Jumanne, 26 Machi 2013

WACHUNGAJI WA KIPENDEKOSTE DAR WAVUNJA UKIMYA. WASEMA NA AJULIKANE MUNGU WA ELIA, WAITISHA MAOMBI YA SIKU TATU KAVU, WASIPOOKOKA WAFE

Ni zaidi ya mwaka sasa kumekuwa na  uchomwaji na mauaji juu ya watumishi wa Mungu wa Kikristo na kwa muda sasa wakristo wamekuwa wako kimya kuona hatua gani zinachukuliwa na serikali yetu ya Tanzania. baada ya kuona kuwa bado mambo hayo yanaendelea wachungaji wameamua kuvunja ukimya. ikumbukwe kuwa kumekuwa na matamko mbalimbali ya jumuiya za kikristo ili kuishinikisha serikali kuwachukulia hatua kali wale wote wanaohusika na vurugu hizi za kidini mpaka sasa kila kitu kimebaki kuwa kitendawili kisichoteguka huku baadhi wa wahamasishaji wakiendelea kurandaranda mitaani na huku wakiwa wamesababisha baadhi ya familia kuondokewa na wapendwa wao walio uliwa katika machafuko hayo.  lakini haijaishia hapo hivi karibuni watumishi mbalimbali walikutana na kujadili kwa pamoja na kufikia muafaka wa kufanya maombi ya pamoja kwa siku tatu mfululizo.

maombi hayo ambayo yataanza Tar 27 - 29 mwezi huu wa March utaratibu wa maombi hayo ni kila kanisa watafunga kwa masaa 24 kwa siku inamaanisha 3 kavu Jumatano na Alihamisi maombi yataishia makanisani na siku ya Ijuma kuu makanisa yote ya kipentekoste yatakuwa na ibada ya pamoja kuanzia asubuhi kwa kuhitimisha maombi hayo vituo vya maombi ni uwanja wa sabasaba PTA  na ATN Mbezi washirika wanaruhusiwa kwenda kati ya vituo hivyo viwili ambako ndiko kutahitimishwa maombi hayo, habari zilizoifikia blog hii zinasema wachungaji hao walitoa matamko makali na kusema kuwa katika maombi hayo yatakuwa ni ya kumwomba Mungu ili wote waliohusika na mchakato wa uchomaji wa makanisa na uuaji wasalimishe maisha yao kwa Yesu na kama wakifanya shingo zao kuwa ngumu basi kufa na wafe.

hivyo wakristo wote wameombwa kushiriki katika maombi hayo ili Mungu wa kweli akapate kujulikana na kuheshimiwa na kuabudiwa na watu wote. 

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

MBONA NIKITUMA MSG YA MAOMBI KWENYE BLOG YA MWL.CHRISTOPHER MWAKASEGE HAIENDI?