Askofu David Oyedepo |
Mwanasheria huyo aliiomba mahakama kumpa adhabu Askofu huyo kwa kutoa jumla ya sh billioni mbili za Kinaigeria kama mfano na kumlazimisha Askofu huyo kuomba msamaha wa umma na katika magazeti ya kila siku na katika televisheni ya nchi hiyo.
Mwanasheria wa kanisa hilo alisema kuwa yeye na washiriki hawawezi kumshitaki, Askofu Oyedepo kutokana na misingi ya sheria la kanisa lao, lakini wanasheria walibainisha kwamba kwasababu ya kukiukwa kwa haki za kimsingi za binadamu ilimpasa atiwe hatiani. Awali ya hapo Askofu huyo alisha wahi kuwasilisha sheria hii ya kuchapa makofi waumini katika kanisa lake kuwa ni kitendo cha kudhibiti uharibifu ndani ya kanisa katika, Sura ya 4 ya Katiba ya mwaka 1999 na Mkataba wa Afrika, Askofu huyo alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kumshitaki yeye wa hata mmoja wa waumini wake
Desemba mwaka jana, video ya YouTube ilionyesha Askofu Oyedepo viciously akimchapa makofi msichana ambaye alikiri kwamba alikuwa "mchawi " wakati wa ibada alipokuwa amepiga magoti mbele ya madhabahu ya kanisa hilo. Video ya pili ilionyesha Askofu kuhalalisha hatua yake na kuongeza kwamba huduma yake ni "huduma ya kofi" na kwamba "kama atapatikana mchawi yeyote atalazimika kumcha makofi mchawi huyo.
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni