Jumatano, 16 Oktoba 2013

MCHAWI AJISALIMISHA KWA YESU KANISANI TAG MAGOMENIHaya ndio yaliyotokea Jumapili katika Kanisa la TAG MAGOMENI MIKUMI KITUONI. Ni muendelezo wa kampeni ya USHUHHDIAJI WA SHABAHA. Kijana aliyekuwa akitumikishwa na shetani katika mambo ya kichawi AOKOKA NA KUKABIDHI
SANDUKU ZIMA LENYE VIFAA VYA KICHAWI ILI LICHOMWE MOTO.

Kijana huyu ambaye ni dereva wa bodaboda na ni mkazi wa Magomeni Mapipa aliyeamua kwa hiari yake kuokoka wakati wa Ibada kuu ya Jumapili Kanisani,
baada ya Ibada alipokuwa na mazungumzo ofisini kwa Mch yeye na mama yake aliomba aleta vitu vyake vya kichawi ili vichomwe moto ......

tukio hilo lilipelekea kilio kikuu kwa mama yake mzazi maana hakuwa akijua kuwa mwanaye anajishughulisha na mambo ya kichawi .......

Kijana alieleza matumizi ya vifaa hivyo vya kichawi; ikiwemo na mvuto ki-biashara, mvuto wa ki-mapenzi na hata kuwadhulu wabaya wake

 ......WALIOSHUHUDIA TUKIO HILO WALISHIKWA NA MSHANGAO MKUU NA KUMTUKUZA MUNGU ...... Mch alimwombea rehema za Mungu kijana huyo na kuongoza shughuli nzima ya kuteketeza huo uchawi kwa MOTO WA PETROL na kisha kumshauri kijana jinsi ya kuuishi WOKOVU ..... Kijana na mama yake wote wapo Kanisani wakimtukuza MUNGU KWA MATENDO YAKE YA AJABU. "YESU KRISTO YU HAI !!!!!".

sanduku la kiuchawi


 

kijana akielezea matumizi ya vifaa vyake


watu wakishangaa vitu kutoka katika sanduku


mama mzazi wa kijana haamini kuona kijana wake ni mchawi

akifanyiwa maombi na Mch Kanemba


choma choma  sanduku na tunguli zake zikiteketea kwa moto


kijana akiwa ofisini na Mch

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni