Jumatatu, 11 Agosti 2014

MASHIRIKA MBALIMBALI YAOMBWA KUDHAMINI PIA MATAMASHA YA MUZIKI WA INJILI


01
Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama kulia na mwimbaji wa muziki wa injili Bonny Mwaiteje katikati na Mwimbaji Chengula kushoto wakati wa tamasha la uzinduzi wa Albam ya Shikilia Pindo la Yesu uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo akisindikizwa na waimbaji malimbali wa muziki huo akiwemo Ephraimu Sekereti kutoka nchini Zambia, Albam hiyo imezinduliwa na Meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula ambaye alimwwakilisha Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba, Akizungumza katika uzinduzi huo wakati akitoa ujumbe aliouwakilsha katika uzinduzi huo kutoka kwa Mh. Januari Makamba Mabula ameuelezea ujumbe huo kuwa Serikali inafanya kila liwezekanalo kushawishi makampuni ili yadhamini pia matamasha ya muziki wa injili ka ambavyo yamekuwa yakiafuturisha vikundi na waumini mbalimbali wakati wa mfungo wa ramadhan, kwakuwa muziki wa injili pia unaeneza amani na upendo kwa jamii ya watanzania, Hii itasaidia kupunguza ghara za uandaaji jambo ambalo kwa namna moja au nyingine litakuwa linarahisisha uandaaji wa matamasha hayo ambayo yamekuwa ni chachu ya watu kuachana na maovu na kuwa watu wema katika jamii
7
Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba wakati wa tamasha hilo kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo
1
Meya wa jiji la Mwanza ya Mhe.Stanslaus Mabula akinyanyua juu albam za mwimbaji Rose Muhando wakati alipozindua albam hiyo mkoani Mwanza leo kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
2
Meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula kulia akiwa amesimama na Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion wakati wa uzinduzi huo kutoa kulia ni waimbaji Chengula Bony Mwaiteje , Tumaini Njole na Rose Muhando.
3
Mmoja wa waratibu wa uzinduzi huo Bw. Hudson Kampga akizunguza katika uzinduzi huo kwa niaba ya Mkurugenzi Alex Msama.
4
Meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion wa Msama Alex, kulia anayefurahia ni mwimbaji Rose Muhando.
5
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bwa. Alex Msama akigawa albam ya Rose Muhando kwa Mh. Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula na Maaskofu waliohudhuria kwenye uzinduzi huo.
6
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza machache katika uzinduzi huo.
8
Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akikamua na wacheza shoo wake wakati wa tamasha hilo kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo
9
Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akipagawisha mashabiki wake wakati wa tamasha hilo kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo
10
Umati wa maelfu ya wa waliohudhuria katika uzinduzi hu wakinyanyua mikono juu juu.
11 12 13
Mwimbaji Bony Mwaiteje akifanya vitu vya sarakasi jukwaani.
14
Miwmbaji wa kimataifa kutoka zambia Ephraim Sekereti ni mmoja wa waimbaji waliokonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa injili.
15
Noa Vicoria Singers wakafanya vitu vyao.
16
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bwa. Alex Msama akifanya vitu vyake na MC Mwakipesile.
17
Miwmbaji Tumaini Njole akafanya mambo yake pia katika uzinduzi huo
18
Ni Full Burudani ya muziki wa injili.
19
Miwmbaji Tumaini Njole akiimba kwa hisia kali katika uzinduzi huo

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 4777775 au Whatup, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Hakuna maoni: