Kwanini
Mzabibu? Kwani Bwana alishindwa kuchagua miti mingine mizuri na ya
gharama zaidi porini, akachagua kujiita Mzabibu? Haya ni mwaswali ambayo
nilijiuliza. Maana Yesu ni Mzabibu na sisi ni matawi, na Baba yake ni
Mkulima (Yohana 15:1, 5).
Nimeona mambo kadhaa:
1. Mungu amekuchagua sio kwa UBORA wako, ila kwa sababu amekupenda.
"1Neno
la BWANA likanijia, kusema, 2Mwanadamu, mzabibu una sifa gani kuliko
mti mwingine, au tawi la mzabibu lililokuwa kati ya miti ya msituni?
3Je! Mti wake waweza kutwaliwa, ili kufanya kazi yo yote? Watu waweza
kufanya chango kwa huo, ili kutundika chombo cho chote? 4Tazama, watupwa
motoni kwa kuni moto umeziteketeza ncha zake zote mbili, nao umeteketea
katikati, je! Wafaa kwa kazi yo yote? 5Tazama, ulipo kuwa mzima,
haukufaa kwa kazi yo yote; sembuse ukiisha kuliwa na moto, na kuteketea;
je! Waweza kufaa kwa kazi yo yote?" (Ezekieli 15:1-5).
2.
Kwa kuitwa MZABIBU au TAWI la mzabibu, maana yake, Mungu anajua MWANZO
wako na udhaifu wako (kwamba huwezi neno lolote pasipo yeye), na ambavyo
hukufaa kwa chochote; ila amekuchagua kwa KUSUDI lake na kwa AJILI
yake, na anategemea MATUNDA kutoka kwako.
Ndo
maana BWANA anasema, "Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi
niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda
yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu
awapeni" (Yohana 15:16) Hatuna haki yetu wenyewe iliyotustahilisha
kuitwa wana wa Mungu; sisi tumechaguliwa tu. Hii ni maana halisi ya
Neema.
3. Kuna GHARAMA imelipwa kukufikisha hapo ulipo sasa.
Ukisoma Ezekieli 16: 1-63, Utaona jinsi ambavyo BWANA ameGHAMIKIA watu wake, na sasa WAMEFANIKIWA na WAMEMWACHA!
Angalia, mambo machache katika mlango huu:
[i]. Ulikotoka/Asili yako - umetoka kati ya mataifa
"Asili yako na kuzaliwa kwako kwatoka katika nchi ya Mkanaani; Mwamori alikuwa baba yako, na mama yako alikuwa Mhiti" (.
Eze. 16:3b)
Eze. 16:3b)
[ii].
Kuzaliwa kwako - Hakuna aliyekijali, ulikuwa masikini tu aliyestahili
kufa kwa sababu uliachwa. Hukupendwa, hakuna aliyekujali, huna jina.
"4Na
katika habari za kuzaliwa kwako, siku ile uliyozaliwa, kitovu chako
hakikukatwa, wala hukuoshwa kwa maji usafishwe; hukutiwa chumvi hata
kidogo, wala hukutiwa katika nguo kabisa. 5Hapana jicho lililokuhurumia,
ili kukutendea lo lote la mambo hayo kwa kukuhurumia; lakini ulitupwa
nje uwandani, kwa kuwa nafsi yako ilichukiwa, katika siku ile
uliyozaliwa" (Eze. 16:4, 5).
[iii]. Mungu akakufuata katika hali yako mbaya na KUKUOKOA, ukapewa UZIMA bure.
"
6Nami nilipopita karibu nawe, nikakuona ukigaagaa katika damu yako,
nalikuambia, Ujapokuwa katika damu yako, uwe hai; naam, nalikuambia,
Ujapokuwa katika damu yako, uwe hai" (Eze. 16:6).
[iv]. Mungu AKAKUBARIKI na KUKUONGEZA
"7Nalikufanya
kuwa maelfu-elfu, kama mimea ya mashamba, ukaongezeka, na kuzidi kuwa
mkubwa, ukapata kuwa na uzuri mno; matiti yako yakaumbwa, nywele zako
zikawa zimeota; lakini ulikuwa uchi, huna nguo" (Eze. 16:7)
[v]. Mungu akakuFUNIKA aibu yako. Sasa unaHESHIMA na JINA mjini
"8Basi,
nilipopita karibu nawe, nikakutazama; tazama, wakati wako ulikuwa
wakati wa upendo; nikatandika upindo wa vazi langu juu yako,
nikakufunika uchi wako; naam, nalikuapia, nikafanya agano nawe, asema
Bwana MUNGU, ukawa wangu" (Eze. 16:8).
[vi]. Ukapewa kusafiwa kwa Neno na kujazwa Roho na VIPAWA, ambavyo vimekufanyia NAFASI ya KUKETI na wakuu wa nchi
"9Kisha nikakuosha kwa maji; naam, nalikuosha kabisa damu yako, nikakupaka mafuta" (Eze. 16:9)
[vii].
UTUKUFU wa Mungu ukadhihirika maishani mwako kwa ile NEEMA uliyopewa;
Mkono wa Mungu ulidhihirika sana juu yako, naam, ukavikwa UTAYARI kwa
ajili ya HUDUMA.
"10nikakuvika
nguo ya taraza, nikakupa viatu vya ngozi ya pomboo, nikakufunga nguo ya
kitani safi kiunoni mwako, nikakufunika kwa hariri. 11Nikakupamba kwa
mapambo pia, nikatia vikuku mikononi mwako, na mkufu shingoni mwako.
12Nikatia hazama puani mwako, na pete masikioni mwako, na taji nzuri juu
ya kichwa chako. 13Hivyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha; na mavazi yako
yalikuwa ya kitani safi, na hariri, na kazi ya taraza; ulikula unga
mzuri, na asali, na mafuta; nawe ulikuwa mzuri mno, ukafanikiwa hata
kufikilia hali ya kifalme" (Eze. 16:10-13).
[viii]. JINA lako likawa MAARUFU kwa sababu ya ile NEEMA juu yako, na KUFANIKIWA sana juu ya nchi.
"14Sifa
zako zikaenea kati ya mataifa kwa sababu ya uzuri wako; kwa maana
ulikuwa mkamilifu, kwa sababu ya utukufu wangu niliokutia, asema Bwana
MUNGU" (Eze:16:14).
4. Baada ya KUFANIKIWA umefanya nini? Je! Umemkumbuka BWANA na kuendelea KUMTAFUTA na KUMFUATA kwa BIDII?
[i]. Wapo walioABUDU mafanikio yao badala ya Mungu! Na kufanya MACHUKIZO yale ya MATAIFA walikotwaliwa.
"15
Lakini uliutumainia uzuri wako, ukafanya mambo ya kikahaba kwa sababu
ya sifa zako, ukamwaga mambo yako ya kikahaba juu ya kila mtu aliyepita;
ulikuwa wake" (Eze. 16:15).
[ii].
Je! Umekumbuka ULIKOTOLEWA na Mungu? Pale ulipokuwa sio kitu chochote,
wala huna jina? Sasa, badala ya kuwapeleka wengine kwa BWANA unawapoteza
na wale walio wadogo; Umewapotosha!
"21hata
ukawaua watoto wangu, na kuwatoa kwa kuwapitisha motoni kwa hao? 22Na
katika machukizo yako yote, na mambo yako ya kikahaba, hukuzikumbuka
siku za ujana wako, ulipokuwa uchi, huna nguo, ukawa ukigaagaa katika
damu yako" (Eze. 16:21, 22)
[iii].
Sasa unajijengea UFALME wako, na JINA lako na wala humwinui Mtakatifu
wa Israel! Unajifanyia mambo yako kwa faida zako kwa kuzidisha machukizo
yako.
"25Umejenga
mahali pako palipoinuka penye kichwa cha kila njia, ukaufanya uzuri
wako kuwa chukizo, ukatanua miguu yako kwa kila mtu aliyepita karibu,
ukaongeza mambo yako ya kikahaba" (Eze. 25).
[iv].
Kwa ajili ya FAIDA yako unafanya KAMA wafanyavyo mataifa, na Jina la
BWANA linatukanwa juu ya nchi. Wanasema, "hivi na huyu ni mtu wa Mungu,
mbona anafanya hivi?"
"26Tena
umezini na Wamisri, jirani zako, wakuu wa mwili; ukaongeza mambo yako
ya kikahaba, ili kunikasirisha....28Pia umefanya mambo ya kikahaba
pamoja na Waashuri, kwa sababu ulikuwa huwezi kushibishwa; naam,
umefanya mambo ya kikahaba pamoja nao, wala hujashiba bado. 29Pamoja na
hayo umeongeza mambo yako ya kikahaba katika nchi ya Kanaani, mpaka
Ukaldayo, wala hujashibishwa kwa hayo" (Eze. 26, 28-29).
[v]. Je! Hukukaza mkono wako KUTAWALA na KUTUMIKISHA wengine kwa FAIDA yako tu?
"30Jinsi
moyo wako ulivyokuwa dhaifu, asema Bwana MUNGU, ikiwa unafanya mambo
hayo yote, kazi ya mwanamke mzinzi, 31apendaye kutawala watu; kwa kuwa
wajijengea mahali pako pakuu penye kichwa cha kila njia, na kufanya
mahali pako palipoinuka katika kila njia kuu; lakini hukuwa kama kahaba,
kwa maana ulidharau kupokea ujira. 32Mke wa mtu, aziniye! Akaribishaye
wageni badala ya mumewe!" (Eze. 16:30-32)
[vi].
Umevifanyia nini VIPAWA vya Mungu? Fedha na utajiri, na Neema? Je!
Hivyo havikuwa uharibifu kwa wengine na kubomoa Zaidi kuliko kujenga?
"17Pia
ulivitwaa vyombo vyako vya uzuri, vya dhahabu yangu na vya fedha yangu,
nilivyokupa, ukajifanyia sanamu za wanaume, ukafanya mambo ya kikahaba
pamoja nazo" (Eze. 16:17)
5.
Kuna jambo Mungu alitarajia kukona baada ya kukuinua kwa kiasi hicho.
Je! Umerudi nyuma hata ukamsikitisha Mungu? Mafanikio yako yanamtukuza
Mungu au yanamtukana?
Kumbuka
hali yako ya mwanzo ulipokuwa si kitu, kama mti wa mzabibu usio faa kwa
chochote, sasa uko juu sana kwa kuwa BWANA amekuinua.
Haya
maneno yamesema na mimi kwa nguvu kubwa, na nimeona nilivyopungua.
Nimeweka hapa, sio kukuhukumu ila kama mimi Frank nilivyopata changamoto
na kujitathminina, nimeweka hapa ili uone kama kuna mahali pa
kurekebisha, rekebisha; ILI kwa mara hii tena MAFANIKIO yako yawe Baraka
si kwa watu tu ila na kwa Mungu pia.
Frank P. Seth
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Mawazo yako ni muhimu sana tafadhali tumia lugha nzuri na tutairusha na wengine waisome.