Jumamosi, 26 Mei 2012

FLORA MBASHA MTAALAMU WA MUZIKI WA INJILI, AMEPATA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI HIYO. SASA ANAMILIKI STUDIO.


Mafanikio ya mtu siku zote hupanga na Mungu, japo pia juhudi binafsi zinahitajika. Flora Mbasha ni mwimbaji mwenye makeke na anaye jituma katika kazi yake akiwa amebahatika kuwa na kibali katika jamii kutokana na ujumbe ndani ya nyombo zake kuwa na mguso wa aina yake kwakila anaye fanikiwa ksusikiliza ama kuona video zake.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Flora Mbasha

Mwimbaji huyu yuko katika ziara nchini marekani baada ya kupewa mwalioko na balozi wa nchi hiyo, ikiwa ni moja ya mafanikio katika kazi. Alizaliwa juni mosi mwaka 1983 katika Hospitali ya Hindu Mandal mjini Mwanza. “Baba yangu anaitwa Henry Joseph Mayalah ambaye kwasasa ni marehemu”. “ Mama yangu anaitwa Caroline Moses Kulola. Katika familia yetu tume zaliwa watoto watano, wakiume ni mmoja aitwae Benjamini na wakike tupo wane, mimi nikiwa wa pili kuzaliwa, akafuata Dorcas, Susan na wamwisho akiwa ni Ester. Sisi ni wasukuma wa Sengerema wilaya ambayo imo ndani ya mkoa wa Mwanza. Flora amekulia katika maadili ya dini ya Kikristo, ambapo babu yake akiwa ni Askofu Mkuu wa kanisa la Evangelistic Assemblies of God ambao ndio waliomlea.

“Babu na bibi yangu mpenzi, Elizabeth ndio walionilea kwa pamoja wakishirikiana na mama yangu mpendwa,”Anasema “Nilianza kuimba nikiwa darasa la tatu wakati huo nilikuwa nikienda na mama zangu wadogo kwenye kwaya hadi nilipokuwa na umri wa miaka kumi na tatu na ndipo nilianza rasmi kuimba kwaya ya kanisa na kuimbisha baadhi ya nyimbo.” Mwanamuziki huyo aliyeolewa na Emmanuel Mbasha, anasema aliolewa akiwa mwambaji katika bendi ya Word Alive na baada ya kufunga ndoa Septemba 22, 2002 walianza kuimba pamoja. “Mungu alitusaidia mwaka 2003 nikajifungua binti mrembo aitwaye Elizabeth, jambo hili hunifanya nimshukuru sana Mungu kwakutupa mtoto huyo.
Flora Mbasha akiwa na mumewe Emanuel

Mwaka 2004 nilifanikiwa kurekodi albamu yangu ya kwanza niliyoiita ‘Jipe Moyo’ ikiwa na nyimbo 10. Anasema kuwa akiwa motto alipenda san asana kusikiliza nyimbo za dini kutokana na familiya yao kuwa katika mazingira ya kidini zaidi. Kama hiyo haitoshi alikuwa akifuatilia kwa ukaribu sana nyimbo za mwanamuziki Maria Carey na Celine Dion.
Flora Mbasha akiwa na babu yake Dr Moses Kulola askofu mkuu wa kanisa la EAGT
Flora Mbasha akiwa makao makuu ya voice of America Radio nchini Marekani kwa mahojiano.
“Vibao vya wanamuziki hao vilikuwa vina ukosha moyo wangu na kunifanya niwe na kazi ya  kuzirekodi nyimbo zao kasha kuziimba kwasauti ya juu kama wao. Kwakuwa sikuwa naelewa kama kufuata nyimbo za kidunia nilikuwa nafanya makosa bali nilikuwa najifunza hasa sauti zao”alisema. Anaongeza kwakusema kutokana na kuvutiwa na uimbaji wao alilazimika kununua daftari na kuziandika nyimbo hizo na kuzikariri akawa na kazi ya kuziimba hasa nyakati za usiku alikiwa halali mapema kwa sababu ya kuimba nyimbo zao.
Flora Mbasha akiwa na barozi wa Tanzania nchini Marekani alipomtembelea ofisini kwake
Flora anasema; “Naweza kusema kuwa wasanii hao ndio walimu wangu wa sauti kwa sababu kipindi hicho nilikuwa naimba njimbo kwa kii ya juu ambayo waimbaji wengi inawashinda, na ndiyo maana mpaka leo hii nyimbo zangu huwa naziimba kwa sauti ya juu sana kisha nashuka.” Kama hiyo haitoshi, Flora anaongeza kwa kusema kuwa alipokuwa motto alikuwa anapenda kucheza  ngoma za asili hasa alipokuwa shuleni. “Kila niliposikia kuna maandalizi ya tamasha, kongamano ama Umitashumita nilijawa na furaha moyoni mwangu na nilikuwa nafanya mazoezi kwa kujituma kiasi kwamba walimu na wanafunzi wenzangu walinipenda”, anasema Mwimbaji huyo alipenda sana awe injinia wa kompyuta na umeme, japo ndoto hii haija timia ipo siku atapiga kitabu kwa lengo la kuyafanikisha malengo yake. “Kuna baadhi ya watu wanadai kutonielewa kwa sababu wakati mwingine nime kuwa naijichanganya na wanamuziki wa kimataifa na hasa niliposhiriki tamasha la ‘Zinduka’ hivi karibuni. “Mimi kuwa mwimbaji wa injili hakunizuii kushiriki katika matamasha  yenye lengo la kulitetea taifa, hasa kwenye kampeni ya kupambana na Malaria,”anasema. Mwanamuziki huyo anasema kuwa anamatarajio mengi sana ya kufanya kuhusiana na suala la muziki lakini akiwamo kutoa albamu nyingine, hata hivyo asilimia 90 ya maisha yake anategemea muziki na kazi yoyote zaidi ya kufuga kuku wa nyama. Na kwasasa nimefungua studio ya kurekodi nyimbo za injili, alisema.
Flora Mbasha akifanya mazoezi na wazungu nchini Marekani
habari kwa hisani ya gazeti la Tanzania Daima
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: