Ijumaa, 2 Mei 2014

BAADA YA KUIGIZA SANA MAINDA SASA KUIMBA NYIMBO ZA INJILI.


Msanii nyota wa filamu Tanzania Ruth Suka 'Mainda'
Msanii maarufu wa filamu nchini Tanzania Ruth Suka maarufu kama Mainda, ameamua kuimba nyimbo za injili ili kumtukuza BWANA YESU aliyemuokoa. Mainda ambaye kwa sasa ameokoka baada ya kumpokea BWANA YESU kama BWANA na MWOKOZI wa maisha yake amedhanilia kufanya vizuri katika kumwimbia MUNGU. 

Mainda ambaye kabla hajaokoka alikuwa akiitwa Mwanaidi Suka  na sasa anaitwa Ruth Suka anafurahia kuwa mteule wa BWANA YESU.

MSANII AMBAYE amepitia kwenye mambo mengi ya kidunia lakini anamshukuru BWANA YESU kwa kumwokoa.

Amesema ataimba nyimbo za dini ili kumtukuza MUNGU maana amedhamilia kumtukuza MUNGU.

Mainda anasema ''Vijana siku zote tuna nguvu, tuna muda wa kutosha, hivyo tunapaswa kumtumikia MUNGU, sio mpaka tuchoke, tuzeeke na tufanye dhambi, tukifika Omega(Mwisho) ndipo tunamkumbuka MUNGU.''

Anaendelea kusema '' Nitaimba kwaya tena sauti ta tatu(3), subirini muone ujio wangu mpya, nimeamua kumtukuza MUNGU aliyeziumba mbingu na nchi.''


HAKIKA UMELICHAGUA FUNGU JEMA AMBALO HAKUNA AWEZAE KUKUONDOLEA.

Mainda katika pozi.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni