Jumatatu, 21 Desemba 2015

JUA HISTORIA YA SIKUKUU KUBWA YA CHRISTMAS NA SHAMLASHAMLA ZAKE

Kwa muda mrefu sikukuu ya krismasi imejulikana kuwa na sikukuu kubwa sana na inaweza kuwa ya kwanza kusherehekewa na watu wengi duniani na dini karibu zote. sikukuu hii ambayo hukumbuka kuzaliwa kwa Yesu kristo hapa duniani. katika nchi zilizoendelea huwa wanaanza shamla shamla za sikuu hii tangu mwezi wa November maduka nyuma ofisi hupambwa na kuanza kuuza vitu vyingi vinavyohusiana na sikukuu hii kubwa Duniani.
 
kumekuwa na utata wa mambo mengi ikiwa uhusika wa father Chrismas, miti ya michrismas pamoja na taa za vimweku mavazi mekundu na meupe. nataka leo tuangalie uhusika wa baba christmas mwenye ndevu nyeupe rangi ya uwaridi mashavuni na anavaa nguo nyekundu.hii imetokana na tangazo la biashara lililobuniwa na kampuni moja ya vinywaji baridihuko america ya kasikazini kati ya mwaka 1931. katika miaka ya 1950 baathi ya watu huko brazil walijaribu kubadili cheo cha baba chrismass na kumpa mtu wa taifa lao waliyemwita babu wa India. matokeo yalikuwaje? si kuwa tu babu chrismas alimshida babu wa India bali imeendelea kutumika kama nembo kubwa ya kibiashara kupita hata wale wanaoadhimisha kuzaliwa kwa Yesu.

Historia ya kuanza kwa sikukuu ya Chrismasi
Katika karne 2 za mwanzo tangu kuzaliwa kwa Yesu, hapo ulipoaanza ukristo, watu wengi hawakuserehekea siku za kuzaliwa wala kufa kwa wafia imani au hata ya Yesu mwenyewe. kinasema Encyclopedia Britannica kwa nini? wakristo waliona kusherehekea siku ya kuzaliwa ni mazoea ya kipagani linalopaswa kuepukwa,  licha ya msimamo wa wakristo wa nyakati hizo ya kupinga mazoea ya kusheherekea siku ya kuzaliwa, kanisa katoriki ndilo lilianza kusheherekea chrismas katika karne ya nne. kipindi hicho kanisa lilitaka kujiimalisha na kupunguza umaarufu wa sikuu za dini za kipagani za roma ambazo zilikuwa zinafanyika katika msimu wa baridi, jua linapokuwa upande wa kasikazini wa Dunia kila mwaka, kuanzia December 17 mpaka Januali 1.
 
Waroma wengi walisherehekea pamoja walicheza, walishiriki katika matamasha, magwaride, na sherehe nyingine walizokuwa wakiabudu miiungu yao, kitabu cha chrismas America kilichoandikwa na Penne L. Restand kinasema ilipofika December 25 waroma walisherehekea kuzaliwa kwa jua lisiloweza kushindwa. hivyo ilibidi kanisa kuwa na ushawishi mkubwa wa kuwashawishi waroma kugeuza siku hiyo ya kuzaliwa jua iwe ni siku ya kuzaliwa Yesu, na ilifanyika ili kuuondoa ibada za kipagani ijapo waroma waliweza kufurahia vitu vyote au michezo yote waliokuwa wakifanya katika msimu wa baridi. kitabu cha Santa Claus, a Biography kilichoandikwa na Gerry Bowler kwa hakika waroma waliendelea kusherehekea hiyo sikuu mpya kama walivyo zoea kufanya zamani.

Biblia Inasema Nini Kuhusu Krismasi?
Biblia haitaji tarehe ambayo Yesu alizaliwa, wala haisemi kwamba tusherehekee siku yake ya kuzaliwa. Kama vile kitabu McClintock and Strong’s Cyclopedia kinavyosema: “Mwadhimisho wa Krismasi haukuagizwa na Mungu, wala hautokani na AG [Agano Jipya].”Kinyume cha hilo, historia ya Krismasi inafunua kwamba inatokana na sherehe za kipagani..
 
Historia ya desturi za Krismasi
  1. Kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Yesu: “Wakristo wa karne ya kwanza hawakusherehekea siku ya kuzaliwa kwa [Yesu] kwa sababu waliiona sherehe ya kuzaliwa kwa mtu yeyote kuwa desturi ya wapagani.”—The World Book Encyclopedia.
  2. Desemba 25: Hakuna uthibitisho wowote kwamba Yesu alizaliwa tarehe hiyo. Huenda viongozi wa Kanisa walichagua tarehe hiyo ili ipatane na sherehe za kipagani zilizofanywa wakati wa au karibu na majira ya baridi kali.
  3. Kupeana zawadi, sherehe, karamu: Kitabu The Encyclopedia Americana kinasema: “Desturi nyingi za kujifurahisha zinazofuatwa wakati wa Krismasi zinatokana na Saturnalia, sherehe ya Waroma iliyofanywa katikati ya mwezi wa Desemba. Kwa mfano, karamu zenye madoido mengi, kupeana zawadi, na kuwasha mishumaa zilitokana na sherehe hii.” Kitabu Encyclopædia Britannica kinasema kwamba “hakuna kazi wala biashara iliyofanywa” wakati wa Saturnalia.
  4. Taa za Krismasi: Kitabu The Encyclopedia of Religion kinasema kwamba wazungu walirembesha nyumba zao kwa “taa na mimea ya kijani-kibichi ya kila aina” ili kusherehekea majira ya baridi kali na ili kuwazuia roho waovu.
  5. Mlimbo, mholi: Kwa kawaida mimea hiyo hutumiwa kama mapambo wakati wa Krismasi. “Wadruidi (makasisi Waselti) walisema kwamba mlimbo ulikuwa na nguvu za kimuujiza. Mholi, mmea ambao haunyauki, uliabudiwa kama ahadi ya kurudi kwa jua.”—The Encyclopedia Americana.
  6. Mti wa Krismasi: “Kuabudu miti lilikuwa jambo la kawaida kati ya wapagani wa Ulaya na waliendelea na zoea hilo baada ya kuwa Wakristo.” Kati ya mazoea yaliyobaki ya ibada hiyo ya miti ni desturi ya “kuweka mti wa Krismasi kwenye mwingilio au ndani ya nyumba wakati wa sikukuu zinazofanywa katikati ya majira ya baridi kali.”—Encyclopædia Britannica.
Hiyo ndiyo historia ya chrismasi na vitu vyake vyote na siku za leo imekuwa ni siku ya kibiashara zaidi na kupeanza zawadi na ndo maana ikaanzishwa na boxing day yani siku ya kufungua mabox ya zawadi watu walizopeana wakati wa Christmasi. Blog tunakutakia wewe msomaji wetu Merry Christmas na heri ya mwaka mpya wa 2016.
 

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Hakuna maoni: