Jumatatu, 21 Oktoba 2013

MWANAMZIKI MAARUFU MAREKANI AOKOKA NI JA RULEMwigizaji na mwanamuziki wa miondoko ya kufokafoka Ja Rule wa nchini Marekani ameweka bayana namna alivyompokea Yesu, wakati akifanyiwa mahojiano katika kipindi cha Huff post live, ambapo ameweka bayana kwamba aliokoka katika kanisa la Hillsong New york ambako amesema wanapokea mtu jinsi alivyo bila kumuhukumu, akieleza zaidi Ja Rule ambaye jina lake kamili ni Jeffrey Atkins amesema alishangaa kuona kanisa ndani ya Club(ni kawaida ya Hillsong kukodi kumbi kubwa na kufanya ibada siku za jumapili) kukiwa na mataa kama ya disko, zaidi alishangazwa kuona mchungaji kavaa suruali ya jeans pamoja na fulana hali iliyomfanya kujisikia karibu zaidi na hatimaye kuokoka.

Mwigizaji huyo ameigiza filamu mpya ya Kikristo ambayo kuna mkono wa askofu T.D Jakes iitwayo "I'm in Love with A church Girl" filamu ambayo ndio iliyompelekea mwimbaji huyo kujikuta Hillsong na kuokoka, awali mwimbaji huyo alikuwa muumini wa kanisa la Mashahidi wa Jehova ama waite Jehova witness, ambapo kwasasa kanisa lake ni Hillsong New York, na jumapili ya jana kanisa hilo limefungua tawi katika mji wa Los Angeles ambako inaaminika itawavuta waimbaji na waigizaji wengi zaidi kwa Yesu.

                                                 Angalia video hii kuanzia dakika ya 14

                                 

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni