Jumanne, 21 Februari 2017

KANISA LIMEITELEKEZA ISRAEL?


 
Shalom mpendwa. Awali ya yote kabla hujaanza kusoma mafundisho haya, ninakushauri uchukuwe notebook, kalamu, Biblia na tafuta mazingira matulivu kabisa alafu utangulie kufanya maombi kualika Roho Mtakatifu akusaidie kuelewa ujumbe wa somo. Baada ya kufanya hayo sasa endelea.
Yakiwa ni majira haya ya mwisho wa mwaka Wakristo wengi toka pande mbalimbali za dunia hii kwenda hija Israel kama sehemu ya ibada zao takatifu ya Mungu, leo ninawiwa kukuletea mafundisho yenye kichwa “Kanisa limeitelekeza Israel?” Uchunguzi nilioufanya kupitia sampuli ya uchunguzi (sample population) ya waumini katika Kanisa ninaloabudia kwa njia ya kuwahoji baadhi yao katika makundi mbalimbali ya kihuduma, rika na jinsia mfano Wanakwaya, shule ya Jumapili, Wazee wa Kanisa, Wanamaombi, waumini wasiojiunga na vikundi; umebaini kuwa Wakristo wengi wana ufahamu mdogo sana kuhusu uhusiano wa Israel na Mkristo.
Wengi wanachojuwa tu ni kuwa imani ya Ukristo ilikuja duniani kupitia Israel na zaidi kwamba Israel lilikuwa taifa teule la Mungu hivyo tu basi. Nikiri kuwa sikuwahoji Wapakwa mafuta, sababu za kufanya hivyo ni kuwa baadhi yao walikuwa likizo, wengine wakikosa muda kutokana na kutingwa na kazi za huduma kama semina ya Neno la Mungu iliyokuwa ikiendelea Kanisani kwa majuma mawili mfululizo.
Sampuli ya maswali niliyotumia niliyaandaa kwenye shajara/diary (ili kuepuka gharama za kuandaa vitine vya maswali questionnaires, hivyo maswali yote niliyauliza kwa mdomo (orally)) kwa kuzingatia makundi ya rika mfano kwa watu wazima nilitumia maswali-mfungo (closed-ended questions), kwa wanafunzi wa shule ya Jumapili nilitumia maswali ya kuchagua (multiple choice questions). Aidha katika uchunguzi wangu nilitumia mbinu ya kawaida (Random Survey).
Maswali ya msingi yalikuwa kama ifuatavyo: Maswali-mfungo (closed-ended questions): 1) Elezea ufahamu wako kuhusu Israel. 2) Uhusiano wa Mkristo na Israel ukoje? 3) Israel ipi ni taifa teule la Mungu ambalo baraka zetu zimefunganishwa nalo? 4) Umewahi kufundishwa, kuhubiriwa au kushuhudiwa madhabahuni Kanisani kuhusu uhusiano wa Mkristo na Israel? 5) Taja dini kuu zilizopo duniani? 6) Unaijuwaje Freemasonry?
Maswali ya kuchagua (multiple choice questions) kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya Jumapili yalikuwa kama ifuatavyo:
1. Injili ilikuja wakati gani?
a) Wakati wa agano la kale.
b) Wakati wa agano jipya.
c) Yote a na b ni majibu sahihi.
 
2. Baba wa Injili ni nani?
a) Musa.
b) Yesu.
c) Paulo Mtume, Yohana, Luka, Marko na Mathayo.
 
3. Umejifunza shuleni kuwa Umoja wa Mataifa ulianzishwa kwa lengo gani kubwa?
a) Kusimamia amani ya dunia.
b) Kusimika nchi.
c) Kutoa misaada ya kibinadamu na maendeleo.
 
4. Biblia inasema Mkristo atabarikiwa na Mungu ikiwa atambariki nani?
a) Palestina.
b) Israel.
c) Yote a na b siyo sahihi.
 
Maswali yasiyo ya msingi yalihusu wasifu wa mtoa majibu (Personal Profile) mfano: Jina, umri, ubatizo, kupata au kutopata ubarikio/kipaimara, kushiriki meza ya Bwana, ndoa, kiwango cha elimu ya dunia nk.
Majibu ya jumla ya uchunguzi huu ndiyo kama nilivyosisitiza kwenye aya za awali za mafundisho haya hapo juu kuwa Kanisa limetindikiwa kwa kiwango kikubwa sana cha maarifa kuhusu mahusiano ya Mkristo/Ukristo na Israel. Na huenda hata kwenye kada ya Wapakwa mafuta wa Bwana kama uchunguzi ukifanyika baadhi yao wanaweza kugundulika kuhitaji kuboreshewa kiwango chao cha maarifa kuhusu mahusiano ya Mkristo/Ukristo na Israel. Hii ni muhimu kufanyika hima kwa sababu wao ndiyo wamekasimiwa jukumu la msingi sana la kuliandaa Kanisa kwa ajili ya unyakuo wake katika siku ambazo huenda haziko mbali sana na nyakati tulizonazo sasa. Kusema hakuna ajuaye majira wala saa inatupa tahadhari kwamba tukio linaweza kutukia karibuni au hata baadaye huko, hivyo ni muhimu kuliweka Kanisa tayari.
Kuanzia tarehe 18 Januari, 2015 katika toleo namba 00117 la gazeti hili, niliandika makala ndefu ya mafundisho yenye mfululizo kwenye matoleo yake mengine yaliyofuata; yenye kichwa “Mgogoro wa Israel na Palestina, Israel alipewa Yakobo siyo Yakubu” lakini kwa kuwa elimu ni bahari/haina mwisho nimeona nilete mafundisho haya juu ya uhusiano wa Israel na Mkristo/Ukristo na hasa nikiweka msisitizo juu ya kwa nini uhusiano huu haufundishwi Makanisani lakini pia nikibainisha mambo ambayo yamefichama ambayo hata hao wachache walioshukiwa na Roho wa Mungu kufundisha somo hili hawayaweki wazi.
Hii inashuhudia ukweli kwamba uhusiano wa Mkristo na Israel haufundishwi wala kuhubiriwa kwenye madhabahu nyingi za Kanisani labda madhabahu chache sana za vyombo vya habari. Mimi mwenyewe ninakiri kuwa toka tumboni mwa mama yangu sijawahi kusikia habari hii iliyoandikwa kwenye Biblia ikihubiriwa au ikifundishwa kwenye madhabahu za Kanisa langu na mengine niliyowahi kuabudu siku za Bwana. Sababu ya Wapakwa mafuta ama kutofundisha au kutohubiri kuhusu uhusiano huu muhimu ambao ni tunu na dira ya imani ya Ukristo hazijulikani.
Labda baadhi wanaweza kujitetea kwamba wanafuata liturjia ambazo masomo yanayohusu agenda hii hayakuingizwa kwenye vitabu hivyo ambavyo ndiyo mwongozo wa ibada kwa Makanisa mengi. Kama sababu ya kutofundisha somo hilo zinatokana na hofu ya kufanya uchochezi na kuchukuwa upande kwenye mgogoro wa Israel na Palestina basi Wapakwa mafuta hawaitendei haki imani na Injili na wakumbuke kwamba hiyo siyo salama yao kwa sababu sote tunajuwa Mungu aliwafanyaje Makuhani waliotumika kwa mikono milegevu.
Nimejaribu kufuatilia kwa miaka mingi madhabahu za vyombo vya habari vinavyofundisha somo kuhusu uhusiano wa Mkristo na Israel nikakuta ni WAPO Radio FM kupitia kipindi chake cha “Ijuwe Israel” kinachorushwa na Mwisraeli namba moja Elibariki Minja (Mkurugenzi wa vyombo vya habari vya WAPO Mission) ambaye anafuatilia na kuripoti matukio yanayovuta hisia za dunia yanayoihusu Israel. Askofu Mkuu Sylvester Gamanywa wa huduma ya BCIC chini ya WAPO Mission amekuwa akifundisha juu ya uhusiano huu kwa takriban miaka miwili mfululizo.
Mwl. Christopher Mwakasege wa huduma ya MANA amekuwa naye akifundisha kwa muda mrefu pia kuhusu somo hili la uhusiano wa Mkristo na Israel kwenye semina zake, wavuti ya MANA, machapisho yake na kwenye gazeti la Upendo linalomilikiwa na KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani.
Mch. Christosila Kalata wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Jimbo la Kati naye hakukaa kimya kwa kupiga kelele kwenye madhabahu ya Bwana ya gazeti la Upendo akifundisha kuhusu uhusiano wa Mkristo na Israel. Halikadhalika Mtumishi wa Mungu Mch. Himili Kimweri (Bwana ameishampandisha cheo kwenda kwenye utukufu) aliyehudumu katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani Jimbo la Kati pia alijihudhurisha kwenye madhabahu ya Bwana ya gazeti la Upendo akifundisha kwa marefu, mapana, kimo na kina kuhusu somo hili na ninahisi ameitika mwito wa Bwana wa umilele huku maandikao yake mengi yakingali hayajalifikia Kanisa.
Askofu Mkuu wa EAGT (Baba wa Uamsho wa Kanisa la Tanzania) Mch. Moses Kulola naye kama Mch. Himili Kimweri; Baba wa Mbinguni ameishampandisha cheo kwenda kwenye utukufu baada ya kumaliza kazi iliyotukuka, yumkini ndiye wa kwanza kwa Kanisa la Tanzania kupiga mbiu ya mafundisho ya uhusiano wa Mkristo na Israel, kwa maisha yake yote ya huduma hakuacha kwenda kuhiji Israel. Inaaminika ndiye Mtumishi wa kwanza kuhamasisha Kanisa la Tanzania kwenda kuhiji Israel baada ya mahusiano ya kibalozi kati ya Tanzania na Israel kukoma na akaendelea kufanya hivyo hata baada ya mahusiano hayo kurejeshwa.
Muhtasari wa mtazamo wa kidini na kisekula kuhusu asili ya Israel kama taifa.
Kanisa la leo kushindwa kuhimiza mafundisho juu ya uhusiano wa Mkristo na Israel ni jambo la kufisha imani ikizingatiwa kwamba baraka na laana za Mkristo zimeunganishwa na Israel “Mwa.12:3 Nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.” Kutokuujuwa vizuri uhusiano wako kama Mkristo na Israel hakika ni shina lizaalo uchungu na pakanga Kumb.29:18; kwa sababu hali hiyo yaweza kukupeleka kuiabudu mingu na kufanyika ibada kamili ya sanamu.
 
Ufundishaji wa somo linalohusu uhusiano wa Ukristo na Israel ni muhimu sana nyakati hizi tulizonazo kiasi kwamba ninatoa changamoto kuwa matoleo mapya ya liturjia yanapaswa kuhimiza ufundishaji wa masomo kuhusu umuhimu wa Israel kwa Mkristo na Ukristo (KKKT liturjia yake bado inaendelea kufanyiwa uhariri kabla ya kuitoa kwa ukamilifu wake, ninawashauri wajumbe wa kamati ya maandalizi ya liturjia hiyo kuzingatia umuhimu wa kuingiza masomo yanayohusu agenda hii ya mahusiano ya Kanisa/Mkristo na Israel ambayo ni tunu ya umilele ili Kanisa lipone na liendelee kufanya maandalizi mazuri ya unyakuo wake ambao hauko mbali na majira haya).
Hivi leo Wakristo wengi wanajiaminisha kuwa wanabarikiwa kwa kuwa na uhusiano na Israel lakini ukimuuliza kwa vipi? Hawezi kukufafanulia. Aidha hawajui vikwazo/utata uliopo kwenye uhusiano huo; ambavyo vinafanyika makwazo ya imani na kizuizi cha baraka tulizoahidiwa na Baba wa Mbingu na nchi; utata ambao wangeutumia kama agenda ya maombi kuombea Israel.
Wengi wamenunua machapisho kuhusu uhusiano wa Mkristo na Israel lakini ni wachache sana wanayasoma. Wengi pia wananunua bidhaa za kutoka Israel kama alama ya ukumbusho souvenir lakini undani wake sana hawajui. Lakini wapo pia ambao wanafuatilia mafundisho kupitia madhabahu za vyombo vya habari lakini hawaelewi kwa kiwango cha kutosha kuwasaidia. Sababu za kutokuelewa au kutokufuatilia mafundisho hayo yenye mafunuo ndani yake kuhusu uhusiano wa Mkristo na Israel; zinatofautiana toka kundi moja hadi lingine kama ifuatavyo:- Wapo ambao kwa asili ni wavivu wa kusoma, lakini wapo ambao wakisoma hawaelewi hadi awe na Mwalimu wa kumfafanulia.
Pia wapo ambao wananunua machapisho hayo kwenye semina kwa ushindani na kujionyesha tu mbele ya watu kuwa ni wasomaji lakini wakiishaingia kwenye magari yao ya kifahari ndiyo mwisho wao na machapisho hayo, baada ya siku mbili ukiwauliza yalipo watakushangaa kweli kweli au hata baada ya mwezi ukiwauliza wakusimulie japo sura moja tu ya chapisho mojawapo hawatakumbuka kama waliwahi kununua kitu kama hicho. Wakati fulani unakuta wasiosoma ndiyo wanapigana vikumbo kupata machapisho hayo na wale wenye muda, nia na utamaduni wa kusoma ndiyo wanakosa machapisho kwa kigezo kwamba vimeisha.
Siku moja nilimuuliza tabibu mmoja mwenye shahada ya uzamili ambaye alikuwa mfanyakazi mwenzangu na ambaye tumehudhuria naye semina za MANA; kuhusu kama anafuatilia machapisho ya MANA akasema “nimeyanunua kibao” (akimaanisha ameyanunua mengi) lakini hajasoma hata msitari mmoja, akasema yeye anapenda tu Compact Diskette (CD) ili awe anasikiliza kwenye gari yake, nikamhoji kwa mshangao mkubwa sana nikizingatia ni mtu muelewa, akajibu kwamba hana muda wa kusoma, tangu amemaliza chuo hakumbuki kama amewahi kununua kitabu akasoma japo mwanzo hata katikati tu achilia kukimaliza chote, kwa sababu hana muda.
Nikaugulia rohoni pale nilipogundua kuwa kwa maana hiyo basi kumbe hata Biblia kuna watu ambao hawasomi, japo wanazibeba na kwenda nazo ibadani, japo wanazo kwenye ipad na smart phone zao, nikasikitika na kujisemesha moyoni kuwa Makanisa ya Efeso na Korintho yanarejea kwa kasi kubwa ama kumbe yangalipo nasi hata baada ya kazi ngumu za hatari ya kuondoa uhai walizofanya Mitume kama akina Petro (alisulubishwa kichwa chini), Paulo (alihukumiwa kunyongwa Urumi), Stephano (alipigwa mawe hadi mauti kwa amri ya Mfalme Sauli), Bartholomeo (alichunwa ngozi yote akiwa hai na kufa baadaye) na wengineo? Ninaamini Kanisa la Tanzania linafanya huduma katikati ya jamii ambayo utamaduni wa kusoma haupo asilani. Jamii ambayo imefarakana na Injili ya Mt.28:19-20.
Watu wanawaachia walimu na wachungaji/wahubiri wafanye rejea wenyewe huko alafu waje darasani/madhabahuni wawalishe kwa kijiko tu, kumfundisha mwanafunzi asiye na tabia ya kujisomea ni hatari kubwa. Fasihi andishi (kusoma machapisho) inatokomea kwenye jamii hii na fasihi simulizi (kusikiliza CD, Radio, TV, Cassette, maigizo, ngonjera, mashairi na majigambo) ndiyo inatamalaki soko, na hii ndiyo maana leo katika nchi yetu waandishi wa vitabu hawana ukwasi kama wasanii wa muziki na maigizo. Ninaamini waandishi wa Neno la Mungu ni mashahidi kuwa CD zao zinauzika zaidi ya vitabu na vitine vyao. Lakini Watanzania wanasahau umuhimu wa fasihi andishi ambayo ndiyo fasihi mama kwa sababu huwezi kutengeneza CD bila kuandika script kwanza, na kuandika script ni fasihi andishi hiyo. Mungu tusaidie! Turejee kwenye mada yetu ya Israel.
Kuna semina moja aliwahi kufundisha Mwl. Mwakasege akitoa tahadhari kwa Wakristo kwamba wasiende Israel kwenye hija kama watalii la hasha, bali kama Wanamaombi, kwa maana taifa lile liko kwenye mgogoro/vita hivyo pasina kujipanga kwa maombi ya nguvu, unaweza kujikuta ukirudi na roho wa machafuko/magomvi/vita kwenye familia yako, ukoo wako, huduma yako au Kanisa lako badala ya baraka.
Haya yote yanatokana na ukweli kwamba walio wengi hawaijui Israel vizuri licha ya kwamba wana Biblia nyingi majumbani, kwenye magari, kwenye simu zao na maofisini pia. Aidha wengi hawa hawafuatilii taarifa za vyombo vya habari zikiwemo mitandao jamii (blogs na wavuti mbalimbali) kuhusu yanayotukia Israel. Pia wapo ambao wanafuatilia lakini hawaelewi ufasaha wa utaifa wa Israel (mgogoro wake na hata ahadi za Mungu kwao) na mahusiano yake na wao kama Wakristo. Aidha wapo ambao wamepewa elimu potofu kuhusu Israel, wote hawa wanahitaji msaada na Kanisa likikaa kimya lazima litadaiwa.
Kuna mgongano wa uelewa kuhusu Israel; ambao nao huu ni wachache sana ndani ya Kanisa la leo wanaufahamu/wanaufuatilia. Kuna kundi ambalo linajumuisha Wakristo na wasio Wakristo linaloamini kuwa Israel hii ya leo tuijuayo na tunayokwenda kuhiji kwayo ili kupata baraka tulizoahidiwa kwenye Mwa.12:3 siyo Israel aliyochagua Mungu kama taifa teule nyakati za Biblia. Wao wanaamini Israel ile aliyoteua Mungu nyakati za Biblia kamwe haipo tena na kwamba iliondoka na enzi hiyo ambayo haipo tena leo na ambayo hatuwezi kuirejesha kamwe.  
Kundi hili linashikilia kwamba Israel hii ya leo siyo ya Mungu (siyo aliyomaanisha Mungu) bali imeasisiwa kimafiamafia na kundi la Illuminati linalojaribu kubadili mfumo wa ibada toka ule uliozoeleka wa nuru na uliopo kwenye vitabu vitakatifu kwenda ule wa giza kwa msaada wa wakala wao Umoja wa Mataifa. Kundi hili linadai kuwa illuminati wana shirika-dada linaloitwa Freemasonry ambalo kwa ushirika huo wamebeba agenda kuu ya kupandikiza mfumo mpya wa dunia (The New World Order) wakitaka kuwepo na mfumo mmoja unaoshabihiana katika masuala yote ya uendeshaji wa mfumo wa maisha ya mwanadamu duniani kuanzia imani, siasa, uchumi, jamii, ulinzi, utamaduni nk.
Wakristo hawa (ambao siyo wana Illuminati yaani wanapinga uwepo wa illuminati na wanapinga pia Israel hii; ilhali ni waumini safi wa imani ya Ukristo) wanashikilia kuwa illuminati imebeba ndani yake wanachama toka katika dini zote kubwa duniani, wanasiasa maarufu duniani wakiwamo baadhi ya wakuu wa nchi, matajiri, walozi, baadhi ya viongozi wa dini walio maarufu na wasio maarufu, wanazuoni waliobobea kwenye fani mbalimbali zinazoendesha maisha duniani; wanadai kuwa Israel hii imeundwa mwaka 1948 na Umoja wa Mataifa hivyo imekuja nyuma ya Israel ile aliyochagua Mungu kama taifa teule.
Wanaikataa katakata na kuikana kabisa Israel ya akina Chaim Weizmann (Mzayoni aliyekuja kuwa rais wa kwanza wa Israel), David Ben-Gurio (Myahudi wa kwanza kuwa Waziri Mkuu wa Israel), akina Yitzhak Rabin, Ariel Sharon, Shimon Perez, Benjamin Netanyahu nk badala yake wanaitambua Israel ya akina Wafalme Daudi, Sauli na waliofuata, wanaitaka Israel ya akina Ibrahimu na Yakobo ambayo wanaamini imetoweka. Sababu yao kubwa ni kuwa Israel hii ya leo imetengenezwa na Illuminati waabudu giza, wanasahau kuwa hata Israel ile wanayoitaka ya nyakati za Biblia nayo kabla ya kuteuliwa na Mungu kama taifa lake liliabudu kama Illuminati pia (kabla ya Ukristo imani iliyokuwepo duniani ilikuwa ni ile ya giza miaka takriban milioni 500 – 400, Ukristo ulishushwa toka Mbinguni ambako ndiyo asili yake). Kabla ya agano jipya hapakuwa na Yesu Kristo, Mungu alijidhihirisha moja kwa moja kwa wanadamu. Biblia inasema hapo mwanzo kabla Mungu hajaiumba dunia, palikuwa na utupu na giza, umewahi kujiuliza kulikuwa na imani gani hapo? Ya nuru au ya giza? Kulikuwa na dini gani hapo? Ya Mungu au ya Freemasonists?
Ibrahimu baba wa imani na rafiki mkubwa wa Mungu, baba yake aliyeitwa mzee Tera biashara yake ya kumpa riziki ilikuwa ni kutengeneza miungu ya kufinyanga udongo na kuchonga mipingo (ambayo hii ni Illuminati na Freemasonism pia kwa sababu ni ibada ya sanamu/giza) na la kushangaza zaidi ni pale ambapo Ibrahimu mwenyewe kwa mikono yake na kinywa chake ndiye alikuwa akiwauzia watu miungu hii gulioni hata pale alipotambua kwamba anamghadhabisha Mungu na kuamua kuachana na biashara hiyo, uamuzi ambao ulimgharimu viboko toka kwa baba yake na mahusiano yao kuingia dosari pale Ibrahimu alipomhoji baba yake kwa maswali ya mtego ya kumfunga baba yake kuhusu miungu hii ambayo alipoiteketeza kwa moto wa nyika na kurudi kwenye boma la babake na kupoteza kabisa mtaji wa biashara na pale ambapo alimjibu babake kuwa miungu imeruka kwenye tenga na kutokomea na babake kumhoji ni kwa vipi miungu hii isiyokuwa na uhai ikimbie?
Hapa ndipo Ibrahimu akapata fursa nzuri ya kumbana kwa hoja nzito kuwa kumbe wewe unadanganya watu waabudu sanamu badala ya Mungu wa kweli? Kumbe hata wewe unajuwa kuwa miungu hii siyo Mungu? Na kwamba ni mfu?! Kitendo hiki cha kijasiri na cha kujitoa muhanga kiliimarisha uhusiano mkubwa sana baina ya Ibrahimu na Mungu. Ukristo wa matokeo mazuri makubwa ni ule wa kuwa tayari kujitoa muhanga kwa imani ya Ukristo.
Kundi hili linaloikataa Israel ya leo kuwa siyo ile aliyomaanisha Mungu, pia linasahau kwamba hata Israel hiyo ya nyakati za Biblia wanayoitambua nayo walikuwemo watu wenye ibada kama ya Illuminati na Freemasonry mfano wao: Herode Mkuu Mt.2; Lk.1:5, Herode Agripa Mdo.12, Herode Antipasi Mt.14; Mk.6; Lk.9, Nebukadreza 2Fal.24-25; Dan.1-4, Mabaali, Maashtorethi na Dagoni Amu.16:23, Pontio Pilato aliyekuwa Liwali wa Yuda aliyevunja rekodi kwa kunyonga watu Mt.27; Mk.15; Lk.31:1; 23; Yn.18-19, Potifa na mkewe Mwa.39, Kayafa Kuhani Mkuu aliyewashauri Wayahudi kuwa ni afadhali mtu mmoja (Yesu) afe kwa ajili ya ufalme Yn.18:14 ndiye aliyeongoza baraza lililomhukumu Yesu. Wengine ni Mfalme Belteshaza Dan.5, Farao wa 40 katika safu ya Mafaro waliowahi kuitamalaki Misri; aliyetumikisha utumwani wana wa Israel wa kabila la Ebrania, Goliathi 1Sam.17, Balaki na Balaam wake walioilaani Israeli Hes.22:5-24; 25, Kadhi dhalimu aliyetoa haki kwa mwanamke mjane aliyemghasi Lk.18:2-6, Simoni mchawi, Kornelio aliyekuwa mtoaji pasina kumuamini Yesu (hakuokoka wala hakubatizwa hivyo siyo mfuasi wa Yesu na imani ya Ukristo, walikuwepo Anania na Safira waliokumbatia ufisadi Mdo.5:1-10), mfalme Dario. Ndiyo maana Biblia inasema mambo ya kale ni kivuli cha mambo ya leo (agano jipya).
Lakini pia hata Israel hiyo ya nyakati za Biblia nayo pia kama leo tunavyohofu masonists; ilihofu dola la Kirumi kupandikiza mfumo mpya wa dunia (new world order) katika dunia hiyo ya zama hizo ukiwemo mfumo wa ki-ibada ukiratibiwa na mfalme Agusto mwanzilishi wa dola la Kirumi aliyezaliwa mwaka wa 63 KK Roma, Italy na kufariki mwezi Agosti tarehe 19 mwaka wa 14 BK huko Nola, Italia. Tunakumbuka hata Yesu alilazimika kupelekwa mafichoni Misri kuhofu mfumo wa utawala uliokuwepo ambao ulikuwa ukipingana na imani ya Kiyahudi na Kikristo.
Kundi hili linalokataa Israel ya leo linasahau kwamba Kol.2:17 ilitoa unabii kuwa “mambo hayo (ya agano la kale) ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo” (hapa Paulo Mtume anawaandikia waraka Wakristo wa Kolosai juu ya miiko na mifumo ya ibada). Hivyo basi Israel ya leo ni kivuli cha Israel ya nyakati za Biblia na kwamba kwenye Kolosai.2:17 amesema kwamba “mwili ni wa Kristo” hapa anasisitiza juu ya umoja katika kumuamini Kristo pasina kuwa na miiko, mipaka na mapokeo. Mungu hakukosea alipoifananisha Mbingu na Yerusalemu mpya.
Mpya maana yake siyo kale/zamani. Yerusalemu mpya inaashiria kuwa kuna Yerusalemu ya zamani (Yerusalemu iko Israel). Yumkini hiyo mpya ndiyo bado inaishi hata leo, kwa mantiki hiyo ya hoja, yawezekana Mungu alichagua mpya badala ya ile ya zamani (ingawa sijajuwa kwa nini aliachana na ile ya zamani), na kwa hiyo Israel mpya Mungu ameuunganisha/ameufananisha na Mbingu/Yerusalemu mpya. Kundi hili linaloikataa Israel ya leo wajipime kwenye ujenzi huu wa hoja wajione wako kwenye Yerusalemu/Israel ya zamani/kale au mpya/ya sasa ambayo ndiyo Mungu ameamua kuzibatiza Mbingu kwa kutumia mfano na jina lake (Yerusalemu mpya).
Aidha kundi hili lijiridhishe pasina shaka kuwa Yesu atakaporudi (ambayo hii wanaamini pasina kigugumizi) atarudi Somalia?, Washington DC? au Israel? (Ingawa kila jicho litamwona pande zote za dunia), na kama atarudi Israel (Yerusalemu tena mpya siyo ya zamani/kale) je, wamejipanga kumkana, kumzuia kuwa asirudi kupitia Yerusalemu kwa maana hii Israel ya leo ni ya Freemasonry, siyo ile aliyoacha wakati anapaa. Natamani hili kundi linaloikana Israel (wao wanasema ya Freemasonry) lingerudishwa kundini japokuwa ni Wakristo walioamini na kubatizwa na wanaomkiri Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao.
Kumbe hata ndani ya Kanisa la leo bado kuna mikondo mingi ya imani kiasi hiki licha ya kuwa tunasoma Biblia moja, Mchungaji mmoja, madhabahu moja, tunakiri imani ya mitume na nikea moja nk. Hapana jamani! Ebu Kanisa chukua hatua kutoa mafundisho sahihi yaliyotelekezwa ya uhusiano wa Israel na Ukristo ili roho zetu zipone kabla Mwana wa Adam hajashuka mawinguni kuja kukunyakua. Misikiti imeendelea kufundisha kwa bidii juu ya kuitetea Palestina wakati huo Makanisa yakionea aibu kufundisha juu ya uhusiano wa Israel na Mkristo, sijui ni kwa sababu ndani ya Illuminati na Freemasonry inadhaniwa wamo baadhi ya viongozi wakubwa wa dini hivyo wanafanyika mawakala wa Illuminati na Freemasonry wa kuzuia elimu sahihi juu ya uhusiano wa Ukristo na Israel isifundishwe Kanisani?
Cha ajabu ni kuwa hata viongozi wa Uislamu nao baadhi yao wanadhaniwa kuwa wafuasi wa Illuminati na Freemasonry lakini bado wameweka msisitizo juu ya kuitetea Palestina dhidi ya Israel, je, ni unafiki wa viongozi wa Ukristo au ni nini? Nasema unafiki kwa sababu kama baadhi yao wanadhaniwa kuwamo kwenye Ufreemason na pia wamo Makanisani basi huu ni unafiki kutumikia nuru na giza kwa wakati mmoja. Mpango wa Freemasonry kuunganisha dunia kuwa kijiji kimoja chenye mfumo mmoja wa maisha unafanikiwa kwa kasi na tayari dalili zinaonekana ikiwemo ile ya hivi karibuni iliyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa mamlaka ya Vatikani tayari imefanyia marekebisho Amri Kumi za Mungu (kumbuka Vatikani iko Roma ambayo ndiyo ilianzishwa na Mfalme Agusto aliyeipinga Israel na aliyeitawala dunia kupitia dola la Kirumi) na ripoti hiyo hadi sasa haijakanushwa wala kukubaliwa na mamlaka ya Vatikani ambayo ina balozi zake sehemu kubwa ya dunia hii.
Mojawapo ya kazi za balozi ni kufafanua na kuweka sawa misimamo ya nchi/mamlaka yake. Umoja wa Mataifa nayo ambayo inadhaniwa ni chombo kilichopandikizwa na Illuminati tayari kupitia shirika lake la UNESCO linaloshughulikia elimu, sayansi na utamaduni, limeitambua Palestina kama taifa huru hata kabla ufumbuzi wa maeneo yanayogombewa ya Yerusalemu, ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa mto Yordani haujapatikana na hivi karibuni limeripotiwa na vyombo vya habari kuweka kwenye milki ya Palestina hekalu lililojengwa na Mfalme Sulemani. Nikirejea kwenye siasa, naona kuna utata baina ya UNESCO na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia migogoro duniani. UNESCO na Baraza la Usalama ni vyombo vya Umoja wa Mataifa. Wakati UNESCO inatambua utaifa wa Palestina, Baraza la Usalama lenyewe limeendelea kushikilia azimio lake namba 242 ambalo linakinzana na uamuzi huu wa UNESCO.
Azimio namba 242 la baraza la usalama la UN, pia ni azimio tata kwa sababu lilitoa agizo kwa Israel kuachia maeneo iliyoyateka katika vita ya Juni 1967 na kutoa haki kwa dola zote zinazohusika na eneo hilo. Hili ni azimio tata kwa sababu tafsiri yake katika lugha ya Kifaransa inasema Israel inapaswa kuondoka katika maeneo hayo huku tafsiri ya lugha ya Kiingereza ikitoa mwito wa kuondoka kwenye maeneo hayo (“Kupaswa” na “Mwito” ni semi mbili zinazosighishana kwenye maana na mantiki kwa jambo moja. Aidha Kifaransa na Kiingereza zote ni lugha rasmi za UN).
Israel na Marekani zinatumia tafsiri ya Kiingereza kubisha kuwa Israel iondoke kwenye baadhi tu ya maeneo lakini siyo maeneo yote ili kukidhi matakwa ya azimio hilo. Kwa miaka mingi Palestina iliendelea kukataa azimio hilo kwa kuwa halitambui uwepo wa utaifa wake na ikataka wakimbizi kupewa makazi ya haki ambako hawatasumbuliwa lakini zaidi kuwa azimio hilo lililotaka utambuzi wa kila mamlaka/dola katika eneo husika, linatoa mwito kwa Palestina kutambua Israel bila Israel kutambua haki za kitaifa za Palestina.
Waisrael wanaamini Yesu atarudi duniani kupitia Yerusalemu ambayo inagombewa na Palestina na Israel na sehemu yake kubwa inakaliwa na Palestina huku Israel ikilazimika kujenga na kuhamishia makao yake makuu Tel Aviv kuepuka hujuma za kiusalama, lakini kwa angalizo kuwa lazima kabla Yesu hajashuka mawinguni watakuwa wamerudi Yerusalemu kumpokea na wanasisitiza kuwa watarudi ama kwa mabavu au maelewano, ubabe au upole, vita au utangamano na tayari wao wanaendelea na matayarisho ya kumtarajia na kumlaki Bwana Yesu.
Kundi hili linaloikana Israel ya leo, kama Yesu atarudi kupitia Israel hii wanayoikana sijui watamkataa na kuendelea kumsubiri Yesu arudi kupitia Israel ya nyakati za Biblia; ya Daudi na Sauli (wafalme wake wa kwanza)? Muunganiko wa viongozi wa dini wanaodhaniwa kuwa wanachama wa Freemasonry na kundi linaloikana Israel hii na kundi linalounga mkono maadui wa Israel; unaelezea ukweli wa maandiko kwenye Eze.2:6 kuwa miiba na michongoma i pamoja naye (Israel), naye (Israel) anakaa katikati ya nge (maadui na wale wanaomkana).
Aidha lipo kundi linaloamini kuwa Israel hii hata ramani yake imechakachuliwa kimabavu kwa nguvu kubwa za kijeshi na maazimio kandamizi ya kimataifa kwa kupora ardhi ya Palestina na kuipa Israel na wanashikilia kuwa hata ramani ya Biblia za awali zilionyesha eneo ambalo atlas za leo zinaonyesha kuwa ni Israel ya leo; kuwa ndiyo ilikuwa Palestina, wakihoji kuwa ukubwa huu wa Israel ya leo wa 20,770 km2 unatoka wapi wakati walikuwa na eneo dogo tu tangu agano la kale?.
Makundi hayo mawili hapo juu hayakubaliani asilani na Wakristo wa leo wanaochukuliana na Israel ya leo kwenye ibada zao wakidai kuwa kitendo hicho ni uovu dhidi ya Palestina wanayodai inaonewa na ni kuambatana na Israel iliyoghoshiwa/iliyotengenezwa na Illuminati kwa ushirika na Freemasons na Umoja wa Mataifa na kwamba Wakristo hawa kwa kitendo chao hicho cha kuitambua na kuambatana na Israel hii ya leo kwenye imani na ibada zao basi wameungana na Freemasons kubeba agenda yao ya mfumo mpya wa dunia (The New World Order). Jamani?!
Makundi hayo yanayopinga uwepo wa Israel hii ya leo yanatindikiwa maarifa ya kutosha kuhusu chimbuko la Israel kimaandiko. Lakini ili kujuwa kuwa maeneo yanayogombewa (Ukanda wa Gaza, Yerusalemu na Ukingo wa Magharibi wa mto Yordani ambayo yote haya yako kwenye nchi ya ahadi ya Kibiblia ya Kanaani ambayo ndiyo inajumuisha na Israel ya leo, ambapo waliishi watoto wa Kanaani Mwa.10:15-18 ambao ni Sidoni, Hethi, Myebusi, Mwamori, Mgirgashi, Mhivi, Mwarki, Msini, Mwarvadi, Msemari, Mhamathi) na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza Mwa.10:19. Waliishi hapo kuanzia karne ya 15–6 KK. Kwanza ni budi tujuwe Kanaani ni nani?
Mwa.10:1,6 inadhihirisha kuwa Kanaani ni mjukuu wa Nuhu kupitia mtoto wa Nuhu aitwaye Hamu. Hapo pia utagundua siri ya ajabu sana kuwa hata Misri ni jamaa katika ukoo wa Nuhu (sasa basi ardhi ya Misri nayo kwa mujibu wa Biblia inaonekana wazi ni ya Waisraeli, kwa maana hata Ishmail ni mtoto wa Ibrahimu kupitia kwa mjakazi Hajiri Mmisri, kwa hiyo Ibrahim alimposa Hajiri ambaye anatoka katika ukoo wa Nuhu kupitia kwa mtoto wa Nuhu aliyeitwa Hamu ambaye tumeona ni baba wa Misri na Kanaani Mwa.10:6).
Kwa mujibu wa mafungamano ya koo hizi za Kanaani ni dhahiri kuwa Mpalestina (ambaye ana mafungamano makubwa ya kisiasa, kidini, mila na utamaduni na nchi ya Misri ni Mmisri pia kupitia uarabu wao, Misri ndiyo chimbuko la uarabu) kwa vigezo hivyo ndani ya mabano anatoka katika ukoo mmoja na mzee Kanaani na katika ardhi moja ya Kanaani (ambako ndiko Israel ya leo pia, ambayo ndiyo nchi ya maziwa na asali na nchi ya ahadi, nchi ya Agano) kwa maana kwa mujibu wa Mwa.10:6, Misri na Kanaani ni watoto wa Hamu na ni wajukuu wa Nuhu, pia 1Nya.1:8,11.
Hivyo basi uwazi huo wa maandiko unashuhudia kuwa Uislamu wa Mwarabu (Mmisri) haukuwepo wakati MUNGU anafanya Agano hili. Misri haikuwa ya Uislamu kwa sababu Nuhu ambaye ni babu wa Misri kupitia mtoto wa Nuhu aitwaye Hamu hakuwahi kuwa Muislamu hata Farao naye hakuwa Muislamu. Hata YESU alimaliza ukombozi wa dunia wakati Uislamu haujaja duniani. Uislamu umekuja duniani kupitia mafundisho ya mtume Muhammad S.A.W katika karne ya 7 BK, na Agano la MUNGU la kuwapa Waisrael Kanaani lilikwishakuwepo.
Ieleweke baada ya vizazi vya Adam, Nuhu, Ibrahimu, Lutu, Musa, Yakobo na YESU ndipo Muhammad S.A.W amekuja kuwepo. YESU mwenyewe amekuja duniani amekuta MUNGU alikwishawapa Wana wa Israel Yerusalemu yao na ifahamike kuwa MUNGU hakuwatumia Mitume kuandika habari za kuwapa Wana wa Israel Yerusalemu bali aliwatumia Manabii. Mitume akiwemo Muhammad S.A.W wamekuja nyuma ya Manabii, Nabii wa mwisho na Mtume wa kwanza aliyepewa jukumu (mission) la wokovu ni YESU.
Mvutano uliopo unatokana na ukweli kwamba hizi koo zilikuja kutawanyika Mwa.10:18,32 wengine baada ya gharika na ule msitari wa 31 unasema kuwa hata Shemu ambaye ni ndugu yake Kanaani kwa Nuhu, walikuja kugawanyika katika lugha zao, katika nchi (ardhi) zao na wakafuata mataifa yao. Sasa MUNGU anapotoa ahadi kuwa nchi yao anawapa Wayahudi/Waisrael; wanakuwa hawaelewi lugha anayoongea MUNGU ambaye ndiye mwenye ardhi hiyo kwa sababu yeye ndiye aliyeiumba kwa mikono na utashi wake, na vitu vyote ni vya kwake Zab.24:1na sawa na mzazi anapogawa urithi kwa watoto huwa hakuna anayeweza kumpangia kinyume na matakwa yake maana ardhi ni yake na watoto ni wake pia, na sababu kubwa ya wao kutoelewa lugha na iliyofanya nchi yao wapewe Wayahudi/Waisraeli ni kuwa walijiingiza kuabudu miungu wakamwacha MUNGU wa Israel ambaye ndiye MUNGU wa kweli.
Na MUNGU wa Israel mwenye wivu alipoona miungu inaabudiwa; alijitenga nao na alipojitenga nao ile nguvu  ya MUNGU iliyokuwa ndani yao wakati anawapa hiyo nchi (kabla hawajageukia miungu) ilihama ikaenda kwa Wayahudi/Waisrael na kutoa mwanya kwa Wakanaani, Sidoni, Hethi, Myebusi, Mwamori, Mgirgashi, Mhivi, Mwarki, Msini, Mwarvadi, Msemari, Mhamathi kuwa wadhaifu kwa kiwango cha kutomudu vita iliyoweka Kanaani katika milki ya Waisrael na ndiyo maana hata leo Palestina ambaye ametoka katika ukoo dhaifu uliopungukiwa na nguvu za MUNGU kutokana na uasi wa kugeukia miungu ameendelea kukosa nguvu na ushindi kila vita vinapoibuka dhidi yake na Israel ambaye nguvu za MUNGU zilihamia kwake.
Licha ya kwamba mgogoro huu wa kihistoria ulikuwepo hata nyakati za Biblia (Nyakati za utawala wa Torati au Agano la Kale) wakati Wayahudi wa kabila la Kiebrania walipotoka utumwani Misri dhidi ya Mkanaani, Msidoni, Mhethi, Myebusi, Mwamori, Mgirgashi, Mhivi, Mwarki, Msini, Mwarvadi, Msemari, Mhamathi waliokuwa wakiishi kwenye eneo hilo ambalo MUNGU muumba wa nchi na ardhi alitwaa milki yake na kuwapa Wana wa Israel (2Nya.20:7,11), mgogoro wa sasa kati ya Waarabu wa Kipalestina na Wazayoni (Israel) ulianza kama mapambano kuhusu ardhi pia.
Kuanzia mwisho wa vita kuu ya pili ya dunia hadi mwaka 1948, eneo ambalo makundi yote mawili yalidai milki yake yalijulikana kimataifa kama Palestina. Jina hilo moja pia lilitumiwa kuelezea eneo ambalo halikutambulika sana “Ardhi Takatifu” na dini tatu za monotheistic (Mungu mmoja). Kufuatia vita ya mwaka 1948–1949, ardhi hii iligawanywa katika maeneo matatu: dola la Israel, Ukingo wa Magharibi wa mto Yordani na Ukanda wa Gaza. Ni eneo dogo la wastani wa maili za mraba 10,000 au takriban ukubwa wa jimbo la Maryland nchini Marekani, kwa mujibu wa Middle East Research and Information Project ya Washington DC.
Usiyoyajuwa kuhusu Israel.
Palestina kuna dini za Uislamu, Ukristo na Druze (dini 3), hali kadhalika Israel kuna dini 9, huku dini kuu ya taifa ikiwa ni ya Kiyahudi (Jewish) inayowakilisha 75.4% ya idadi ya watu wote wa Israel. Dini zingine ni Uislamu 16.9%, Ukristo 2.1%, Druze 1.7%, Judaism, Kurd, Armenia, Aramean na Bahai zote kwa pamoja zinawakilishwa ndani ya 4% ya watu wote wa Israel wapatao 8,296,000ml [2014] kwa takwimu za Benki ya Dunia, mgawanyo huo wa idadi ya wafuasi wa dini uliripotiwa mwaka 2015 na ripoti ya utafiti wa ndugu Shalom Goldman (ISLAMIC Commentary) yenye kichwa ‘Surveys of religious affiliation in the US and Israel”. Ingawa kuna hoja kuwa Judaism ingestahili kuwa dini ya taifa kwa sababu zaidi ya kuwa dini ni falsafa, ni utamaduni, ni mfumo wa maisha ambavyo vyote hivyo vinagusa raia wengi katika Israel kupitia maingiliano yao ya kimaisha. Sheria za Israel zinatoa uhuru wa kuabudu na serikali ina wizara maalum ya kuratibu masuala ya kidini kama kukarabati nyumba za ibada na kuzilinda zote kwa ajili ya watalii na watu wanaokwenda hija, lakini pia serikali ya Israel inaziruzuku toka bajeti ya taifa dini zote zilizosajiliwa kwa mujibu wa sheria.
 
Taifa la Israel lina mahakama ya juu kabisa ya dini inayosikiliza mashauri yanayohusu dini ambayo yayo hayo hayafunguliwi kwenye mahakama za kiraia. Israel ni nchi yenye nguvu kubwa duniani lakini ambayo haina katiba iliyoandikwa tangu uhuru wake Mei 14, 1948. (Kumbe kuna uwezekano wa nchi kuendeshwa bila katiba na ikawa nchi yenye nguvu kubwa tu duniani kama ilivyo pia Uingereza ambayo katiba yake iko vipande vipande tu yaani siyo moja lakini ni taifa kubwa duniani. Katiba kumbe wakati fulani inaweza kuchelewesha maendeleo kwa mivutano isiyokoma na isiyo lazima inayotokana na katiba yenyewe kushindwa kujisimamia ili kulihuisha taifa).
 
Taifa la Israel mwaka 1949, vyama vya siasa vya kidini ambavyo vina nguvu kubwa pia vilipinga taifa kuwa na katiba ili kuepuka mazingira tata ambayo walihofu kuwa katiba ingeweza kukinzana na misahafu ya dini zao na kuwavurugia mifumo yao ya ibada. Hapa ndipo vyama vya siasa vya kisekula (visivyokuwa vya kidini) vikachagiza ujenzi wa taifa imara duniani (ambalo wakati huo lilikuwa changa kwa umri wa mwaka mmoja tu) kupitia bunge lake linaloitwa Knesset kama chombo kikuu cha taifa. Mataifa mengine katiba ndiyo chombo kikuu ambacho mihimili yote ya dola inaongozwa nayo.
 
Katiba ambayo ndiyo sheria mama, inatoa fursa ya kutungwa sheria za kawaida za kila siku za kuendesha nchi (Acts) ambazo hizo mara nyingi zimekinzana na sheria za kidini mfano unyongaji kwa makosa ya uhaini (dini nyingi zinapinga kutoa uhai), idadi ya watoto wa kuzaa (serikali nyingi zimeweka ukomo wa watoto wanne, wawili nk na zimehamasisha uzazi wa mpango kwa kusisitiza matumizi ya vizuizi vya uzazi, hii ni kinyume na sheria za dini), ndoa ya jinsia moja (Dini nyingi zinapinga uwepo wa ndoa za jinsia moja kwamba ni kinyume na misahafu yao, Israel ni rafiki mkubwa sana wa enzi na enzi wa Marekani ambao wote mataifa yao yanaamini katika Mungu, lakini Israel haikubaliani asilani na sera ya Marekani ya ndoa za jinsia moja) aidha serikali kadha wa kadha zimeruhusu utoaji mimba hata usiotokana na kusalimisha maisha ya mama mjamzito (dini nyingi zinaamini kutoa mimba ni dhambi) nk. Nyumba za ibada za Israel ambayo ina uhuru wa kuabudu zina nguvu kubwa kupitia madhabahu zao ambazo zina uwezo wa kuamua mustakabali wa nchi kupitia waumini wao. Israel ni taifa la ajabu duniani ambapo siasa na dini siyo mahasimu bali ni mapacha wanaofanana, wanaopendana, wasiohujumiana, wanaotegemezana na wanaoshirikiana kuendesha nchi yao, huwezi kutenganisha siasa na dini Israel.
 
Ugumu wa mgogoro kati ya Israel na Palestina.
Israel kuna Waislamu ambao pia wako Palestina na Waislamu wote hawa wanaoamini msahafu mmoja kila mmoja anashikilia kuwa nchi yao ndiyo halali kuwepo kwenye uso wa dunia na siyo vinginevyo.
 
Wadruze wamo Palestina na Israel, nao pia licha ya kuwa na msahafu mmoja lakini kila mmoja katika nchi yao anaamini kuwa nchi yao hiyo ndiyo ina uhalali wa kuwepo kwenye ramani ya dunia.
 
Wakristo wa Israel na wale wa Palestina ambao wote wanaamini msahafu/Biblia mmoja (ila tu kama hao wengine pia, wametengwa tu na mipaka ya nchi hizi mbili hasimu) kila mmoja anaamini kuwa nchi yao ndiyo ipo kwa mujibu wa maandiko na kutaka sheria za kimataifa zitambue hivyo.
 
Wayahudi ambao wameendelea kuamini kuwa Biblia halali ni agano la kale tu yaani kuanzia kitabu cha Mwanzo hata Malaki basi, na kwamba agano jipya siyo Biblia halali japokuwa wanaishi nyakati zake; nao wamo ndani ya taifa la Israel ya leo wakiamini kuwa hakuna kitu kinaitwa Palestina ila Israel tu, sijajuwa kwa nini wasirudishe nyakati/majira nyuma ili wakaishi nyakati za agano la kale.
 
Maajabu ni haya: Waislamu wa Israel wanazikubali nchi za Magharibi ambazo ni marafiki wa Israel ikiwemo Marekani kinyume na Waislamu wengine duniani wanaoipinga Magharibi na Marekani. Kama enzi ya Donald Trump mwenye msimamo mkali dhidi ya Uislamu ikitimia atafanyaje na Waislamu wa Israel ambayo ni rafiki mkubwa wa Marekani? Waislamu wa Israel wana uadui na Waislamu wa Uarabuni kupitia mataifa yao ambayo ni mahasimu wa enzi na enzi. Jeshi la Israel linapohami nchi yao kwa njia ya medani dhidi ya maadui wake wa nchi za Kiislamu huwa vikosi vyake ambavyo vina maafisa wa imani ya Kiislamu pia hushambulia maadui pasina kujali kama dini zao ni Uislamu.
 
Falsafa na sera ya ulinzi na usalama ya Israel imeweka msisitizo kuwa kila raia pasina kujali dini yake; wa rika linalotambuliwa na sheria kuwa mtu mzima ni askari, na wako watu milioni 8,296,000 tu. Aidha maadui wa Israel wanaendesha propaganda kuwa dini zote 8 kasoro dini ya Kiyahudi zinapata haki za msingi za kitaifa kinadharia tu.
 
Maswali magumu ambayo Kanisa lina kigugumizi kwayo.
Yafuatayo ni maswali magumu ambayo Kanisa limekaa kimya na asilimia kubwa ya Wakristo wasio Waisrael hawajafunuliwa kwayo ili wakajuwe kwa ufasaha uhusiano wao na Israel.
 
Je, unafahamu kwamba unapoiombea Israel unaziombea pia imani zingine zisizo za Kikristo kama Judaism, Jewish, Uislamu, Druze, Kurd, Armenia, Aramean na Bahai? (hawa hawamkubali Kristo) maana serikali ya Israel inazitambua imani zote hizo kuwa zina haki sawa katika ardhi na baraka zote za Israel kama taifa.
 
Je, kama serikali ya Israel haijazibagua imani hizo, wewe usiye Muisrael utazibaguaje katika imani na maombi yako? Haijalishi zingine zinaabudu giza (imani isiyo ya Ukristo)? Wakristo wako 2.1% tu ya watu wote wa Israel. Inaaminika hata hapa Tanzania Waislamu ni wengi kuliko Wakristo. Mfano rahisi kuthibitisha hili ni huu: katika eneo linalohudumiwa na Kanisa/usharika/parokia moja kuna shule ya Jumapili moja yenye takriban kwa uchache wanafunzi 150 lakini madrasa zikiwa ni zaidi ya kumi yenye watoto zaidi ya 50 kwa kila madrasa.
 
Je, unajuwa kwamba unapofungamana na Uislamu wa Israel kwa kigezo kwamba wako ndani ya ardhi moja na Wakristo (ardhi ambayo ndiyo baraka za Mkristo zimeahidiwa kwa kufunganishwa nayo) basi pia unafungamana na Uislamu wa nchi yako, Palestina na sehemu zingine za dunia maana imani yao inashabihiana popote duniani na msahafu wao ni mmoja japo wana madhehebu kama Suni, Shia na Ibadi? Israel inawatambua Waislamu na wako 16.9% wakishika nafasi ya pili nyuma ya Jewish ambao ni 75.4%, Tanzania nako serikali inatambua Uislamu.
 
Je, Mungu aliposema ukiibariki Israel utabarikiwa, alimaanisha kuwa uzibariki na imani zingine hizo zisizofungamana na Ukristo? Kumbuka Kanaani mwana wa Hamu mtoto wa Nuhu alisambaratishwa na Mungu kwa kosa la uasi (kuabudu miungu na kujitegemeza kwenye baraka zitokanazo na miungu hiyo).
 
Je, utaambatanaje na Wakristo wa Israel kwa sababu wewe ni Mkristo mwenzao na ukawabagua Wakristo wa Palestina ambao wote mnaamini Biblia/Msahafu mmoja? Umoja wenu katika mwili wa Kristo uko wapi hapa? Lakini kumbuka Mkristo wa Palestina ni hasimu wa Mkristo wa Israel. Hili swali pia nimelitega kwa lile kundi linaloikana Israel ya leo (jibu lake naliweka kwenye mabano ili wachemshe bongo).
 
Je, kwa nini tusiende kuhiji pia Palestina ambako nako kuna Wakristo tena wengine wametoka Israel kwenda kuolewa huko? Palestina na Israel ziko kwenye ardhi moja ya Nuhu tunayemhubiri kwenye Biblia (Misri na Kanaani ni watoto wa Hamu mwana wa Nuhu).
 
Je, unapopeperusha bendera ya Israel au kutumia kitu chochote kinacho kampenia utaifa wa Israel unajuwa kuwa unatukuza pia miungu ya Judaism, Uislamu, Druze, Kurd, Armenia, Aramean na Bahai kwa sababu dini hizi pia ziko ndani ya Israel na zinatambuliwa na serikali ya Israel hiyo?
 
Je, unajuwa kuwa dini zote hizo katika nchi zote mbili za Israel na Palestina zinaruhusu kuoana (inter-marriage) maana sheria za nchi hazibagui uhuru wa mtu kuoa (japo hili hapo awali liliruhusiwa kama mbinu ya kijasusi dhidi ya taifa lingine kutaka kujuwa siri za hasimu wake)? Sisi hapa Tanzania imani zetu hazijakubali kuoa dini/imani nyingine, ingawa serikali haizuii, Yasser Arafat alikuwa Muislamu aliyeoa Mkristo mzungu.
 
Je, unajuwa kuwa unapoikanyaga na kuibariki ardhi ya Israel na unapotwaa udongo wake kuuleta nyumbani kwako basi umebariki ardhi na pia umetwaa udongo ambao umesimikwa na roho za Ukristo, Judaism, Jewish, Uislamu, Druze, Kurd, Armenia, Aramean na Bahai ambazo zote hizi ndizo zinaunda Israel?
 
Je, tunabarikiwa na kufungamana na Israel ambayo dini yake kuu (ya serikali) ni dini ya Kiyahudi ambayo hiyo inaamini kuwa Biblia ni agano la kale (Mwanzo hata Malaki) tu basi na kwamba hawaikubali agano jipya (Mathayo hata Ufunuo wa Yohana) ambayo hii ni kuikana Injili na kama ni kuikana Injili basi ni kumkana Kristo (ambaye agano la kale wanalolikubali limetangulia kutabiri ujio wake wakati wa agano jipya) ambaye huduma yake ya kuikomboa dunia imefanyika na kuandikwa kwenye agano jipya. Kumbuka Injili maana yake ni uweza wa Mungu uletao wokovu. Sasa ina maana tunafungamana na kubarikiwa na Israel isiyotambua uweza wa Mungu (wokovu)? Duh! sasa tunafanyaje hapa? Homework hiyo kafanye ulete majibu, tena tufanye haraka maana Yesu yu karibu kulichukuwa Kanisa.
 
Je, wajuwa kwamba kuna Wayahudi ambao dini yao ni ya Kiyahudi (Jewish) na kuna Wayahudi ambao ni wafuasi wa dini za Ukristo, Judaism, Uislamu, Druze, Kurd, Armenia, Aramean na Bahai? Huko Ulaya kwenye karne ya 18 walikuwepo Wayahudi ambao pia walikuwa kwenye dini ya Freemasonry kama ambavyo tutaona kwenye mfululizo wa mafundisho haya.
 
Je, tukifungamana na Wakristo tu wa Israel ina maana Judaism, Jewish, Uislamu, Druze, Kurd, Armenia, Aramean na Bahai tunawakana wakati kwa sheria za Israel ukisema Israel maana yake ni dini 9 zote hizo, hivyo kuzikana hizo 8 (kasoro Ukristo) ni kuwanyima haki zao za kuwa Wana wa Israel, au Wana wa Israel ni Wakristo tu (ambao ni 2.1%)?. Vipi kwa nchi yetu hii inawezekana kukana dini nyingine au kufungamana nayo?
 
Je, Mungu aliposema katika “Mwa.12:3 jamaa zote za dunia watabarikiwa kwako (yaani Israel)” ina maana alimaanisha Israel ya dini/imani ipi kati ya Ukristo, Judaism, Jewish, Uislamu, Druze, Kurd, Armenia, Aramean na Bahai?
Je, Israel hii inayotambua dini/imani zingine ambazo mfano wake katika agano la kale Mungu alizisambaratisha kwa dhambi ya kuabudu miungu; kweli ni Israel ya Mungu au ni iliyotengenezwa na Freemasonry? Homework kwako mpendwa mwanafunzi wa somo hili.
Mungu alipiga marufuku kuabudu miungu mingine, anasema kwenye “Kut.20:2-3 Mini ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi” Israel ya leo kama ilivyokuwa ya Agano la Kale pia kuna miungu ya Judaism, Uislamu, Druze, Kurd, Armenia, Aramean na Bahai, idadi ya wafuasi wao ni kubwa kuliko wafuasi wa Yesu (Wakristo ambao ni 2.1% tu).
Imani kubwa zinazopatikana duniani zimesimama kwenye falsafa na nguzo zao ambazo ndizo zinafanyika utambulisho wao na kuzitofautisha na imani zingine; falsafa hizo kwa majina ya dini zake ni Roman Catholicism, Eastern Orthodox, Lutheranism, Anglicanism, Calvinism, Methodism, Islam Suni, Islam Shia, Islam Ibadi, Theravada Buddhism na Vajrayana Buddhism.
 
Inline image
 
 
Illuminati na Freemasonry ni nini?
Hizi ni itikadi za kiibada zilizozuka baada ya Yesu Kristo (AD) zenye malengo ya siri kubwa; yanayosighishana na ibada zinazoabudu Mungu katika Utatu Mtakatifu (Holly Trinity) au katika umoja wake (Monotheistic God), itikadi ambazo agenda zao kuu ni kubadili mfumo wa dunia uliopo na kuusilimisha kuwa mfumo mpya mmoja wa ibada na wa maisha kwa ujumla wake. Illuminati na Freemasonry ni taasisi za kiibada mbili tofauti lakini zinazofanana kwa agenda na mikakati yao kwa asilimia kubwa. Tayari inaaminika kuwa wamefanikiwa kuchagiza mabadiliko ya mfumo wa dunia kwa kiwango kikubwa. Ibada pasina sadaka siyo ibada tangu enzi za Agano la Kale na kwa imani zote na mifumo yote ya kuabudu chini ya jua. Sadaka za ibada za taasisi hizi zinadhaniwa kuwa ni kafara ya damu, wakiamini juu ya nguvu ya damu kama sadaka kuleta mabadiliko, wakimrejea hata Bwana Yesu kuwa alifanikiwa kuikomboa dunia kwa kafara ya dhabihu ya damu yake msalabani.
 
Kwa imani ya Ukristo, msalaba kama mti uwao wote ule haukuwa na nguvu hadi pale ulipopokea (ulipochuruzikiwa) damu ya Yesu ambayo ndiyo nguvu kuu. Kama msalaba ungekuwa na nguvu basi hata ardhi ya Kalvari ingepokea nguvu hiyo ya msalaba maana ulisimikwa kwayo, lakini ardhi ile ikaja kuunguruma kwa tetemeko kuu baada tu ya kuchuruzikiwa damu ya Yesu isiyokuwa na hatia, hatutakaswi kwa msalaba bali kwa damu ya Yesu. Hata sasa kuna madhehebu ambayo yanavalia rozari yenye msalaba lakini wakati fulani wasipate majibu ya mahitaji yao hadi pale wanapoalika nguvu za damu ya Yesu, ingawa hatuwezi kupuuza nafasi ya msalaba kwa habari ya kusulubisha dhambi.
 
Sina uhakika kama dini ya Freemasonry ambayo inadhaniwa ina wafuasi wanasiasa, matajiri, viongozi wa dini, walozi, wataalam waliobobea kwenye fani mbalimbali muhimu kwa maendeleo ya binadamu imesajiliwa na serikali ya Tanzania au la, na kama imesajiliwa rasmi kama dini zingine sijajuwa iko chini ya umoja upi wa kidini unaotambuliwa na serikali kati ya CCT, TEC na CPCT au hawana umoja wao kama walivyo wapagani. Aidha kama wanaoabudu huko wengine wanadhaniwa kuwa Wakristo, Waislamu na labda Wapagani, basi ni sawa na kusema kuwa Freemasons hawahitaji usajili wa kiserikali madhali kwenye sehemu zingine za dunia wanaripotiwa kujipenyeza na kuwatwaa viongozi wa dini ambao sasa wanatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja.
 
Illuminati na Freemasonry zenyewe zinahusianaje?
Kimsingi, uhusiano wa pekee ulio kati ya taasisi hizi mbili za imani ni kuwa baadhi ya wafuasi wao walikuwa na uanachama wa taasisi zote mbili huku wengine wakisalia kwenye taasisi moja tu. Hata hivyo, uafuasi katika Illuminati ulivyokuwa haraka, serikali ya Bavaria ilianza kuzivunjilia mbali. Hatua hiyo ilipelekea wao kuanza kujijenga upya kwa mfumo wa madaraja ya ufuasi (degree system) ambayo hii ilichagizwa na Masonists. Aidha wapo wana illuminati ambao hawajuani na Freemasons.
 
Zilianzishwa wapi na lini?
Kwa mujibu wa chapisho la Masonic Light iliyohaririwa mnamo tarehe 17 Aprili 2004, Illuminati ilianzishwa huko Bavaria, Ujerumani mwezi Mei 1776 na Freemasonists Adam Weishaupt na Adolph Von Knigge.
 
Kwa madhumuni gani?
Freemasons wanajitanabahisha kuwa agenda yao kuu ni huruma kwa binadamu (ambayo ndiyo falsafa ya dini yao) kwa njia ya kutoa fadhila na misaada kwa masuala yanayokwamisha mataifa na dunia kama mabalaa kama milipuko ya magonjwa, misaada ya kibinadamu katika vita na maafa yanayofanana na hayo. Kwa hapa nyumbani Mkuu wa wilaya ya Ki-freemasonry ya Tanzania amewahi zaidi ya mara moja kufadhili kampeni ya kitaifa ya chanjo ya kutokomeza ugonjwa wa polio kupitia Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa.
 
Aidha wanadhaniwa kuwekeza mitaji mikubwa katika teknolojia ya habari na mawasiliano, uwekezaji ambao ni mojawapo ya mikakati yao ya kuitamalaki dunia wakitumia mifumo ya teknolojia ya habari na mawasiliano ya mitandao jamii kuifanya dunia ijiendeshe kama kijiji kimoja ambapo lengo ni kumjuwa kila mtu kwa anuani yake, utaifa wake, wajihi wake, sura yake na wasifu wake ili kurahisisha utekelezaji wa mikakati yao ya kusimika mfumo mpya wa dunia (The New World Order).
 
Sambamba na mkakati huo, sekta ya fedha na uchumi ndiyo njia kuu ya kuchagiza shughuli za Freemasonry na katika hili inadhaniwa pia kuwa wanafanya bidii kubwa kufanikisha unabii wa maandiko kuwa mojawapo ya ishara za siku za mwisho wa dunia ni kuwa kutakuwa na sarafu moja ambayo hiyo ndiyo itatamalaki sekta ya fedha na uchumi duniani kwa kuwa sarafu pekee ambayo itakuwa inatumika kwenye miamala yote ya malipo duniani, tayari mataifa mengi yanathamanisha sarafu zao kwenye dola ya Marekani. Mojawapo ya mikakati ya kufanikisha mpango huo inaaminika kuwa ni utaratibu wa sasa wa mabenki mengi duniani kuridhia matumizi ya kadi moja ya malipo (credit card) na kadi ya visa ya kutolea pesa kwenye mashine maalum (Automated Teller Machine) ambapo kupitia mfumo huo wa kibenki unaweza kutoa pesa popote duniani na kwamba mpango huu sasa umefanikiwa kuiunganisha dunia nzima kwenye soko moja la fedha. Mabadiliko ya serikali nchini Marekani ambayo kwa mitazamo mingi na kwa kuzingatia historia huwa yanahusishwa na Freemasonry na ndiyo maana mabadiliko hayo yanapotokea huwa masoko ya hisa na thamani ya sarafu za nchi mbalimbali duniani yanaathirika.  
 
Itikadi hizi za kidini za Illuminati na Freemasonry kama tulivyoona hapo juu kuwa wanafadhili miradi mingi ya kijamii kupitia serikali zilizopo, pia wanatumia mifumo dhaifu inayolalamikiwa; ya serikali za dunia kuchagiza mabadiliko hata kwa kuangusha serikali hizo lakini kwa agenda ya siri ya kupata sadaka zao za kafara ambazo mahala pengi zimeaminika kuwa ni damu. Hivyo mabadiliko yanafanyika kwa njia ya machafuko ambayo humwaga damu lakini baada ya hapo mfumo bora unasimikwa na wanajamii wanaridhika. Endelea kusoma utaona rejea ya madai haya kwenye mfululizo unaofuata wa mafundisho haya.
 
Israel ya leo inahusishwa vipi na Freemasonry?
Uchunguzi na tafiti nyingi ama za kushabihiana au kusighishana na maarifa haya zinaweza kuendelea kufanyika na kwamba haya yaliyofunuliwa hapa hayatoshi asilani.
 
Itikadi na falsafa ya Bolshevism iliyoundwa na kundi la wafuasi wa Marxist Russian Social Democratic Labour Party ambao wanaaminika kushirikiana na Bolsheviks wa Kiyahudi waliokuwa Urusi wanahusishwa na mapinduzi ya Kirusi (Russian Revolution au Bolshevik Revolution ya Oct 1917). Vladimir Lenin anatajwa kumkariri Kiongozi wa Bolshevik wa Kirusi George Solomon aliyeasi toka kwenye Freemasonry aliyesema kuwa Bolshevists wa Kiyahudi ambao walikuwa Freemasons walifadhili mapinduzi ya Urusi kwa nia ya kupata kafara ya damu hivyo wakakubaliana na wenzao wa Kirusi kuasisi mapinduzi hayo yanayokadiriwa kumwaga damu za watu wanaokadiriwa kuwa kati ya 85ml na 100ml kwa mujibu wa Socio-economics History Blog na pia Black Book of Communism by Martin Malya.
 
Hii inathibitisha kwamba Freemasonry ina mtandao dunia nzima hadi ndani ya Uyahudi. Hata hivyo huko Ulaya, kila mahali walipoasisi machafuko/mapinduzi walivunjwa na serikali hizo baada ya kugundulika, maana wanafanya kazi zao kwa siri kubwa sana ambapo kuwagundua siyo rahisi, wanagundulika baada ya maangamizi makubwa kutimia na kuziweka dola katika hali tete hivyo mojawapo ya hatua zilizochukuliwa na dola hizo ni kutokomeza makundi haya.
 
Aidha Illuminati wanadhaniwa kuasisi pia mapinduzi ya Ufaransa (French Revolution) ya mwaka 1789 hata 1799, ambayo kiini chake siyo kwamba Ufaransa ilikuwa masikini lakini zaidi kwa sababu Kiongozi aliyepokea kijiti cha mapinduzi na kuyaendeleza Napoleon Bonaparte; kupitia mafukara walioitwa Proletariats waliona kwamba wachache wenye ukwasi wa mali na elimu walioitwa Bourgeois walishindwa kuhusisha kiwango cha maendeleo ya elimu na uchumi wa taifa na kuyafasiri na kuyaakisi kwenye uhalisia wa kisiasa na kijamii chini ya Mfalme Louis wa 14, badala yake mafanikio hayo yakaelekezwa kuimarisha ufalme wa Louis kwa kukata mizizi ya ukabaila huku mifumo ya ukabaila kutoka nje (walanguzi-papa wa ardhi toka nje) ikishamiri na kufanyika mzigo mzito kwa mafukara Proletariats.
 
Ufaransa ikawa inaongozwa na Ma-bourgeois na Makuhani huku wavuja jasho walio wengi wakibebeshwa mizigo mingi mizito ya kodi kwa ajili ya kufadhili vita vya nje ya nchi (Italia, Misri nk), matumizi ya kifisadi ya idara ya mahakama iliyokuwa imejikita kushughulikia mashauri ya watuhumiwa wa mapinduzi na mapapa wa ufisadi toka kwenye kundi la Mabourgeois waliotaka kuiweka sehemu kubwa ya ardhi oevu ya Ufaransa kwenye milki ya makabaila, pia mzigo huo wa kodi ulitumika kulipia deni la taifa lililokuwa likipaa. J. M. Thompson, The French Revolution (1945), N. Hampson, A Social History of the French Revolution (1963), The French Revolution (1928), a royalist account. Wengi wameandika juu ya mapinduzi haya yaliyoleta enzi mpya Ulaya.
 
Sasa hapa tunaona moja ya mizizi ya kale sana yanayohusisha Makuhani na Wayahudi na kazi za Illuminati na Freemasonry. Leo uhusiano huu bado unarejelewa kuwepo kwenye uso wa dunia hata leo. Unabii ulitolewa kuwa kabla Yesu hajarudi kuchukuwa Kanisa, Wayahudi wote waliosambaa nchi za mbali watarudi Israel katika hali zote ama wakiwa hai au mifupa yao kwa ajili ya tukio hilo la kurudi Yesu (Advent). Sasa kati yao wanaorudi, wamo ambao wanadhaniwa kuwa ni wafuasi wa Freemasonry na Illuminati na hawa basi ndiyo wanaweza kuhisiwa kufanyika mawakala wa kuratibu Israel ya sasa kuwa ya Freemasonry.
 
Uhusiano wa Freemasonry na Marekani.
Suala la ama kweli au uongo kuwa Thomas Jafferson anahusishwa na Freemasonry limejadiliwa kwa miaka mia mbili huku waumini wa Masonic wakipinga kuwa hakuwahi kuwa mfuasi wa Freemasonry kwa vile hakuna ushahidi wa kumhusisha na ufuasi huo. Hata hivyo uhusiano wake wa karibu sana na Masonics kama akina George Washington, Benjamin Franklin, John Paul Jones, James Monroe, Lewis Meriwether, William Clark na Voltaire vinamhusisha na Freemasonry. Ushahidi unaoshikiliwa kumhusisha Thomas Jafferson Rais wa tatu wa Marekani mwaka 1800 kinara aliyeandika tangazo/azimio la uhuru wa Marekani; na Freemasonry ni baada ya kifo chake July 4, 1826 ambapo nyumba za wageni zilizoitwa Grand Lodge of South Carolina na Grand Lodge of Louisiana zilifanyika matanga ya Kimasonic kwa ajili ya msiba wake.
 
Pia anadaiwa kuhudhuria mikutano ya Kimasonic enzi za uongozi wake. “I believe that every human mind feels pleasure in doing good to another, Thomas Jafferson” (Ninaamini kuwa kila fikra ya binadamu inaridhika katika kumtendea mwenzake mema, tafsiri isiyo rasmi), kauli yake hii inachukuliwa kuwa hakukana kujihusisha na shughuli za Kimasonic. Wengi walihitimisha mjadala huu wakidai kuwa kumhusisha Rais Thomas Jafferson na ufuasi wa Masonic ni chaguo/uamuzi wa kibinafsi wa ama ndiyo au hapana, anaandika mwandishi wa kitabu cha Famous American Freemasons: Volume II. Sasa inathibitika kuwa mataifa makubwa duniani (na hata madogo) yana uhusiano na Freemasonry. Hapa pia ndipo Israel ya sasa inahusishwa na Freemasonry, ikizingatiwa uhusiano wake mkubwa sana wa kihistoria na taifa la Marekani.
 
Kwa nini nyumba za ibada hazipaswi kuzihofu Illuminati na Freemasonry?
Mifumo mipya ya dunia (New World Orders) iliwahi kuwepo pia huko nyuma, nazo ni: Agano la Kale ambalo lilikuja pale Mungu alipotaka kuiondoa dunia toka katika imani iliyokuwepo, na Agano Jipya lililokuja baada ya lile la kale, na sasa tunaona mchuano mkali wa kupandikiza mfumo mpya wa dunia (New World Order) ya Illuminati na Freemasons ambao hatujui utakuwa kama ule uliotangulia Agano la Kale au la. Tofauti ya msingi ni kuwa mfumo wowote mpya wa dunia uliokuwa ukiasisiwa na Mungu ulilenga utawala wa nuru na ule wa Illuminati na Freemasons unalenga utawala mbadala na huo.
 
Kwa hiyo Kanisa na jamii havipaswi kuona chagizo hili la mfumo mpya wa dunia wa Illuminati na Freemasonry kama mwisho wa dunia la hasha! Maana tumeona hapo kuwa mifumo mipya ya dunia imewahi kuwepo tangu uumbaji na kwamba hii ya Illuminati na Freemasonry inatakiwa kuwa changamoto tu ya kiimani na kufanya kazi za kihuduma kwa mikono imara zaidi kwa ajili ya kumuandaa Bi. Harusi (Kanisa) kumlaki Bw. Harusi wake (Yesu Kristo) anaporudi kwa ajili ya unyakuo. Hata huko nyuma tumeona giza halikuwahi kuishinda nuru. Kristo maana yake ni ushindi. Shalom, Shalom Kanisa.
 
Majwala

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Maoni 1 :

Japhet Kamkono alisema ...

Halo ndugu habari za wakati huu.
Kabla ya kusoma makala yako hii nilikua nimesoma na kutazama video moja hivi inayo waonyesha waisrael(wayahudi).Wakifanyiwa mahojiano na mtu mmoja hivi hasa aliwahoji juu ya YESU.
Maswali na majibu haya hapa.
1.YESU NI NANI? Jibu: "NABII WA WAKRISTO".
2.Adui wa kwanza wa MYAHUDI NI NANI? Jibu: WAKRISTO.
3.Kwanini wakristo ndio adui mkubwa wa MYAHUDI?
Jibu:Wakristo ndio watu wakwanza duniani kuazimia kuifuta nchi ya israel na kuazimia kuwaua waisrael wote wasiwepo katika uso wa dunia.Kutekeleza azimio hilo wakristo walianza kuwaua wayahudi kokote walikokua katika nchi za ulaya zote na mashariki ya kati.Ambapo zaidi ya wayahudi milioni 12 waliotawanyika ulaya pekee waliuliwa.Italia ya papa iliua wayahudi milioni 6 na wakristo wengine milioni50 ambao walikataa kumtambua papa kua ni muwakilishi wa MUNGU DUNIANI.Ufaransa,Ureno,Uhispania kwa pamoja ziliua wayahudi zaidi ya milioni 5.Hivyo adui namba moja wa myahudi ni mkristo.

4.Adui wa pili wa myahudi ninani?
Jibu:Waarabu ndio adui wa pili wa myahudi ambao walifuata nyayo za wakristo kuazimia kuwafuta wayahudi katika uso wa dunia.Tena mwarabu amejaribu mara nyingi lakini bado majaribio ya mwarabu hayajaweza kuleta madhara kwa myahudi kama majaribio waliyoyafanya wakristo.
5.ISRAEL NA WAISRAEL NI DINI GANI?
Jibu:Wayahudi wanadini yao ya JUDAISM na kitabu chao kitakatifu cha TORA.
ANGALIZO:Wayahudi waliotawanyikia ulaya walilazimishwa kujiunga na ukristo na wale waliotawanyikia arabuni walilazimishwa kujiunga na uislamu. MKRISTO UNAPO ENDA KUHIJI KULE ISRAEL UNAKWENDA KAMA MTALII UIENDE UKITEGEMEA WAYAHUDI WANAKUFURAHIA NA WANAPENDA UKRISTO HAPANA.WANAPENDA KUPOKEA WATALII SABABU WANAINGIZA PESA KATIKA IDARA YA MAKUMBUSHO.