Jumapili, 17 Februari 2013

PADRI WA KATOLIKI AUWAWA ZANZIBARTaarifa ambazo Tumezipata kupitia vyombo vya habari zinasema Padri Everist Mushi (Mushi) wa kanisa katoliki huko visiwani Zanzibar, amepigwa risasi ya kichwani na watu wasiojulikana na kufariki papo hapo asubuhi ya leo wakati akielekea kwenye ibada katika kanisa katoliki Mtoni Zanzibar.


Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kuwa watu hao waliofanya tukio hilo walikuwa wawili na walikuwa wamepakizana kwenye pikipiki aina ya Vespa wakati padri huyo alikuwa kwenye gari lake ambalo baada ya kutokea kwa tukio hilo nalo liliacha njia na kwenda kugonga nyumba moja iliyokuwa jirani na kanisa hilo.

Mpaka sasa haijajulikana sababu hasa ya kutokea kwa tukio hilo.   KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni