Jumatano, 15 Januari 2014

USHUHUDA WA MUISLAMU ALIYEOKOKA ALIKUWA NA MAJINI YA CHUMA ULETE SASA NI MWINJILISTI, COSMAS JUMA HAMIS


 Mimi Mwinjilisti Cosmas Juma Hamis nimezaliwa mwaka 1975 Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora nikiwa ni mtoto wa kwanza wa mama Mwamini Said Ntembela na Baba Shekh Juma Hamis Mdaki, Baba akiwa msumbwa na mkazi wa Wilaya mpya ya Kaliua na Mama mwenyeji wa tarafa ya Usoke wilaya  Urambo akiwa ni wa  kabila la watusi wazawa wa mkoa Tabora. Mwaka 1985 nikiwa na umri wa miaka 10 nilianza elimu ya msingi katika shule ya msingi mapinduzi iliyoko tarafa ya Usoke wilaya ya Urambo mkoa wa Tabora pamoja na kuanza elimu ya msingi pia nilijiunga na shule ya kiislamu (yaani nilijiunga na shule ya kiislamu (madrasat) kusoma elimu ya kiislamu na hii ilitokana na Baba yangu na Mama yangu kuwa ni waislamu hivyo nilipelekwa katika madrtasa hiyo ili nisome uislam ambao ndio dini ya wazazi wangu na ndugu zangu wote.

 Nikiwa ni mzaliwa wa kwanza kati ya watoto 12 katika tumbo la mama yangu Mwamini Said Ntembela ambapo mimi kwa Baba tumezaliwa watoto 2 mimi na dada yangu Johari Juma Hamis na mimi nikiitwa wakati ule kwa jina la Hamisi Juma Mdaki mama yangu aliachana na Baba yangu shekh Juma Hamisi Mdaki tukiwa tumezaliwa watoto wawili na baada ya kuachana Mama na Baba ambapo ilikuwa mwaka 1979 mimi nikiwa na umri wa miaka minne na dada yangu akiwa na miaka miwili tukaenda kuishi kwao na Mama ambapo ni tarafa ya Usoke wilaya ya Urambo kwani hapo mwanzo tulikuwa tukiishi mwanza na kaliua baada ya kuishi pale usoke mama yangu aliolewa nma mume mwingine ambae anaitwa Shabani bakari amri moja. Waliishi na mume huyo ambapo kisheria alikuwa mume halali kutokana na mafundisho ya dini ya kiislamu kwa kuwa alishapewa taraka, hivyo waliendelea kuzaa watoto ambapo jumla walifika watoto kumi na hivyo kufanya idadi ya watoto wa Mama huyo kufikia 12 na mimi nikiwa mkubwa wa wote.

 Baada ya kuanza Elimu ya dini ya kiislamu sambamba na elimu ya msingi niliitimu elimu ya msingi mwaka 1991 na baada ya kutokuchaguliwa na elimu ya secondary mwaka 1992 nilichukuliwa na Baba yangu Shekh Juma Hamis Mdaki na kunipeleka alipokuwa akiishi yeye ambapo ni kijiji cha Igagala No 3 na kuniandikisha katika shule ya msingi kamusekwa iliyopo kijiji cha Igagala No 2 ili niludie masomo ya elimu ya  msingi ambapo yeye kwa wakati huo alikuwa ni shekh wa msikiti wa Igagala No 3 pamoja na mwalimu wa madrasat ya pale msikitini hivyo na mimi niliendelea na masomo ya elimu ya dini yeye Baba yangu akiwa mwalimu wetu nilisoma kwa mwaka mmoja na kuhamia mjini, wakati huo ikiwa bado ni tarafa hivyo nikiwa kaliua nilijiunga na madrasat ya kiislamu pale kaliua kwa mwalimu mwingine ambae aliitwa shehe Omari mimi na wenzangu tuliendelea na masomo pale mpaka mwaka 1993. Mwaka 1994 niliondoka kwa shekh huyo ambae kwa sasa ni marehemu na kurudi Usoke baada ya kushindikana kupata nafasi ya kuendelea na masomo ya sekondari. baada ya kufika Usoke iliyoko wilaya ya Urambo niliendelea na masomo ya dini ya kiislamu kwa shekh aitwaye Juma Almas mpaka mwaka 1995 nikaondoka kwenda mwanza nikiwa nimeshakuwa mwelewa katika dini yangu ya kiislamu nikaendelea na masomo kwa mashekh mbalimbali akiwemo shekh Juma Hamis Sungusungu ambae alikuwa akitoa darasa na masomo katika msikiti wa Mabatini uliopo katika kota za mapolisi pale Mabatini Mwaza. Mwaka 1999 nilihama Mwanza na kuhamia mkoani Shinyanga wakati huo nilikuwa na miaka 24 nilipofika Shinyanga niliingia katika chuo cha kiislamu kiitwacho MADRASAT NURANIA chini ya mwalimu Masoud na walimu wengine nikaendelea na Uislam nikiwa Muumini mzuri wa imani ya dini ya kiislamu. 

Niliendelea na masomo hapo ambapo chuo hicho kilikuwa katika msikiti wa Ngokolo matope chini ya Imamu alieitwa Maalimu Selfu. Mwaka 2000 niliondoka shinyanga wakati huo nikiwa tayari na uelewa wa kutosha juu ya dini yangu na tayari ninao uwezo wa kufundisha na wengine nilielekea jijini Dar es Salaam na nikiwa Dar nilifikia kurasini kwa Shekh Juma Kassim Ngupepe yeye akiwa mwenye asili ya Rufiji na Mafia nikiwa pale nilijifunza Elimu nya unajimu au Tiba za Kiarabu nikiwa naendelea kuishi hapo na wakati huo nilikuwa na majini ya Uganga ambayo yaliniongoza katika mambo yangu ya kimaisha nilifanya kazi pale kwa shekh huyo kwa muda wa mwaka mmoja nasikuchelewa kuanza kufanya kazi zangu binafsi za uganga wa majini kwani tayari nilishapata baraka toka kwa shekh wangu na ndipo nikafungua na mimi ofisi yangu ya uganga maeneo hayohayo ya kurasini, tiba ya majini na mimi binafsi nilikuwa namiliki majini. 

Mwaka 2002 niliendelea na kazi hiyo huku nikienda kwa mashehe mbalimbali kujiongezea elimu zaidi juu ya majini na tabia zao(yaani elimudunia) watu wengi walikuja kwangu wakati huo nilikuwa nimekwishaoa na kuishi na mwanamke ambaye yeye asili yake alikuwa mkristo maana majini yangu yalinitaka nioe mwanamke ambaye ni mkristo kwa maana kwamba ipo siku na yeye huyo mwanamke atabadili dini na kuwa muislam kama mimi na hayo majini. Baada ya kufanya kazi hiyo ikiwa pamoja na kuwafundisha wengine mwaka 2003 majini yalinitaka niende kwa mganga ili nikajiongezee karama ya kipato wakati huo nikiwa nina mtoto mmoja niliyezaa na mwanamke huyo niliyekuwa ninaishi naye. 

Niliondoka na kuelekea Mwanza na pale nilikutana na rafiki yangu na kunipeleka kwa mganga mkoani Shinyanga maeneo ya Bariadi kijiji cha Bunamalambugani nikakaa kwa mganga kwa miezi mitatu(3) nikapewa majini ya chuma ulete nikarudi Dar, nikiwa Dar ndani ya muda mfupi mambo yalianza kwenda vizuri sana kwani nilitumia chuma ulete kwa kujiongezea kipato nikaweza kununua gari mwaka huo na kupanga nyumba nzuri na ya kisasa nikaachana na kazi ya uganga, chuma ulete niliitumia kwa watu wasio mkubali Yesu pamoja na kuwa walikuwa wakristo (yaani wasiookoka) hivyo ndani ya mwaka mwingine niliweza kujenga nyumba kwetu Tabora na kuishi maisha ya uhakika sikuwa na shida, ila chuma ulete nilipewa sharti nitumie kwa watu walio wakristo tu tena kwa wale ambao hawajaokoka kwani niliambiwa nikitumia kwa wale waliyookoka haitafanya kazi itazidiwa nguvu na walokole maana wao wanauwezo zaidi ya chuma ulete,  basi nilisafiri mikoa mingi hapa nchini na hiyo chuma ulete nikiwachukulia watu fedha bila kunigundua.

 Baada ya mafanikio mganga aliniagiza niende kule kwake, Bariadi ili akanielekeze mambo muhimu wakati ule maisha yangu yalikuwa mazuri sana! kwani niliweza kuwasaidia ndugu zangu, nikiwa kwa mganga mwaka huo wa 2004 mganga akanitaka nimtoe  mwanangu wa kwanza afe (yaani nimtoe sadaka mali iweze kukaa na kutulia) baada ya kusema hivyo mganga mimi nilikataa akanifukuza na baada ya kuondoka kwa mganga huyo mali ziliteketea ikiwa pamoja na magari nyumba na mwisho nikakubali, ila wakati na mpeleka yule mtoto kwa mganga kumtoa sadaka nikakuta mganga amekufa mwaka huo ulikua mwaka 2005,  mwishoni mwaka 2006 nikiwa nimeshafilisika na wakati huo nikiwa na watoto watatu nikalukwa akili ndugu zangu wamenipeleka kwa waganga wengi bila mafanikio mwishowe ndugu wakanitelekeza bila msaada, mke wangu akaenda kwao na mali chache ndugu waliziuza ili kunitibisha kwa waganga bila mafanikio niliendelea kuteseka na nilipokutana na YESU KRISTO kwa kufanyiwa maombi hiyo ilikuwa mwaka 2008 Magomeni kanisa Anglikana,a mbapo siku ya jumanne nilifika pale nikakutana na mtumishi wa Mungu haitwae Henry Ramadhani ambaye alinifanyia maombi nikapona kabisa majini yote yakaondoka, mwaka huo huo 2008 nikabatizwa hapo magomeni Angalikana  na chini ya mchungaji Elisha Tendwa ambapo ilikuwa tarehe 11- 5 -2008 nilibatizwa mimi Hamis Juma Hamisi nakupewa jina la Cosmas Juma Hamis nilisimamiwa ubatizo na huyo mzee Henry Ramadhani ambaye aliniombea nakupona nilibatizwa mimi na wanangu siku hiyo hiyo ambao mmoja anaitwa Suzana Cosmas Juma mwingine Martin Cosmas Juma na yule ambaye alitaka mganga amchukue kichawi ili niendelee kumiliki mali alibatizwa Zanzibar kwa jina la Marrygoreth Cosmas Juma.

 Baada ya ubatizo niliendelea na mafundisho juu ya imani mpya ya kristo nikapata kipaimara kanisa la Angalikani mbezi lous chini ya mchumngaji Paul Mtweve na baada ya kipa imara mzee Ramadhani aliongea na wachungaji ambapo nilipelekwa kwenda kusomea kozi ya utumishi wakanisani chuo cha Anglikana morogoro kiitwacho kwa jina la MOROGORO BIBLE COLLEGE nilisoma mpaka mwaka 2010 baaada ya kumaliza masomo nikaludi Dar, nikiwa Dar nilipangiwa kituo cha kazi kama mwijilisti kanisani, kanisa la Anglikana na Roho Mtakatifu chini ya mchungaji Johnson Lameck ambapo mwaka mmoja nilipata pigo kubwa sana kifamilia la kufiwa nikarudi Tabora, nikiwa Tabora niliendelea kumtumikia mungu ambapo pamoja na ndugu kuwa waislam na, mimi ni Mkristo nimeona njia ya mimi kwenda mbinguni nikimfuata Yesu Kristo yeye ndiye njia, kwa sasa napatikana katika kanisa la Anglikana Kakola Kahama dayosisi ya Tabora nikiwa ndie Mwinjilisti wa kanisa hilo lakini pia ni mwenyekiti wa Kamati ya uinjilisti chini ya mchungaji Israel Baada, lengo langu ni kuendelea na masomo zaidi kwani namshukuru mungu kwa kuisoma elimu ya kiislam kwa miaka 25 hivyo naelewa dini hiyo vilivyo kwanza nikiwa nimeisoma na pia kukulia katika familia ya kisomi ya dini hiyo na wenye kufuata maadili yote kiislam, kiu yangu kwa sasa pamoja nakutumika kwenye makanisa mengi nikifundisha semina mbalimbali, endapo na nitapata mfadhili wa kuniendeleza kimasomo zaidi kwa upande Ukristo nitafurahi zaidi na muda huu ambao niko Kahama Shinyanga nimeendelea kutumika nikiwa na mwinjilisti wa kanisa la Angalikana katika parishi ya Kakola, natumika katika kutoa ushuhuda namna nilivyo zama katika uchawi wa kimajini baada ya kukaa nayo na jinsi ambavyo Babu yangu alivyonilisisha uchawi na namna nilivyo achana na hayo yote na kumupokea yesu kristo, endapo mtu au kanisa au kikundi chochote cha kikristo kikinihitaji kwa ajili ya ushuhuda wa nguvu za Yesu zilizo niokoa mimi na wanangu napatikana kwa

No:-  0789 351 590 ,0714 351 590
au Barua pepe
amostelesphory@gmail.com
Asante Mungu Awabariki sana
Mimi Ev Cosmas Juma
Mwislam niliyeokoka.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Hakuna maoni: