Alhamisi, 29 Agosti 2013

ASKOFU MKUU DR MOSES KULOLA AFARIKI DUNIA


Taarifa ambazo zimetufikia hivi punde zinasema kuwa Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia leo asubuhi.
Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika  kutoka kwa watu wa ndani wa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam.

Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu.

Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi.tutaendelea kukufahamisha kwa kadri ambavyo taarifa zitakuwa zikitufikia.Kufahamu historia ya maisha ya Hayati Askofu Dr. Moses Kulola ingia hapa.

BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe. 

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni