Jumatatu, 7 Oktoba 2013

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA KATIKA LIVE RECORDING YA JOHN LISU

Ubora wa mandhari wa Live Recording pamoja na Itifaki ya Mtiririko wa waimbaji ndio uliosahaulisha machungu ya Maelfu ya Wakazi wa Jiji la Dar-es-Salaam, Morogoro, Pwani , Zanzibar na nchi jirani Kenya waliochelewa kuingia ndani ya ukumbi wa CCC Upanga kufuatia utaratibu mpya wa usalama wakati wa kuingia kwenye Live Recording ya “Uko Hapa” ya Mwanamuziki John Lisu.

Siku ya Jana katika Ukumbi wa CCC Upanga Mwanamuziki wa Injili John Leonard Lisu ameandika historia kwa mara nyingine kwa kurekodi albam ya pili ya DVD katika Ukumbi huo. Kabla ya John Lisu kupanda na Kuanza kurekodi watumishi wengine wa utangulizi walianza kazi ya kusafisha njia hiyo. Wanamuziki waliohudumu ni pamoja na Mbomby Johnson, Neema Gospel Kwaya, Pastor Paul Safari, Paul Clement na Abedinego Hango.

John Lisu alipanda round ya kwanza na kurekodi nyimbo 12 mfululizo ambapo katika nyimbo hizo 12 amemshirikisha mwanamuziki maarufu wa Kenya Timothy Kaberia, pia amemshirikisha Mwanamuziki bora wa Injili Barani Afrika katika Ukanda wa Africa Mashariki Christina Shusho. Katika Collable hilo la John Lisu na Christina Shusho lilikuwa la aina yake na kukonga nyoyo za watu. Mwanamuziki John Lisu alirudi tena na kumalizia kurekodi nyimbo 6 na kutengeneneza jumla ya nyimbo 18.


John Lisu akienda sawa Katika Event.
Muonekano wa Mbele
 Bomby Johnson akiwa Kikazi zaidi siku ya Jana
 Kikazi Zaidi siku Ya Jana
 Watu wakiwa wanaenda Sawa
 Pastor wa DPC Abel akiwa anafunguwa event kwa maombi
 John Lisu na Timoth Kaberia toka Kenya wakiendaa Sawa kwenye Collable
 Neema Gospel Kwaya wakienda sawa
 Pastor Paul Safari akishusha kitu "Tuko Salama"
 Backers Wakiwa wanaenda Sawa na pastor Safari
 Twende Kazi
 Mambo Yetu Yale Ya Milio Milio
 Paul Clement a Kitu Cha "Mpenzi wa Karibu"
 Katibu Mkuu wa TAG Pastor Ron Swai akifungua rasmi Live Recording ya Jo Lisu
 Mbele
 Ma Mc wa Event Godwin Gondwe kutoka ITV Ze Blogger kutoka Clouds Tv
 KIkazi Zaidi
 John Lisu akiwa anajiandaa Kupanda Jukwaani
 Mbioooo Zikaanza za Kwenda Jukwaani
 Ukiona hivi Ujue mambo ya Sebene
 Back Vocalist wakienda sawa
 John Lisu Ze Great
 Kikazi Zaidi
 Uncle Jimmy akiongoza Wadau kucheza
 Watu Peopleeeeee
 Full Shangwe
 Kikazi Zaidi Jana
 Hapana Chezea
 Huyu dada huyuuuuu 
 Arangemaaaaa
 Jana ilikuwa Kikazi Zaidiii
 Kila Mtu na Kazi Yake
 Kikwetu Kwetu
  GODWIN GONDWE Ndani Ya Uwepo
 Uweponi Mwake
 Bombi na Lisu
 Lukindo Jr akiwa Uweponi
 Kaberia Kikazi Zaidi
John Lisu na Timoth Kaberia wakiwa Kikazi zaidi
 
Mungu awabariki sana watu wote mliotoa muda wenu kuja siku ya jana na mlio ombea ibada hiyo kufanikiwa Mungu awabariki sana sana, Nawashukuru wote mliotoka mbali kuja kuhudhuria Mikoani na Waliotoka kenya na ZenjI Mungu awabariki sana Mmekuwa baraka sana, Naomba muendelee kuniombea Nawashukuru saaaana timu ya waimbaji na wanamuziki waliojitoa muda wao kwaajili ya kazi hii Mungu awazidishie sana na Kaberia na Christina Shusho, Na waimbaji wote mlio jitoa kuja kuja kuhudumu Pastor Safari Poul, Bomby Johnson, Poul Clement, Neema Gospel, Abednego, Mungu awabariki sana sana sana.

 KWA HISANI YA BWANA HARUSI MTARAJIWA SAMUEL SASALI

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni