Jumapili, 10 Machi 2013

BAHATI BUKUKU MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI ANAYEPENDA MZIKI WA REGGER NA HUWA ANAIFANYIA HAKI

Katika waimbaji wa nyimbo za injili ambao ni mihimili ya waimbaji wa nyimbo za injili huwezi ukaacha kumtaja bahati Bukuku ambaye ametoa matoleo mengi ya albam, na ni kati ya waimbaji ambao wamefanikiwa kimaisha kupitia uimbaji. waimbaji wa nyimbo hizi za injili wamekuwa na uhuru wa kuimba aina yeyote ya mziki wanaotaka kama regger, zouk, sebene, segele, south, jazz, blues.mduara nk. leo namuangazia Bahati ambaye baada ya kufuatilia nyimbo zake nyingi nimegundua kuwa anapenda sana nyimbo za regger na hakuna hata albamu hata moja aliyotoa bila kuweka nyimbo za regger na kiukweli anazitendea haki.

huu ni wimbo ambao aliutoa katika albamu yake ya kwanza ya ni nyakati za mwisho na ni wimbo ambao ulimtambulisha vizuri sana katika ulimwengu wa mziki wa injili, wimbo huu uko katika mahadhi ya reggerUpo wimbo mwingine pia ambao ni maarufu sana na unakubalika sana na watu wengi nao ni mahadhi ya regger huu unaitwa waraka Naamani, huu wimbo ulipoingia ulikuwa unapigwa kila mahali na kweli bahati aliutendea haki

huu nao ni wimbo wa regger ambayo nao umekaa vizuri sana unaitwa lazima usamehe kwa mtu yeyote anayependa miziki ya regger atakubaliana na mimi kuwa miziki hii iko vizuri sana na zimetendewa haki.

Lakini si hivyo tu katika albamu mpya aliyotoa ya dunia haina huruma, kuna nyimbo mbili za Abinel na Ahabu ambazo nazo ukizisikiliza kwa kweli zipo katika kiwango cha kimataifa tafadhali tafuta uzisikilize

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: