Jumanne, 5 Aprili 2016

SIRI ZA JANGWANI SEHEMU YA KWANZA BY Frank P. Seth

 
 
Kama wewe ni msomaji wa biblia, utagundua kwamba katika hadithi maarufu za biblia, na ambazo mahubiri mengi sana yametaja, tangu zama za manabii na mitume wa zamani hata sasa, ni safari ya wana wa Israel Jangwani.
Pamoja na mambo MAGUMU mengi ya jangwani, hapo ndipo Mungu ALISEMA uso kwa uso na Musa, na hata wana wa Israel walisikia sauti ya Mungu kwa masikio ya damu na nyama.
 
Ni katika kipindi hiki cha kupita Jangwani, ambapo Mungu amesema na Musa kule mlimani, na kumpa amri 10. Ni kule jangwani ambapo vitabu vya Torati, ambavyo ni mwongozo wa taifa la Israel hadi leo viliandikiwa kutokana na mambo ambayo Mungu alizungumza. Kwenye safari za maisha kuna sehemu nyingi za kujifunza, lakini usikose darasa lako upitapo jangwani.
 
Je! Umegundua kwamba katika maisha yetu kuna vipindi vya kupita jangwani? Nyakati ambazo unaona kabisa mambo hayaendi (kifamilia, kazini, kwenye ndoa, shuleni, nk). Jangwani ni mahali pa kupungukiwa na kiu; Ni mahali pa kero na misukosuko mingi, lakini, hapo ndipo kuna DARASA zuri la maisha yako. Hapo jangwani ndipo Mungu atasema na wewe kwa habari ya hatma yako. KOSA la kuondoka JANGWANI isivyosahihi litakugharimu HATMA ya maisha yako.
 
Sasa angalia jambo hili. Bwana Yesu alipopelekwa kujaribiwa, Roho alichagua kumpekeka NYIKANI pia. BWANA Alikaa siku 40 usiku na mchana bila kula wala kunywa, hapo ni jangwani. Zingatia jambo hili, ukiwa jangwani, ni mahali ambapo pia utaisikia sauti ya Ibilisi kwa DHAHIRI sana. Kila mara sauti hii itakuwa ikikutaka KUONDOKA jangwani (to find a comfort zone) kwa namna ya KUMKOSEA Mungu. Ndio maana Ibilisi alikuja na vitu vingi vya kuvutia, ili kuondoa USIKIVU wa Yesu kwa Mungu wake (Neno). Kila adui alipotaka kumhamisha katika KUSUDI la Mungu, Yesu alisema, "imeandikwa" kisha Alikataa vishawishi vya Adui.
 
Kukaa katika Neno la Mungu, ndio siri ya ushindi wako upitapo jangwani. Kumbuka siku zote, jangwa halitadumu siku zote, ni njiani tu, lakini hapo ndipo utasikia suati ya Mungu pia, Akikwambia mambo mengi ya hatma ya maisha yako. Hapo ndipo utajifunza mambo na kumsikia Mungu akijibu yale maombi yako ya siku nyingi. Kaa hapo jangwani usiondoke. Zidi kumkaribia Mungu kwa KUFUNGA na KUOMBA, kaa jangwani kwa saburi na utulivu kabisa, naam, bila KUNUNG'UNIKA. Ushindi wako ni mkubwa ukivuka hapo.
 
Usishangae wakati ukiuwa PEKEYAKO jangwani, ndipo ADUI hukujia na kukuonesha UZURI wa TUNDA, kama alivyofanya kwa mama yetu Hawa pale kwenye bustani ya Eden (alipokuwa peke yake). Zingatia jambo hili, kweli tunda lafaa kwa chakula, kweli tunda linapendeza macho, kweli tunda linavutia sana; lakini kumbuka hapo unashughulika na HATMA yako. Kweli unaweza KUEPUKA jangwa lako kwa kufanya mambo mengi ya kukupa AHUENI (kivuli kidogo), lakini jiulize, Je! Ndivyo Neno la Mungu limekuagiza hivyo? Kama jibu ni HAPANA, jua Adui anataka KUKATILIA MBALI hatma yako kama alivyofanya kwa mama yetu Hawa.
 
Utulivu wako JANGWANi utakusaidia kusikia SAUTI ya Mungu kwa namna ambavyo hujawahi kusikia ukiwa katika madarasa mengine. Darasa la jangwani ni la muhimu; tulia hapo usiondoke hadi utakapopita, maana, hapo sio mahali pa kudumu sana japo kuna maumivu mengi. Vumilia tena kidogo.
 
Frank P. SethKAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni