Jumatatu, 28 Julai 2014

UNABII ULIOTOLEWA NA REV BEN KUMHUSU MWIMBAJI WA NYIMBO ZA HIPHOP GAZUKO WATIMIA


Ni mwezi sasa umepita ambapo mwimbaji wa nyimbo za Gospel Hiphop anayejulikana kwa jina la Gazuko alipohudhulia katika ibada zinazofanyika katika kanisa la Assaph Ministries International Buguruni Rozana. katika ibada hiyo Mtumishi wa Mungu Assaph Benjamini alitoa unabii kumhusu mwimbaji huyo na kusema Bwana atamwinua na atakuwa mumbaji wa kimataifa na huduma yake ni kubwa.
Christina Shusho na Rose Mhando ambao nao wako kwenye tuzo hizo

 baada ya mwezi mumbaji huyo alichaguliwa kuwania katika tuzo ya waimbaji wa hiphop africa ambazo zinaandaliwa na AGMA ambao wako UK. Tulipopata taarifa tuliwasiliana nae kuhusu hilo alisema amefurahi sana hadi anatokwa na machozi hakuwa amewaza wala kutegemea kuwa mmoja wa watu wa kuwania tuzo kama hizo.

http://3.bp.blogspot.com/-eO5Kll23l14/U89pfS9F6DI/AAAAAAAF5Cs/TqmgjZo2Yu0/s1600/unnamed+(8).jpg
Mwimbaji Gazuko aliyetolewa unabii na kutimia

AGMA mwaka huu watatoa tuzo kwa mwaka wa 5 na miaka ya nyuma waimbaji wa TZ ambao wamewahi kuwania tuzo hizo ni Christina shusho, Martha Mwaipaja, na mwaka huu ni Chistina shusho, Rose Mhando na Gazuko.
Assaph Benjamini akihudumu
Tunamshukuru Mungu awezeshae mtumishi wake kusema vitu ambavyo vinakuja, na kuthibitishwa kwa kutokea katika katika uharisia, Tunawakaribisa katika ibada zetu ili uje ukutane na nguvu za Mungu aliye juu. unaweza kuwasiliana na kanisa letu kwa no 0782 499991

Kwa hisani ya Assaph Ministries International 

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 4777775 au Whatup, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni