Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri la Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa |
Maaskofu wa Jukwaa la Wakristo ambao ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Kikristo (CCT), Askofu Dk Alex Malasusa, Mwenyekiti wa Baraza la
Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Tarcicius Ngalalekumtwa na
Mwenyekiti wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (CPCT) Askofu Daniel Awet,
kwa sauti moja wamewataka waumini wao kujiandikisha kwa wingi katika
Daftari la Wapigakura, kuisoma vyema Katiba Inayopendekezwa na hatimaye
kuikataa kwa kuipigia kura ya ‘hapana.’
Sababu kuu za kuwahamasisha waumini wao na Watanzania kuikataa Katiba
Pendekezwa ni mbili. Mosi ni kulazimisha kura ya maoni ya katiba mpya
kufanyika bila maandalizi ya kutosha, yakiwamo maridhiano ambayo
yameligawa Taifa katika vipande vipande.
Pili viongozi waandamizi wa Serikali ya CCM kuupigia debe muswada wa Mahakama ya Kadhi.
Tamko hili nyeti ambalo limesambaa katika makanisa mengi iwapo litasomwa
kwa waumini wote na kuhamasishwa na mapadri, wachungaji na wainjilisti
basi unaweza ukawa ndiyo mwisho wa Katiba Inayopendekezwa kupigiwa kura
Aprili 30 mwaka huu.
Viongozi wa jukwaa hilo wana wajibu wa kushiriki kikamilifu katika zoezi
la kuandika Katiba Mpya ambalo linawahusu waumini wao pia. Katiba siyo
suala la siasa, bali ni la Watanzania wote.
Itakumbukwa kuwa CCM ilitumia mabavu na fedha nyingi katika kusimamia
mijadala ya Katiba Mpya, wakapitisha Katiba kwa kutumia vyombo vya dola.
Hofu ya kukataliwa kwa Katiba Mpya kumeifanya Serikali ya CCM ivunje
kabisa makubaliano na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kwamba Kura ya
Maoni ingesitishwa hadi baada ya uchaguzi 2016.
Hata hivyo, kwa sababu ya hofu ya kuanguka madarakani, CCM imeamua
iendelee kulazimisha kura ya maoni kwa kutumia mabavu na hivyo
kuwaburuza wananchi.
Matokeo yake Serikali ya CCM inafanya kila hila ili Daftari la
Wapigakura lisiboreshwe ili waweze kuchota kura vizuri kiholela holela.
Nionavyo hofu kuu ni Katiba hii kuja kukataliwa na umma, hivi Rais
Kikwete ameona heri aendelee kuisukuma walao ikubalike na umma. Lakini
ukweli ni kwamba katiba hii imekataliwa na wananchi wengi pia hata na
Mungu kwa sababu ‘sauti ya wengi ni sauti ya Mungu’.
Sababu nyingine kubwa ya kukataliwa na wananchi wakiwamo maaskofu ni
Katiba Inayopendekezwa kulenga kulinda masilahi ya watu wachache ndani
ya chama na Serikali ya CCM.
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni