Jumamosi, 15 Julai 2017

SOMO : UZAZI WA MPANGILIO


MALENGO
1.      Utangulizi
2.      Jinsi ya kupata ujauzito
3.      Jinsi ya kuzuia mimba
4.      Kuhesabu Kalenda
5.      Lini tuanze tendo la ndoa baada ya kujifungua
6.      Faida za uzazi wa mpangilio
7.      Uzazi unapochelewa


Utangulizi
MWZ 1:27A zaeni mwongezeke mkaijaze nchi.
Uzazi wa mpangilio (child spacing): ni sehemu ya uzazi wa mpango ambapo wanandoa/wenza hupanga ,lini wapate mtoto /watoto wao wa kwanza ,na wapumzike kwa muda gani , ili waweze kupata mtoto/watoto wanaofuata.
Uzazi wa mpango: ni tendo la wanandoa /wenza kupanga   na kuamua wawe na watoto wangapi na ni kwa kipindi gani
Mambo mhimu
         Wanandoa wafanye maamuzi  ni lini wapate watoto na idadi ya watoto wanao wahitaji
         Kama watahitaji kuzuia mimba ,ni vema wakaenda hospitali wakapewa ushauri na  wataalamu
         Uamzi wa kuchelewa kupata watoto ni vema ukazingatia  yafuatayo:
Umri wa mke/mme (Wanawake  wanashauriwa kuzaa mpaka miaka 35,Zaidi ya hapo kunaweza kuwa na athari)
                     Uwezo wa kiuchumi
                     Fursa za kielimu zilizopo  mf. Kwenda masomoni n.k.
                     Kama mwanandoa anaugonjwa  sugu mf Kisukari n.k.
 Jinsi ya kupata ujauzito
Ujauzito hupatikana pale mbegu ya mwanaume  iliyo kwenye shahawa ikikutana na yai  la mwanamke  lililoko katika mfuko wa uzazi
Kitaalamu mwanamke yeyote ambaye hajazuia mimba kwa namna yoyote   na  yupo kwenye mahusiano ya kindoa anatakiwa abebe mimba ndani ya mwaka mmoja.

Jinsi ya kuzuia mimba
ziko njia kdhaa za kuzui mimba:
         Njia zote zina faida na maudhi madogomadogo
         Ni vyema tukaambiwa hospitali kuliko kusikiliza maneno ya mtaani
         Tusitumie njia yoyote ya kuzui mimba bila ushauri wa kitaalamu
         Siyo kila njia itamfaa mtu ,kila mtu ana njia yake kulingana na mwili wake
Njia mbalimbali zinatumika kuzuia mimba ambazo ni njia za kisasa na asili:

Njia za kisasa
         Njia za muda  mfupi: mfano sindano,vidonge na mpira wa kiume na wa kike (condom)
         Njia za muda  mrefu:   mfano kipandikizi,kitanzi
         Njia za  kudumu : kufunga mirija ya uzazi kwa wanaume na wanawake.
         Njia za asili ni kama vile:
           kunyonyesha ndani ya miezi 6 endapo mama ananyonyesha muda wote,hajaanza kuona siku zake,
         kufahamu siku za hatari (i.e fertility awereness),
         kutumia kalenda ,
         kumwaga mbegu nje kwa wanaume
NB- Kwa upande wa ndoa changa ni vema kuzuia mimba kwa kuhesabu kalenda (safe days).Kwa sababu haitakuwa inaingilia  mfumo wa mwili  na vichocheo  (hormones) wakati wa siku za hatari tumieni condom.

Kuhesabu Kalenda
         Mwanamke hupata hedhi kila mwezi
         Mzunguko unaweza kuwa mrefu zaidi ya siku 35, mfupi siku  21 na mzunguko wa kawaida siku 28-35.
         Siku salama ni siku zisizokuwa na uzazi
         Siku hatari ni siku zenye uzazi
         Yai hupevuka siku 14 kabla ya kuona hedhi yako (Ovulation)
Mfano kama mzunguko wako  ni siku 21 yai litapevuka siku ya 7, na kama ni siku 35 itakuwa ni siku ya21 nk.
Ili kutumia njia hii mama ni lazima awe na mzunguko wa kueleweka (regular cycle) na ajue mzunguko una siku ngapi.
Siku zisizokuwa na uzazi zitakuwa siku tatu baada na kabla ya yai kutoka katika hedhi


Dalili za kupevuka kwa yai (Ovulation)
         Joto la mwili hupanda kidogo siyo homa (0.5-1)
         Kuongezeka hamu ya tendo la ndoa
         Maumivu ya tumbo chini ya kitovu kwa upande mmoja yaani kushoto au kulia.
         Matiti kuuma kidogo
         Ute huwa mwingi ukeni kama  ute mweupe wa yai,na huvutika sana.

Lini tuanze tendo la ndoa baada ya kujifungua
         Baada ya  kila uzazi  mwanamke hutokwa na damu/uchafu (lochia) ambayo kwa wengine huchukua hadi wiki sita
         Kwa wanawake wanaojifungua kawaida ,baada ya wiki sita wanakuwa tayari wamepona.
         Kwa wanawake wanaojifungua kwa upasuaji,kidonda kinapona ndani ya wiki sita na maumivu ya tumbo yanakuwa yameisha, hivyo wanaweza kuanza tendo la ndoa . Kama tumbo linauma unashauriwa kwenda hospitali kutibiwa
Mwanamke yeyote ambaye ananyonyesha kidogo au hanyonyeshi  anaweza kupata ujauzito kuanzia wiki 4-6 baada ya kujifungua.
         Unashauriwa kuwaona wataalamu kabla ya kuanza tendo la ndoa.
         Shauriana na mwenzi wako ni lini mnataka kupata mtoto mwingine, kabla hamjaenda kwa mtaalam.
         Ni vizuri wote mke na mme mkaenda pamoja kupata ushauri.

UMUHIMU WA UZAZI WA MPANGO
         Uzazi wa mpango hupunguza vifo vya mama na mtoto
         Hupunguza mimba zisizotarajiwa
         Husaidia watoto kuwa na afya njema
         Husaidia wazazi kujiandaa na kujiweka sawa kiuchumi

Muda mzuri wa kupata ujauzito
          Kati ya miaka 18-34
         Angalau miaka miwili (2)baada ya kujifungua
         Angalau miezi  sita(6 ) baada ya kuharibika kwa ujauzito

Faida za Uzazi wa mpangilio
Uzazi wa mpango una faida kubwa kwa mama na mtoto kama vile:
          Kupata watoto wenye afya nzuri na waliofikisha umri wa kuzaliwa.
         Kupunguza vifo vya watoto wachanga
         Afya ya mama kuimarika
         Kipato cha familia kuimalika.

Madhara yatokanayo na mama kupata ujauzito wa mara kwa mara
         Kupata mtoto mwenye uzito mdogo
         Kuzaa mtoto njiti
         Vifo vya watoto wachanga.
         Kupasuka kizazi wakati wa kujifungua na pengine kupeleke kifa kwa mama

Uzazi unapochelewa
         Hiki ni kipindindi ambacho mwanamke anashindwa kupata ujauzito  baada ya mwaka mmoja ,akiwa anaishi na mwenzi wake ,muda wote na hajatumia njia yoyote ya uzazi wa mpango
         Baada ya mwaka mmoja wanashauriwa wote wawili mke na mume ,kwenda hospital kupima,
         Mume anatangulia kupima mbegu zake,akionekana hana tatizo,mke naye hupimma (vipimo vya mwanamke vinauma sana),lazima tuwe na uhakika kuwa mme yuko vizuri.

Katika swala zima la ugumba wanaume huchangia 40%,wanawake 40% na 20% ni kwa wanandoa wote.
Angalizo -Ni lazima mme akapime
          -Ni vema kwenda hospitali badala ya kwenda kwenye tiba mbadala
          -Kama wanandoa hawaishi pamoja wanahitajikukutana wakati wa siku za hatari.

                                               HITIMISHO
-         Watoto kwetu ni zawadi bali ni urith kwa Bwana
-         Sala na Hana walipitia katika jaribu hili lakini walishinda, hilo ni jaribu lako kuna mlango wa kutokea.
-         Kanisa tuwe washauri wazuri na kama tumeshiriki katika kunena vibaya tutubu.


MUNGU AWABARIKI

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe cha kusimama peke yangu bila mwili wa kusimama na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na Dk DAWN, baada ya kumwambia. kuhusu hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kiukweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi huku akiniomba kuwa hatoniacha kamwe. tena. Miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
* upendo
inaelezea * inaelezea kivutio
* kama unataka ex wako nyuma
*acha talaka
* kuvunja obsessions
* huponya viharusi na magonjwa yote
* uchawi wa kinga
*Ugumba na matatizo ya ujauzito
* bahati nasibu
* uchawi wa bahati
Wasiliana na Dk Ediomo kwenye barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp:+2349046229159