ni sehemu gani ya filamu hii likuwa na
athari kubwa kwako?
JIM
CAVIEZEL: Kijana acha niwemkweli kuna vitu ambavyo nilivipitia, ni ngumu
hata kuvielezea. Nilihisi kama uwepo mkubwa ulikuja ndani yangu wakati
tulipokuwa tunaigiza sinema. Yale maombi niliyokuwa nikiomba, sikutaka watu
wanione mimi, nilitaka wao wamuone Yesu. Na kupitia vile wokovu utapatikana.' Hicho
ndicho nilihitaji kuliko kitu kingine, kwamba watu kuona matokeo na hatimaye
kufanya uamuzi wa kumfuata yeye au la.
SCOTT
ROSS: Na huo ndio uchaguzi tu, ama kufanya
au la. Waigizaji wengi wamekuwa wakishitushwa na filamu ya mateso ya
Yesu (The Passion of The Christ). Lakini wachache tu hutambua umuhimu
wa kufanya filamu hii. Ni pamoja na Jim
Caviezel mwenyewe. Caviezel alienda kumsaidia mtayarishaji wa 700 Club huko
Scott Ross iliaelewe kwa undani zaidi nini maana ya kucheza filamu ya
kusurubiwa kwa Mwokozi.
SCOTT
ROSS: Filamu
ilikuwaje?
JIM
CAVIEZEL: Nakumbuka kipengele kimoja wakati naigiza mateso ya Kristo,
“unaweza usijali lakini kwetu sisi ilikuwa ni hatari yamkini hata kuvunjika
migongo” “Wakati ule msalaba unayumbayumba, na nilikuwa juu ya jabali yapata
futi elfu moja. Kama lile jabali lingeli bomoka ingekuwa ni hatari kwangu. Na
Mel hakuwa na lakufanya, tulikuwa ndo tuko katikati ya tukio lililokuwa
linachukuliwa mkanda kwa wakati ule, na ghafra ulitokea upepo uliovuma kwa
nguvu,na kusababisha mlsalaba kuyumbayumba sana nilipokuwa pale juu, japo
msalaba ulikuwa umeshindiliwa vizuri lakini sikujihisi kama ni salama na upepo
uliendelea kuvuma, na nilikuwa nikiumia kila upande, mabega yakatenganishika,
sijui kama umewahi kupitia hata moja ya hayo.
Lakini
nilifikiri tumefanikisha, siku iliyo fuata tuliangalia filamu hiyo na
ilionekana nzuri sana, Lakini Mel akasema, “Hatuta itumia hii.” Nikasema
“Unamaanisha nini kusema hatuta itumia hii?”. Akasema “Kama watu wataangalia
msalabani hawata muona Yesu, watakuwa wakiona tu msalaba unayumbayumba. Sahau
hii tunaanza tena” ikatuchukua wiki nyingine tano kwaajili ya kipande hicho cha
kusulubiwa peke yake.
SCOTT
ROSS: Huzuni kweli.
JIM CAVIEZEL: Hiyo ni kwaajilii ya kipande
cha kusulubiwa.
SCOTT ROSS:
Katika sehemu ya kwanza ya filamu hii nabii Isaya Alisema
kuwa Yesu alipigwa, alichubuliwa na alipondwa kiasi kwamba ilikuwa vigumu
kumtambua kama yeye ni mtu.
JIM
CAVIEZEL: Hatukuweza kufikia kiwango hicho. Na hatukuenda kwa undani
zaidi kwa vile tulivyo soma, tulifanya kwa sehemu tu. Tulitaka angalau watu
waweze kumwona kuwa ni mtu. Kwa sababu kuna kitu kuhusu jinsi gani inaweza ikapoteza
mvuto kwa watu kuangalia na hatukutaka iwe hivyo.
SCOTT
ROSS: Pia sijui kama ilikuwa kweli au la!, ulipokuwa uanaigiza
ilikuwa kama unapigwa na umeme vile, hii ilikuwa ni kweli?
JIM
CAVIEZEL: Nilikuwa natoa hotuba nikiwa mlimani,
nilifikiri ule moto utaniumiza kwa dakika nne kabla haujatokea. Nilifikiri
“Ungeweza kuniumiza”. Na wakati ulipotokea niliona
manyasi katika aridhi yakinyauka.
Walichoona
ni kwamba moto ulikuwa ukija kutoka upande wangu wa kushoto na kulia mwa kichwa
changu. Ukaning’alizi mwili wote, na walipoendelea kuchukua video wakasema,
“unaonekana katika kamera?” kilichotokea wakati Mel amesema “action” kamera
zote zikanielekea na kunimulika na hapo ndipo mianga ilitokea. Na wakati kamera
zikinielekea, nilimsikia Mel akipiga mayowe, “Nini kimetokea katika nywele
zake?” Nilionekana na fanania na staili ya nywele za Don King.
JIM CAVIEZEL: Baada ya kuumizwa kwa dakika tano hivi, Jon Mikalini, ambaye ni msaidizi alikuja na kuniuliza uko safi? Naye akaumizwa, utofauti ulikuwa kwamba wa waliona tu ile bolt ikishuka na kumpiga Jon; hawakuweza kuona kule nilipokuwa nimesimama. Nilihisi kuumizwa kwa kiasi kikubwa sana katika masikio na macho.
SCOTT
ROSS: Ulifanya miujiza pale ulipokuwa
umeketi. Unaisifiaje miujiza hiyo?
JIM
CAVIEZEL: Yeah. Ni kweli palitokea miujiza mingi sana kuliko ile iliyokuwa
tayari kufanyika, pamoja na kuumizwa na ile miale ya mwanga, pia Jon naye
alikuwa tayari ameumizwa pamoja na kijana mmoja. Lakini miujiza iliyotendeka
ilikuwa mingi kuliko miujiza mingine.
SCOTT
ROSS: Ulipokuwa umeketi?
JIM
CAVIEZEL: Mmoja wa vijana tuliofanya nao filamu
hii alikuwa muislam. Yeye alikuwa miongoni mwa wale askari walionipiga, aliamua
kubadili dini na kuwa mkristo, alikuwa ni muislam mwenye uzoefu
wakutosha,unajua.
Ujue
kilichotokea ni kwamba tulikuwa na wakati wakutosha wakufanya maombi tulipokuwa
tukiendelea kuigiza filamu hii, na alikuwa anaomba kweli, na kutuombea
tulipokuwa tukiendelea kufanya kazi.
Waigizaji
wote walioigiza filamu hii, Baadhi yao hawata amini, lakini nafasi itaendelea
kuwepo kwaajili yao.
SCOTT
ROSS: Unafikiri kufanya filamu hii itakusaidiaje katika kazi yako?
JIM
CAVIEZEL: Hichi ndicho ninachojisikia. Na fikiri ilikuwa sahii mimi kuitwa
kuja kufanya filamu hii, nikitazama marafiki zangu wa kimarekani na wengine
wote duniani, nawaambia waonyeshe imani zao hadharani pasipo kuwa na aibu
yoyote. Na ndicho nilichokifanya mimi katika filamu hii. Sifahamu itakuwaje, lakini
sita badili mtazamo nitaendelea kufanya kazi hii, na nibado muigizaji, na
nitaendelea kuwa muigizaji, hata kama nitapata kazi nyingine ua la!. Nimemaliza
kazi yangu. Sasa nimetambua kuwa nilikuwa sahihi, na ilikuwa nafasi yangu, na
ninaweza kufanya filamu nyingine ambazo ninzuri zaidi.
JIM
CAVIEZEL: Kupitia hii, watu wanapo kuwa ndani ya kristo nakutoka nje ya
kristo, na wasioamini wakiwaona. Wana sababisha watu kumkataa, lakini wapo wengine
huishi maisha ya kikristo ya kumaanisha wakijua thamani ya mwili wa kristo. Kwa
watu kama hao kwao inakuwa ni zaidi ya kumaanisha. Vijana wengi wa kiyahudi
wamekuwa na hofu. Watu wa kiyahudi walinijia na wengine walikuwa wakinitumia
barua pepe wakiniambia, ‘Jim,’ umewahi kusoma haya mambo? Yana ogofya. Hatukumuua
Kristo, Nikawaambia, ‘Hapana, watu walisimama mbele ya Kristo na pilato wakati
wa mashitaka wakisikiliza mashitaka yaliyo tolewa na watu wakitaka Kristo
auwawe na sio ninyi, lakini pia dhambi zangu na zetu zilisababisha Kristo afe
msalabani, naelezea kitu hiki kwakuwa ni muhimu sana watu waelewe. Napenda wayahudi
waangalie filamu hii. Na watu wa imani yangu pia. Napenda wapagani na wasio
nadini waangalie filamu hii, filamu hii haipo kwa ajili ya kulaumiana. Wote tunahusika
katika kifo cha Kristo.
wakati mwingine tuonane ili usome historia yake kama mzeza filamu na historia ya picha ya The passion of The Christ. Ubarikiwe
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni