Jumatano, 6 Novemba 2013

MTOTO ALIYEKUWA ANAIBA WATOTO WAGANGA KICHAWI NA KUWAUA AOKOKA NA KULEZEA

Jisomee ushuhuda huu ulioandaliwa na Mary Mosha kutoka kanisa la Ufufuo na Uzima Arusha.

Nyumba ya ufufuo na uzima Arusha ikiendelea kuona matendo makuu ya Mungu, ni katika ibada ya jumatano ikiwa ni wiki ya "KUVUKA" Mtoto huyu ashuhudia jinsi alivyokuwa akitumikishwa na bibi wa jirani kufanya uchawi, alikuwa akitumika kuchukua na kuua watoto wachanga pamoja na vijana (wanaume) wengine walitumika kama vitoweo na wengine aliwapeleka kwa mfalme wao huko kuzimu. Alikuwa akitumia vifaa kama pete na sindano katika kazi hiyo ya kuchukua watoto wachanga waliozaliwa baada tu ya mama kujifungua, Pete ilimsaidia katika kazi zake hizo pale alipokuwa akitaka kwenda kuchukua watoto wachanga mahospitalini aliiminya na kujiminya utosi wake ndipo anapotokea ukutani na hawezi kuonekana, na SINDANO kama zinavyoonekana hapo katika picha zilitumika kuwateka wanaume na baada ya hapo wanaume hao humfuata na huwabadilisha kuwa kipepeo kama yeye na ndipo huwapeleka kuzimu, namnukuu "(sindano moja ilikuwa ina sumu ya mapenzi) ambayo ndiyo inayotumika kuwateka wanaume)", cha kusikitisha zaidi kama uonavyo pichani bibi huyo aliyekuwa akimtumikisha alifanikiwa kumuweka BINTI huyu alama ya NYOTA, NYOKA, pamoja na NAMBA 8 katika paja lake. Zaidi ya yote tunamrudishia MUNGU sifa kwa sababu amekubali kuokoka na kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yake.


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni